Biashara kwa mtindo huu ni ngumu sana kwa ulimwengu wa sasa, Tangaza biashara ukiwa umeweka details zote
N40 bei gani, N50 bei gani, N70........
Mkuu ndio maana nimeweka namba zangu za simu na email kwa mdau yeyote ambaye yuko interested na product zetu anitafute, nitamjibu fasta.
mkuu naomba nitoe hoja zingine za ziada kama ifuatavyo,
Kwanza, kwanini sijaweka bei ni kwasababu kuna kitu kinaitwa
price instability. kuna wakati gharama za kodi na import duties itafanya bei za betri kupanda kila baada ya muda fulani na kuna wakati bei zinashuka. sasa nikiweka price list hapa kwenye uzi huu kuna wateja watakuja kunipigia simu mwaka mmoja baadaye wanataka bei ya N40 halafu nikiwatajia bei wataanza kusema mbona bei yako iko juu tofauti na na kwenye post ya JF.
Kumbe hawajui kwamba post ni ya muda mrefu na hali ni tofauti na sasa itakuwa mtihani kwa mtu wa sales kuanza kutoa sababu za kwanini bei zimepanda na kumshawishi tena mteja anunue betri kwa bei ambayo mteja hakujua.
Pili, kuna kitu kinaitwa
customer confidential. siri ya mteja na muuzaji. hii kitu tunazingatia sana kwa wateja wetu hatutangazi wateja wetu public na ndio maana nashauri mdau yeyote ambaye yupo interested na product yetu apige simu kuuliza au tuma email ntakujibu fasta.
Tatu kuna
competitors yaani
wapinzani wetu, kama exide,Atlas, puma na wengineo mbona wao bei zao hawatangazi hadharani na sijui kama nimewahi kuona matangazo yao lakini wapo mtaani wanafanya biashara kama kawaida.
kwahiyo wadau wawe free, wapige simu ntawapa bei za betri au njoo ofisini tuzungumze biashara.