Mahakama ya Juu ya Kenya imetengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo na kuamuru urudiwe ndani ya siku 60.
Sisi wa CHADEMA tulimuunga mkono Uhuru Kenyatta na chama chake cha Jubilee, ambaye alitangazwa mshindi kwenye Uchaguzi huo.
Hata hivyo, uamuzi wa Supreme Court ya Kenya ni ushindi mkubwa kwa wapigania demokrasia kila mahali duniani na kwetu pia.
Uamuzi huo umetokana na Kenya kuwa na Mahakama iliyo huru na isiyokuwa na hofu, woga wala upendeleo katika utendaji wake wa haki.
Mahakama hiyo huru imetokana na Kenya kuwa na Katiba Mpya ya kidemokrasia ya mwaka 2010.
Katiba hiyo ilipunguza na au kudhibiti mamlaka ya Rais wa Kenya, na ilimaliza utawala wa kiimla uliodumu Kenya kwa karibu nusu karne.
Kwetu sisi uamuzi huu ni fundisho kubwa sana.
Tunahitaji demokrasia itakayoondoa utawala wa kidikteta katika Tanzania pia.
Tunahitaji Katiba Mpya itakayolinda haki za binadamu, kuleta utawala wa sheria na kuondoa utawala wa amri za majukwaani na bomoa bomoa.
Ili kupatikana kwa demokrasia hiyo, tunahitaji Katiba Mpya.
Katiba Mpya itakayopunguza na kudhibiti Urais wa Kifalme ambao umekuwa 'organizing principle' ya Katiba yetu tangu mwaka 1962.
Katiba Mpya itakayoiweka huru Mahakama ya Tanzania, ambayo leo haina hata Jaji Mkuu, na kuwatoa hofu majaji wetu.
Katiba Mpya itakayowawezesha watawaliwa kuwadhibiti na kuwaadabisha watawala, wanaojigeuza miungu watu mara wakishaingia madarakani.
Kwa hiyo, pamoja na kuwa urais uliotenguliwa ni wa mgombea tuliyemuunga mkono, hatuna budi kushangilia ushindi huu wa utawala wa sheria na uhuru wa mahakama.
Na, bora zaidi, hatuna budi kuyafanyia kazi mafundisho ya demokrasia ya Kenya: Katiba Mpya na ya kidemokrasia.
Katiba Mpya ya Kenya haikujileta. Ililetwa kwa jitihada, jasho na damu ya waKenya. Katiba Mpya ilipiganiwa, ilidaiwa na, baada ya kupatikana, imelindwa.
Na kwetu lazima iwe hivyo hivyo. Haitapatikana kwa kuombewa makanisani au misikitini tu. Itapatikana kwa kudaiwa mitaani na barabarani na Mahakamani na kila mahali.
Haitapatikana kwa vigelegele na vicheko. Itapatikana kwa vilio vya wanaodai haki na wanaokandamizwa.
Hebu na tujielekeze katika kazi ngumu na muhimu iliyoko mbele yetu. Kazi ya kudai Katiba Mpya.