*MASWALI MUHIMU YALIYOMTAABISHA TUNDU LISSU BBC HARD TALK*
Tofauti kubwa katika mahojiano haya ilikuwa ni kati ya mtangazaji anayeijua kazi yake na mpayukaji aliyejipanga kwenda kuzoa umaarufu kwa kuwazodoa viongozi wakuu wa nchi yake, kuidhalilisha nchi hake na hata kuwatusi wanasiasa wenzake.
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Rais Magufuli anasifika kwa kutekeleza sera alizoahidi ikiwemo kupambana na rushwa, kuongeza mapato, kuboresha huduma za kijamii n.k
LISSU: (Akionekana kuchanganywa na jinsi Mtangazaji anavyojua yanayojiri Tanzania) lakini pia tunajua anajenga uwanja wilayani kwao Chato (akificha kueleza kuwa kwa saaa kuna viwanja vya ndegw zaidi ya 15 vinajengwa Tanzania), mapato yalipanda ndio lakini baadaye yakashuka (jambo ambalo si la kweli kadanganya).
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Mimi nazungumzia masuala ya kujenga mfumo mzuri, nazungumzia kiongozi anayeahidi na kutekeleza, hata kwenye madini amepambana kuongeza kunuifa kwa nchi ndio maana ameanza mazungumzo na Barrick na wamekubaliana kuongeza mapato ya Tanzania.
LISSU: Barrick hawajatoa hata senti mpaka sasa.
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Mbona huonekani kushukuru kazi kubwa anayoifanya Magufuli tena katika sekta ambayo hata wewe kwa miaka mingi ulitaka mageuzi.Je, unaunga mkono harakati hizi?
LISSU: (Akikwepa swali) Nimekuwa kwenye harakati za kudai haki katika madini kwa miaka mingi.
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Wakati wewe unaonekana kusita kutambua mafanikio haya, baadhi ya wanasiasa wenzako wa upinzani wanahama na kujiunga na Magufuli wakitambua utekelezaji mzuri anaofanya.
LISSU: Wanahongwa!
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Wewe ni mwanasheria mwandamizi. Unaifahamu sheria vizuri kuliko mimi. Ni hatari sana kukurupuka na kudandia mambo serious pasipokuwa na uthibitisho au ushahidi thabiti wa unayoyasema.
Baadhi ya watu unaowatuhumu ni wapinzani wenzio na misimamo yao inakinzana na kukanusha madai yako kabisa.
LISSU: Wapigie simu.
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Mfano Lawrence Masha alikiwa Waziri wa Kikwete kabla ya kuhamia upinzani na kumpinga sana Magufuli lakini sasa amekuwa akimsifu na kutambua kazi yake!
Sasa unaituhumu Serikali ya Magufuli kwa mambo mengi mabaya (hata kwa mazuri yanayoonekana). Uko tayari kurudi nyumbani Tanzania kupambana na Magufuli?
LISSU: Hadi nitakapopona. Madaktari wakisema niko fiti tu, kesho yako nitapanda ndege kurudi (Mtangazaji anamtazama kama anachosema ni kweli).
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Utakuwa na ulinzi wowote?
LISSU: Serikali itawajibika kunilinda saa 24 (Mtangazaji akamstukia kama ni mzima. Kweli mlinzi wako ndiye utajaribu kumkandia hivyo).
MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Utalinda haki za mashoga na wanafunzi wa shule za msingi wasome wakiwa na mimba?
LISSU: Mashoga wana haki ya kutoingiliwa vyumbani mwao. Wana haki ya usiri. Wasichana wenye mimba wataendelea na shule.
MTNGAZAJI STEPHEN SACKUR: Nataka uweke wazi watu wasikie, Je, ukiwa .
mwanasiasa maarufu, siku ukiingia madarakani utafuta sheria hizi zinazoitwa kandamizi zinazozuia ushoga?
LISSU: Kama ni kandamizi na zinazoingilia faragha, na naamini ziko hivyo, nitazifuta (Mtangazaji anabaki kaduwaa, anaamua kuagana na Lissu na kumtakia kheri).
Sent using
Jamii Forums mobile app