Tundu Lissu alonga mambo mhimu na makubwa juu ya yaliyotokea Kenya

Hivi Lissu sio wewe unayeshinda case mahakamani dhidi ya jamhuri kila leo? Huo sio uhuru unao ulilia?
Mbona hujasema mtazamo wako juu ya neno tume huru ya uchaguzi na maamuzi ya mahakama juu ya dosari na makosa ya IBEC ya kenya?
mkuu tume huru ipo ndani ya rasimu ya katiba moya ya warioba
 
Tundu Lissu ....hatuhitaji elimu ya umuhimu wa katiba mpya ...tunataka tuone Chadema inao mkakati huo na jinsi mnavyoutekeleza ....tatizo lenu mnafanya siasa za matukio ....hata hili la Kenya mtalifanya kama tukio then mtaendelea na maigizo yenu ya kila siku yasiyo na tija ...
Slaa aliileta hiyo katiba mpya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni lazima tukubali kumwaga damu ndio katiba mpya itapatikana
angalizo , viongozi pia wakubali kupoteza maisha kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo
 
Naunga mkono kupigania katiba mpya, mahakama huru, tume ya uchaguzi huru na tasisi zinazohusu siasa ziwe huru.

LAKINI LISSU AMEMUULIZA MWENYE CHAMA (LOWASSA) kuhusu kufurahia matokeo ya kesi!?

Maana CDM siku hizi ni Lowassa.
Mahakama ya Juu ya Kenya imetengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo na kuamuru urudiwe ndani ya siku 60.

Sisi wa CHADEMA tulimuunga mkono Uhuru Kenyatta na chama chake cha Jubilee, ambaye alitangazwa mshindi kwenye Uchaguzi huo.

Hata hivyo, uamuzi wa Supreme Court ya Kenya ni ushindi mkubwa kwa wapigania demokrasia kila mahali duniani na kwetu pia.

Uamuzi huo umetokana na Kenya kuwa na Mahakama iliyo huru na isiyokuwa na hofu, woga wala upendeleo katika utendaji wake wa haki.

Mahakama hiyo huru imetokana na Kenya kuwa na Katiba Mpya ya kidemokrasia ya mwaka 2010.

Katiba hiyo ilipunguza na au kudhibiti mamlaka ya Rais wa Kenya, na ilimaliza utawala wa kiimla uliodumu Kenya kwa karibu nusu karne.

Kwetu sisi uamuzi huu ni fundisho kubwa sana.

Tunahitaji demokrasia itakayoondoa utawala wa kidikteta katika Tanzania pia.

Tunahitaji Katiba Mpya itakayolinda haki za binadamu, kuleta utawala wa sheria na kuondoa utawala wa amri za majukwaani na bomoa bomoa.

Ili kupatikana kwa demokrasia hiyo, tunahitaji Katiba Mpya.

Katiba Mpya itakayopunguza na kudhibiti Urais wa Kifalme ambao umekuwa 'organizing principle' ya Katiba yetu tangu mwaka 1962.

Katiba Mpya itakayoiweka huru Mahakama ya Tanzania, ambayo leo haina hata Jaji Mkuu, na kuwatoa hofu majaji wetu.

Katiba Mpya itakayowawezesha watawaliwa kuwadhibiti na kuwaadabisha watawala, wanaojigeuza miungu watu mara wakishaingia madarakani.

Kwa hiyo, pamoja na kuwa urais uliotenguliwa ni wa mgombea tuliyemuunga mkono, hatuna budi kushangilia ushindi huu wa utawala wa sheria na uhuru wa mahakama.

Na, bora zaidi, hatuna budi kuyafanyia kazi mafundisho ya demokrasia ya Kenya: Katiba Mpya na ya kidemokrasia.

Katiba Mpya ya Kenya haikujileta. Ililetwa kwa jitihada, jasho na damu ya waKenya. Katiba Mpya ilipiganiwa, ilidaiwa na, baada ya kupatikana, imelindwa.

Na kwetu lazima iwe hivyo hivyo. Haitapatikana kwa kuombewa makanisani au misikitini tu. Itapatikana kwa kudaiwa mitaani na barabarani na Mahakamani na kila mahali.

Haitapatikana kwa vigelegele na vicheko. Itapatikana kwa vilio vya wanaodai haki na wanaokandamizwa.

Hebu na tujielekeze katika kazi ngumu na muhimu iliyoko mbele yetu. Kazi ya kudai Katiba Mpya.
 
