Katibu mkuu wa CUF amebainisha mbinu chafu za CHADEMA za kuiua CUF na kuhatarisha amani ya nchi. Akieleza kuwa CHADEMA ndio wachochezi wakubwa wa mgogoro wa CUF. CHADEMA wamekuwa na vikao mbalimbali na wasaliti wa CUF na kutoa matamko mbalimbali yenye lengo la kuhujumu CUF.
Lengo kubwa la CHADEMA wanahisi wakiua CUF, CHADEMA watashamiri. CUF ipo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa kwa kanuni namba 5 ya uanzwishaji wa vyama vya siasa inayokataza chama kimoja kutumia nguvu iliyonayo ya pesa, dola kuingilia chama kingine.Hivyo washaripoti kwa vyombo vya dola na msajili wa vyama.
My take
Kwa kuwa CHADEMA imekiuka sheria ya uanzishwaji wa vyama vya siasa kanuni ya 5 kwa kuingilia kwa wazi chama cha CUF na kuhatarisha amani ya nchi ningeomba msajili wa vyama aangalie ni jinsi gani anaweza kuiadhibu CHADEMA ikiwezekana kukifutia usajili kwani wamekiuka sheria ili iwe fundisho kwa vyama vingine.