Watu wengi wameingalia interview ya Lisu wakiwa tayari Na mitazamo yao moyoni . Hii imepelekea kuja na mitazamo mbali mbali.
Wapo waliongalia hard talk ile kama kampeni ya Lisu kwa ajili ya kugombea Urais 2020 . Na hapo ndipo walipofanya makosa . kati ya sasa na 2020 ni mbali mno , Lolote laweza kutokea kwenye Siasa. Ukiangalia kwa mtazamo huo unaweza kuona kama Lisu akulifanyia mema Jukwaa hilo... la hasha,nia ya Lisu kwenye hardtalk hiyo haikuwa kujijenga kwa ajili ya Urais 2020.
Wapo pia waliongalia kwa jicho la kichama , maana ya kama ni CCM basi aponde lolote litakalojadiliwa , kwa mtazamo huo pia utapelekea kupata picha tofauti na utaona Lisu amekosea ?. Kwa nini akueleza na mazuri yakiofanywa na JPM?
Wapo waliotazama kwa mtazamo wa chama kama Chadema, Hawa wamesifia na hata wengine bado waliona Lisu akutumia vyema jukwaa.. kwamba alitakiwa kutaja mambo mengi zaidi ya hapo.
Wapo waliongalia hard talk ile kwa mtazamo wa kufuatilia mambo ya siasa bila kujali chama wala suala la Uchaguzi. Hawa wameiona nia ya Lisu ya kuutangazia umma kile ambacho labda Lisu anaamini Dunia haijui.
Wapo pia watu ambao si watanzania bali ni wafuatiliaji wa karibu wa Siasa za Africa, hasa Misingi ya Demokrasia . Hawa wamepata kusikia toka kwa Mtanzania , tuhuma ambazo zinahitaji uchunguzi...
Yapo Mataifa na Mashirika mbalimbali ambayo nayo yametazama hardtalk kwa ajili ya kupata habari wanazozitafuta au kuthibitisha kile wanachokifahamu...
Je Ni Upi hasa Mtazamo wangu.
- Lisu pamoja na kuwa ni mtu anayetegemea kuja kugombea Urais kama akipendekezwa na chama chake alitaka kutumia fursa hii kuionyesha Dunia kuwa Tanzania ile ya amani na utulivu haipo tena. Sijui kama ni kweli au la yeye anajua?
- Lisu alitaka kuonyesha Dunia kuwa kwa sasa Tanzania mtu anaweza kupigwa Risasi mchana kweupe na bado FAIL la kesi yake likafungwa ndani ya mwaka bila jitahada zozote.Sijui kama ni kweli au la, Ili hili lijulikane serikali ina wajibu wa kufanya uchunguzi na kukanusha.
- Lisu alitaka kuonyesha Dunia kuwa mbunge aliyetakwa kuuwawa na watu wasiojulikana anaweza kunyimwa matibabu hata kama ni stahili yake. Sijui kama hili ni la kweli au la, Lisu anajua na serikali wanatakiwa kutoa majibu
- Lisu alitaka kueleza Dunia kuwa yapo mambo yanayohitaji uchunguzi wa kina kuhusu haki za binadamu yanayoendelea Tanzania. Sijui kama ni kweli au la , Lisu yeye anajua na serikali itawajibika kukanusha
- Lisu alitaka kueleza Dunia kuwa kuna kubanwa kwa Demokrasia kwenye Nchi ya Tanzania. Sijui hili kama ni la kweli?, Lisu anajua na Serikali itawajibika kukanusha
- Lisu alitaka kueleza dunia kuwa kuna mambo yanayofanywa kinyume na Katiba. Hili nalo serikali iatwajibika kukanusha
- Lisu alitaka kuonyesha Dunia kuwa kuna manunuzi yanafanywa nje ya kupitishwa na Bunge. Hili nalo serikali itawajibika kukanusha
- Lisu alitaka kuonyesha dunia kuwa kuna haki ambazo zipo kwenye Katiba kuhusu Uhuru wa mambo ya ndani ya mtu ambayo serikali inabidi kuyaheshimu. Hili nalo serikali inatakiwa kukanusha
Tatizo kubwa lililokuwepo kwenye kipindi kile ni Bw Stephen na Lisu kutaka kujadili mambo mengi wakati muda ulikuwa kidogo. Hii ilipelekea kwa Lisu kutokupewa muda wa kutosha wa kujieleza na Stephen kumkatiza na kuuliza maswali mengine ili kufikia lengo la maswali aliyotaka kumuuliza .
Sijui wewe uliangalia ukiwa na mtazamo Upi ? tujadili