Huyu TUNDU LISSU nina mashaka na msimamo wake,hii kum support UHURU-KENYA imeletwa CHADEMA na LOWASSA na bila kutumia akili CDM wakaingia kichwa kichwa mpaka kutoa tamko kama chama pale Dodoma,alipouwawa jamaa wa IT-MSANDO,Lissu hakuwahi toa maoni wala kulaani,aliposhinda UHURU alipongeza na kudai Kenya wamekomaa kidemokrasia,leo uchaguzi umebatilishwa analeta blah blah,mi huwa nasema mwanaume asiye na MSIMAMO hafai,haijalishi ni mwanasiasa au nani.Nashangaa mnaomuona LISSU kama HERO,ni mpuuzi fulani asiye na msimamo na dhambi ya kumchafua EL baadae kumpa nafasi ya ugombea uraisi na kumtukana Slaa baada ya kusisitiza msimamo itawatafuna CDM milele.Mtaji mliobaki nao kwasasa ni vijana wa mtandaoni basi.Mtaani mnaonekana wapiga dili tu,soon mtaamini maneno haya,hata muitishe maandamano leo haendi mtu,wananchi wanazidi kuwashtukia uongo wenu.
 
Nipo tofauti sana na ccm, lakini kwa hili nakuunga mkono.
Hivi Lissu sio wewe unayeshinda case mahakamani dhidi ya jamhuri kila leo? Huo sio uhuru unao ulilia?
Mbona hujasema mtazamo wako juu ya neno tume huru ya uchaguzi na maamuzi ya mahakama juu ya dosari na makosa ya IBEC ya kenya?
 
Mahakama ya Juu ya Kenya imetengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo na kuamuru urudiwe ndani ya siku 60.

Sisi wa CHADEMA tulimuunga mkono Uhuru Kenyatta na chama chake cha Jubilee, ambaye alitangazwa mshindi kwenye Uchaguzi huo.
...
Uamuzi huo umetokana na Kenya kuwa na Mahakama iliyo huru na isiyokuwa na hofu, woga wala upendeleo katika utendaji wake wa haki.

Mahakama hiyo huru imetokana na Kenya kuwa na Katiba Mpya ya kidemokrasia ya mwaka 2010.
...
Katiba Mpya ya Kenya haikujileta. Ililetwa kwa jitihada, jasho na damu ya waKenya. Katiba Mpya ilipiganiwa, ilidaiwa na, baada ya kupatikana, imelindwa.

Na kwetu lazima iwe hivyo hivyo. Haitapatikana kwa kuombewa makanisani au misikitini tu. Itapatikana kwa kudaiwa mitaani na barabarani na Mahakamani na kila mahali.
...

Lissu katika ubora wake wa kuropoka. CHADEMA mnahamasishwa kuingia barabarani kudai Katiba mpya, du!

Lissu ulikuwa wapi kudai hilo? Je, Mahakama ya Kenya ingetupilia mbali madai ya NASA, ungesema nini?
 
Hivi Lissu sio wewe unayeshinda case mahakamani dhidi ya jamhuri kila leo? Huo sio uhuru unao ulilia?
Mbona hujasema mtazamo wako juu ya neno tume huru ya uchaguzi na maamuzi ya mahakama juu ya dosari na makosa ya IBEC ya kenya?
Kuna Majaji wanaojitambua, na Katiba huru. Hakuna Tume huru. Tume ndio hiyo imechemsha had I uchaguzi unarudiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni mpya!

Leo CHADEMA wanashangilia mahakama kumpiga stop Uhuru Kenyatta ambaye wameshirikiana naye kuharibu uchaguzi!

Hii ni sawa na Unapelekwa mahakamani halafu ukishindwa unaanza kushangilia.
Tundu Lissu anafanya propaganda za kitoto na kijinga.

Kabla ya maamuzi ya mahakama walikuwa wanatuambia uchaguzi umefanyika katika hali huru na haki halafu leo wanatuambia tofauti ili kwenda na upepo wa kisiasa.

