Tundu Lissu aanza mashambulizi upya!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu aanza mashambulizi upya!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bukanga, Apr 30, 2012.

 1. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge Tundu Lissu akihutubia mkutano viwanja vya stendi ya zamani mjini Singida, tangu mahakama kuu impe ushindi dhidi ya kesi
  [​IMG]
  Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack
  [​IMG]
  Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano
  [​IMG]
  Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu akimtolea mfano muuza maji mjini Singida kwa kutumia toroli, maarufu kwa jina la 'Chai
  Aprili 30,2012.
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili waikomboe nchi, kutoka kwa wezi na mafisadi wa fedha za umma.
  Mnadhimu mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye mkutano wa hadhara, aliufanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida, kwa lengo la kukiimarisha chama, bada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi.
  Lissu ambaye pia ni mbunge Singida mashariki, aliwashauri wajiondoe mapema, badala ya kung’ang’ania huko, kusubiri CHADEMA itawale nchi, halafu ndio wajitokeze kusema na wao ni wafuasi wa chama hicho.
  Pia aliwaomba viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hivi sasa wachukue tahadhari, vinginevyo watapata madhara makubwa, ikiwemo hata kupoteza maisha yao.
  Alisema kitendo cha kuuawa kwa mwenyekiti wao huko Usa river, mkoani Arusha na kukatwa katwa kwa panga wabunge wa CHADEMA mkoani Mwanza, ni onyo kwa wanachama na viongozi wa chama hicho.
  “Vita hii ni kubwa, lazima tuielewe, kuanzia sasa kaeni chonjo, vinginevyo CHADEMA tutauawa, mwenyekiti wetu kule Arusha amechinjwa na wabunge wetu huko Mwanza wamekatwa katwa mapanga, tena mbele ya polisi….tuangalie sana,”alitahadharisha Lissu.
  Kuhusu ushindi wa kesi iliyomkabili, ambayo ni moja ya mashauri 14 yaliyofunguliwa, kati ya majimbo 23 ya CHADEMA nchini, Lissu aliishukuru mahakama kumuona hana hatia, ingawa anaamini wadai wamepoteza fedha nyingi, zinazofikia zaidi ya Sh. Milioni 200, ili ubunge wake utenguliwe.

  Huo ulikuwa mkutano wa kwanza kufanyika Singida mjini na watatu kimkoa, tangu mahakama kuu, kanda ya Dodoma, kupitia Jaji Moses Mzuna wa Moshi, Mkoani Kilimanjaro, kufutilia mbali shauri la kupinga ubunge, alilofunguliwa na wanachama wawili wa CCM.

  Kwa hisani ya Mjengwa!

   
 2. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ndo wabunge makini,unashinda kesi unarudi kwa wananchi,na sio kushinda baa na vimada ukijipongeza,safi kamanda,sasa watumikie wananchi wako kwa nguvu zaidi,naamini ile tention ya kesi imeisha chapa kazi,2015 uwe waziri makini wa sheria na Katiba na upendekeze AG wa ukweli na sio mwenye mapenzi yz dharura!
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Asante, lakini hili la mauaji, linatisha sana....CDM wekeni kumbukumbu ya wale wote walipoteza maisha katika mapambano haya na CCM, ndio watakuwa mashujaa wenu siku mkiingia ikulu
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Akiwa waziri Apendekeze tuandike katiba mpya, hii tunayochakata sasa tunaelekezwa tuandikeje.
   
 5. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hata huyu Jaji atakua CDM, c mwenyeji wa Knjaro bana! Angekua ametokea Swanga kama yule aliyehukumu kesi ya Lema angepika majungu kama alivyopikiwa Lema!
   
