Tunaweza kuwaepuka wahindi?

Bethlehem

Member
Feb 24, 2019
44
54
WAHINDI (INDIANS)
Tunaweza kuwaepuka?

Kwanza kabisa ninawasalimu sana.

Pili naomba niwalete kwenye mada iliyobeba kichwa cha habari hapo juu kuwa TUNAWEZA KUWAEPUKA WAHINDI?

.........................

Wahindi ni akina nani?

Wahindi ni jamii ya watu ambao asili yao hasa ni huko bara Hindi, INDIA.

Ni moja ya jamii ambazo zimesambaa sana duniani, hapa Afrika na Tanzania kiuhalisia ni Takribani hakuna mtu asiyemjua MHINDI, ni kwasababu tunao wengi na kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi katika nchi yetu.

Kwa Taarifa yako sio Tanzania tu, hata Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika Kusini, Ulaya na Hata Amerika wamejazana.

Kule MAREKANI kuna JIMBO linaitwa INDIANA, huko pia wanaoishi kwa asili kabisa ni Wahindi (Red Indians) ambao inasemekana kuwa ndio watu wa kwanza kabisa kuishi Marekani.

Kwasasa Dunia inashuhudia idadi kubwa sana ya wahindi ambao wanaongezeka kwa kasi sana, wanazaliana mno kwani kwa mujibu wa takwimu za ongezeko la watu duniani, India inaongoza kwa kuwa na kasi ya ongezeko.

Kwasasa India ina watu takribani Bilioni mbili nyuma ya china huku ikitarajiwa kuipiku china miaka kumi ijayo.

Sifa kuu ya Wahindi ni Biashara, hawa ni wataalamu wa Biashara kwa asili.

Inaaminika kuwa wahindi ni moja ya jamii tatu duniani ambazo kibiashara ziko vizuri.

Wakati wa ukoloni, Waingereza kokote walikotawala walienda na Wahindi na kuwakabidhi kitengo cha biashara.

Hapa Tanzania wakati wa Uingereza kutawala wahindi walijazana kote Bara mpaka Visiwani, Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa wakati huo ilikuwa mtu akifika kariakoo yote Mnazi Mmoja mpaka Posta angeweza akahisi yuko Bombay India kwa jinsi wahindi walivyo wengi.

Hata wakati Sultan akiwa anatawala eneo la mwambao wa Afrika Mashariki alikuja na wahindi na walijazana vilevile wakiendesha eneo la Biashara.

Kwa maana hiyo Wahindi hutakiwi kushindana nao kibiashara, unapaswa kuwa mshirika wao.

Kwa taarifa yako tu, Wahindi ni wataalam wa biashara za kimataifa kwani yeye kuingia Uingereza, China,Marekani na kokote kwa ajili ya Biashara ni kawaida mno, na huko kote walishatengeneza mtandao (partnership) kwa muda mrefu sana. Kama huamini mtafute Marehemu Idd Amin Dadaa aliyekuwa Rais (Dikteta) wa Uganda miaka ya 70 na 80.

Idd Amin kwa chuki zake dhidi ya Waingereza na Wahindi aliamua kutangaza kuwaondoa wahindi Uganda,

Aliwapa siku chache sana za kuiachia ardhi ya Uganda huku wakipangiwa vitu vya kuondoka navyo,

Kampala iligeuka vilio kwa wahindi waliokuwa wamejazana wakitakiwa kuondoka na kuacha mali zao.

Baadhi ya waganda pia waliumia kwani kupitia kwa uwepo wa Wahindi nao walikuwa wanaendesha maisha yao. (Katazame Movie inaitwa MISSISIPI MASALA).

Wahindi waliondoka Uganda kweli, lakini cha ajabu hawakukosa pa kwenda na ni wachache sana walirudi India,

Wengi walielekea Marekani na Uingereza.

Huko Uingereza walijazana kwenye mtaa ambao hii leo ni kituo kikubwa sana cha kibiashara ambacho kilianzishwa na hao waliotimuliwa na Amin, japo waliondoka bila mitaji, ujuzi wao wa biashara waliubeba kwenye vichwa vyao.

Baada ya Idd Amin kuwafukuza kilifuata kipindi cha mdororo wa uchumi kwani hata mazao ya kilimo yalishuka bei kwani wasafirishaji wakubwa wa mazao hayo kwenda nje walikuwa ni Wahindi.