Hii inaonyesha ni jinsi gani chama hakina msimamo.
Kwa hapa mimi naungana na Lisu. Mahakama imetenda,ni jambo jema. Ukweli huu lazima usemwe. Bila kujali nani kashinda,lakini nguvu hiyo hapa kwetu haipo,hasa mambo ya uchaguzi mkuu. Tume ikitangaza basi!Hiyo ni dosari kubwa sana. Na ili kupata haki hiyo,ndipo umuhimu wa Katiba Mpya(siyo ile ya wachache inayopendekezwa)bali ile ya RASIMU YA 2 iliyoratibiwa na mzee Warioba. So kwa hapa Lisu yupo sahihi 100%
 
Hivi Lissu sio wewe unayeshinda case mahakamani dhidi ya jamhuri kila leo? Huo sio uhuru unao ulilia?
Mbona hujasema mtazamo wako juu ya neno tume huru ya uchaguzi na maamuzi ya mahakama juu ya dosari na makosa ya IBEC ya kenya?
Katiba mpya ndio suluhu..,Raisi wa Tanzania ana uwezo mkubwa sana,hata Nyerere aliwahi kuzungumza hayo,kama tunapata raisi dikteta basi anaweza kuipeleka nchi anavyotaka yeye bila ya kujali wengine,acha kubwabwaja..

Tuwasifu wakenya na mahakama kuu ya Kenya kwa walichokifanya,kuhusu dosari za IBEC ni yao wenyewe wewe hayakuhusu...,furahia mema kemea mabaya
 
Katiba mpya Tanzania itapatikana kwa damu sio kwa maneno. Watanzania tunatakiwa kuondoa woga na tuacheni unafiki. Tudaini katiba mpya kwa kuingia mitaani
Anza wewe na lisu kuingia mitaani kudai katiba wengine tutafuata siyo unapiga kelele tu hapa. Unahamasisha ila siku ikifika unajifungia nyumbani kwako ukichungulia dirishani wenzio wakivunjwa miguu. Shame on you Fanya kazi kwa ajili ya familia yako.
 
Kwa hapa mimi naungana na Lisu. Mahakama imetenda,ni jambo jema. Ukweli huu lazima usemwe. Bila kujali nani kashinda,lakini nguvu hiyo hapa kwetu haipo,hasa mambo ya uchaguzi mkuu. Tume ikitangaza basi!Hiyo ni dosari kubwa sana. Na ili kupata haki hiyo,ndipo umuhimu wa Katiba Mpya(siyo ile ya wachache inayopendekezwa)bali ile ya RASIMU YA 2 iliyoratibiwa na mzee Warioba. So kwa hapa Lisu yupo sahihi 100%
Mahakama nayo ikitangaza basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo, pamoja na kuwa urais uliotenguliwa ni wa mgombea tuliyemuunga mkono, hatuna budi kushangilia ushindi huu wa utawala wa sheria na uhuru wa mahakama.

lissu amewahi sana kutoa tamko hili, alitakiwa awe na subira. kwa tension iliyopo kenya kwa sasa, ni rahisi sana kutokea machafuko.

" life is a gamble, let flipism guide your ramble"
 
Hii ni mpya!

Leo CHADEMA wanashangilia mahakama kumpiga stop Uhuru Kenyatta ambaye wameshirikiana naye kuharibu uchaguzi!

Hii ni sawa na Unapelekwa mahakamani halafu ukishindwa unaanza kushangilia.
Tundu Lissu anafanya propaganda za kitoto na kijinga.

Kabla ya maamuzi ya mahakama walikuwa wanatuambia uchaguzi umefanyika katika hali huru na haki halafu leo wanatuambia tofauti ili kwenda na upepo wa kisiasa.

Nchi ya Kenya inaingia gharama nyingine ya uchaguzi kwa sababu ya ushirikiano wa CHADEMA na Uhuru Kenyatta ambao umesababisha uchaguzi kurudiwa.

Hii inaonyesha ni jinsi gani chama hakina msimamo.
Yani CHADEMA ni kama wamekufa kifikra hata hawaeleweki wanasimamia nini, wanapigania nini, wa moto au uvuguvugu au wamepoa kabisa ni wapowapo tu hawajitambui kwa sasa.
 
U
Katiba mpya ndio suluhu..,Raisi wa Tanzania ana uwezo mkubwa sana,hata Nyerere aliwahi kuzungumza hayo,kama tunapata raisi dikteta basi anaweza kuipeleka nchi anavyotaka yeye bila ya kujali wengine,acha kubwabwaja..

Tuwasifu wakenya na mahakama kuu ya Kenya kwa walichokifanya,kuhusu dosari za IBEC ni yao wenyewe wewe hayakuhusu...,furahia mema kemea mabaya
Huru alivyo tangazwa mlibwabwaja na kupiga makofi mengi Leo tena mnamuunga mkono Raila mkoje?????
 
Back
Top Bottom