 6. patriq

  patriq Senior Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  big up kaka,
  mungu amekupigania hongera sana. Sasa tuendeleze maendeleo kwa watu wetu. Lakini naomba kitu kimoja, kwa nguvu zote tushirikiane katika kutoa tamko na kulaani juu ya mauaji yanayofanyika kwa watu wetu. Chama tunakiomba kitoe tamko na kipendekeze suluhisho ili tujadili. Kama serikali imekwama sisi kama chama tupate solution ya kuiwajibisha serikali hata kimataifa. Tupe mwelekeo mkuu wa kisheria unasemaje katika ku deal na mambo kama haya
   
 7. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  mapambano yanaendelea na halali mtu hadi kieleweke!
   
 8. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Lissu, wanachadema tuko imara na tayari kwa mapambano ya aina yoyote. Wataua wachache, lakini wengi watabaki na watasonga mbele. PEOPLE'S POWER & MOVEMENT FOR CHANGE.
   
 9. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hongera tundu Lissu najua hao wanyiramba watakombolewa
   
 10. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Big up Jembe! Singida ninayoijua inahitaji dozz nzito sana hadi majirity watoke kwenye lepe la usingizi wa kudumu.
   
 11. m

  matawi JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hii ststement ni ya kimapinduzi hasa mfano mdogo Magamba kupitia policcm waliua vijana watatu wa chadema leo chama hakina hata balozi wa nyumba 10 kudadadeki
   
 12. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Watachinja wangapi??? kwasababu kwasasa zaidi ya 90% ya Watanzania wenye akili timamu hawataki kabisa kuusikia utawala wa CCM na ndiyo maana hawakumchagua kikwete mwaka2010 aombe Mungu tume ya Taifa ya uchaguzi ilifuata maagizo. Unachinja watu huku ukihubiri kwamba nchi ina amani, kikwete ninamchukia sana kuna mwana CCM alifariki mbeya kwa kupigwa aliagiza polisi wamtafute muuaji lakini huyu wa Arusha hajatoa tamko lolote.
   
 13. Fekifeki

  Fekifeki JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,161
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Historia itawahukumu tu, hawa mafedhuli wauwaji wa wanaotetea haki za wanyonge! Siku zote Mungu yu upande wa watenda haki(CDM)! Tusikate tamaa ndugu zanguni, tutashinda tu!
   
 14. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana kamanda wetu
   
 15. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  ... Hili jembe ni noma na nalifahamu toka enzi zile likifahamika kama "mwanasheria wa mazingira" likitetea wachimbaji wadogo wa madini! Lakini niseme tu kwamba lilini-let down lilivyomwaga chozi baada ya kushinda kesi ya ubunge. Kama mwanasheria wa mahakama kuu na mwanaharakati analia baada ya kupata haki yake, sisi vibajaji tutakuwa na hali gani huko mahakamani!? It was really a sad scene.
   
 16. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hivi haka kaneno 'banned' kana maana gani siku hizi?
   
 17. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hivi haka kaneno 'banned' kana maana gani siku hizi?
   
 18. M

  Masantula2012 Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba hata mimi nilishangazwa sana na Hapo kwenye rangi nyekundu. Kwangu mie niliipa tafsiri tatu; Moja ni kuwa hakuamini kuwa Jaji angelitolea kesi yake maamuzi hayo, Pili, Ni kuwa Machozi ilikuwa ni ishara ya furaha ya ushujaa na uadilifu wake lakini tafsiri ya tatu; ni kuwa alihitaji huruma ya wapiga kura wake na watanzania kwa ujumla kufuatia kuonewa kwake. Sasa ukiwa Mbunge, Mnadhimu Mkuu kambi ya Upinzani mjengoni, Mwanasheria na wakili wa mahakama kuu, msomi nguli wa sheria n.k, inatia shaka sana akilia. Ujasiri ni muhimu katika upambanaji. Lia hiyo ninaitegemea zaidi kwa yule anayeachiwa huru kwa kuwa alikuwa na makosa dhahiri shahri. SIO YEYE pliiiiiiiiz!!!. I was particularly disappointed waungwana!!!
   
 19. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wamekula kichwa mkuu wangu!!
   
 20. IFUNYA

  IFUNYA JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Mkuu ebu Washauri viongozi wa CDM wafike hata vijijini tunawahitaji msiishie mijini tu.
   
Loading...