Bidhaa muhimu zilikuwa haziingii Uganda maana Wahindi ndio walikuwa waingizaji wakuu. Hata zilipoingia nyingi zilikuwa fake na sio Jiniani (genuine) kama wanavyosema wahindi wenyewe.

Hapa Tanzania tunao wahindi wengi pia, wakati mwingine wamekuwa wakihusishwa kwenye biashara zenye Rushwa lakini ukweli ni kwamba kitengo cha Biashara wanakijua na wamekishikilia kwa miaka mingi sana tangu ukoloni mpaka sasa.

Nawasikiaga tu akina Patel, Dewji, Manji, Maza n.k.

Hawa wanajua pa kuipeleka Korosho, Mbaazi, Yanga, Simba, Pilipili, Tangawizi, Mihogo n.k. ( Tumewatikisa nini?)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika kusoma kwangu koteeee kuanzia darasa la kwanza hadi la nne sijawahi kulisoma bara la hindi mkuu ni bara jipya?
 
Unaanzaje kuwaepuka Wahindi?
Wamewashika kila upande.
Juzi kuna mwenzenu kaanzisha uzi analialia eti kwanini Wahindi ndo maboss maofisini nikamwambia kwa akili zenu hizi watu weusi Wahindi wataendelea kuwatawala na kuwarukisha kichura chura.
Dewji ana 49% ya hisa ndani ya simba lakini yeye ndiye kila kitu pale na siku akijitoa simba watalia vilio vya kila rangi.
Live long Bharat the land of river Jelum.
Live long Bharatians.
 
Katika kusoma kwangu koteeee kuanzia darasa la kwanza hadi la nne sijawahi kulisoma bara la hindi mkuu ni bara jipya?
Eneo lote la India,Pakistan,Sri lanka na Bangladesh utambuliwa kama bara hindi hata kwenye Biblia imeandikwa "mfalme Ahasuero alitawala maeneo yote ya Babeli,Kush mpaka bara hindi"
Kitabu cha Esta sura ya 1.
Usiogope dunia ina mabara saba.
 
Waafrika tatizo ubaguzi unaanzia serikalini na Africa haitaendelea kamwe kwa sababu inawaonea wivu badala ya kuwaiga na kushindana nao kibiashara.

Daima kama serikali zinawabagua na wananchi watawachukia tu kwa sababu akili hakuna
Angalia leo UK mayor of London ni muislam na asili ya Asia
Waziri wa mambo ya ndani ni mapkistan pia na muislam sasa kwetu kinana kashambuliwa sana wakati ni mtoto wa hapo
Halafu mleta ungenipa namba ya simu ya Idd Amin maana umelisema hilo
Na population of India is 1.3b and not 2b

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Kulanzenze

Sasa hilo bara Hindi ni la nane ama?
 
Sasa hilo bara Hindi ni la nane ama?

Mkuu, ni hivi kwenye kiingereza inaitwa the Indian Sub-continent, yaani nusu bara. Hii ni kwa sababu imezungukwa na bahari sehemu tatu na kufungwa juu na Himalaya Range. Kwa sababu imejiwekea pekee, imepata sifa ya sub-continent, lakini bado inahesabika kama sehemu ya bara la Asia.
 
Sasa hilo bara Hindi ni la nane ama?
Isikupe taabu eneo hilo limekuwa termed hivyo kwa sababu ya ukubwa wake.
It is big worth a continent.
Kwa mfano eneo la kinondoni limepewa adhi ya mkoa wa kipolisi japo kijiografia sio mkoa.
Umenielewa ndugu?
 
Unajua maana ya mkoa wa kipolisi au unakurupuka? Sema upewe darasa
 
WAHINDI (INDIANS)
Tunaweza kuwaepuka?

Kwanza kabisa ninawasalimu sana.

Pili naomba niwalete kwenye mada iliyobeba kichwa cha habari hapo juu kuwa TUNAWEZA KUWAEPUKA WAHINDI?

.........................

Wahindi ni akina nani?

Wahindi ni jamii ya watu ambao asili yao hasa ni huko bara Hindi, INDIA.

Ni moja ya jamii ambazo zimesambaa sana duniani, hapa Afrika na Tanzania kiuhalisia ni Takribani hakuna mtu asiyemjua MHINDI, ni kwasababu tunao wengi na kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi katika nchi yetu.

Kwa Taarifa yako sio Tanzania tu, hata Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika Kusini, Ulaya na Hata Amerika wamejazana.

Kule MAREKANI kuna JIMBO linaitwa INDIANA, huko pia wanaoishi kwa asili kabisa ni Wahindi (Red Indians) ambao inasemekana kuwa ndio watu wa kwanza kabisa kuishi Marekani.

Kwasasa Dunia inashuhudia idadi kubwa sana ya wahindi ambao wanaongezeka kwa kasi sana, wanazaliana mno kwani kwa mujibu wa takwimu za ongezeko la watu duniani, India inaongoza kwa kuwa na kasi ya ongezeko.

Kwasasa India ina watu takribani Bilioni mbili nyuma ya china huku ikitarajiwa kuipiku china miaka kumi ijayo.

Sifa kuu ya Wahindi ni Biashara, hawa ni wataalamu wa Biashara kwa asili.

Inaaminika kuwa wahindi ni moja ya jamii tatu duniani ambazo kibiashara ziko vizuri.

Wakati wa ukoloni, Waingereza kokote walikotawala walienda na Wahindi na kuwakabidhi kitengo cha biashara.

Hapa Tanzania wakati wa Uingereza kutawala wahindi walijazana kote Bara mpaka Visiwani, Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa wakati huo ilikuwa mtu akifika kariakoo yote Mnazi Mmoja mpaka Posta angeweza akahisi yuko Bombay India kwa jinsi wahindi walivyo wengi.

Hata wakati Sultan akiwa anatawala eneo la mwambao wa Afrika Mashariki alikuja na wahindi na walijazana vilevile wakiendesha eneo la Biashara.

Kwa maana hiyo Wahindi hutakiwi kushindana nao kibiashara, unapaswa kuwa mshirika wao.

Kwa taarifa yako tu, Wahindi ni wataalam wa biashara za kimataifa kwani yeye kuingia Uingereza, China,Marekani na kokote kwa ajili ya Biashara ni kawaida mno, na huko kote walishatengeneza mtandao (partnership) kwa muda mrefu sana. Kama huamini mtafute Marehemu Idd Amin Dadaa aliyekuwa Rais (Dikteta) wa Uganda miaka ya 70 na 80.

Idd Amin kwa chuki zake dhidi ya Waingereza na Wahindi aliamua kutangaza kuwaondoa wahindi Uganda,

Aliwapa siku chache sana za kuiachia ardhi ya Uganda huku wakipangiwa vitu vya kuondoka navyo,

Kampala iligeuka vilio kwa wahindi waliokuwa wamejazana wakitakiwa kuondoka na kuacha mali zao.

Baadhi ya waganda pia waliumia kwani kupitia kwa uwepo wa Wahindi nao walikuwa wanaendesha maisha yao. (Katazame Movie inaitwa MISSISIPI MASALA).

Wahindi waliondoka Uganda kweli, lakini cha ajabu hawakukosa pa kwenda na ni wachache sana walirudi India,

Wengi walielekea Marekani na Uingereza.

Huko Uingereza walijazana kwenye mtaa ambao hii leo ni kituo kikubwa sana cha kibiashara ambacho kilianzishwa na hao waliotimuliwa na Amin, japo waliondoka bila mitaji, ujuzi wao wa biashara waliubeba kwenye vichwa vyao.

Baada ya Idd Amin kuwafukuza kilifuata kipindi cha mdororo wa uchumi kwani hata mazao ya kilimo yalishuka bei kwani wasafirishaji wakubwa wa mazao hayo kwenda nje walikuwa ni Wahindi.

Bidhaa muhimu zilikuwa haziingii Uganda maana Wahindi ndio walikuwa waingizaji wakuu. Hata zilipoingia nyingi zilikuwa fake na sio Jiniani (genuine) kama wanavyosema wahindi wenyewe.

Hapa Tanzania tunao wahindi wengi pia, wakati mwingine wamekuwa wakihusishwa kwenye biashara zenye Rushwa lakini ukweli ni kwamba kitengo cha Biashara wanakijua na wamekishikilia kwa miaka mingi sana tangu ukoloni mpaka sasa.

Nawasikiaga tu akina Patel, Dewji, Manji, Maza n.k.

Hawa wanajua pa kuipeleka Korosho, Mbaazi, Yanga, Simba, Pilipili, Tangawizi, Mihogo n.k. ( Tumewatikisa nini?)

Sent using Jamii Forums mobile app
Lkn rostam sio muhindi na Tz hatuwezi kumkwepa huyu mtu. Dadeki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom