Tunawataka waje: CUF wa Lipumba yawatambia CHADEMA

Tunawataka waje: CUF wa Lipumba yawatambia CHADEMA

Hivi huyu mama kakubali kutumika hivi?? yaani leo hii anawaona chadema wanatala kuiua CUF anasahau walivyobebwa na chadema huku bara hadi wakafanikiwa kupata wabunge wengi wa kuchaguliwa kuliko hata chadema then leo hii anawaona wanataoka kuimaliza cuf??? hivi kweli cuf ni threat kwa chadema!!! yaani chama ambacho bara hakijawahi fikisha wabunge hta wa5 ndio chadema kitumie nguvu nyingi kukimaliza??? kwa angesema maalim ningemuelewa maana kwa zenji haina mjadala kuwa cuf ndio kila kitu!!!!

Hawa hawajielewi wanashindwa kuona kiini cha mgogoro ni mtu kususa afu baadae anarudi kwa mabavu !! kma wangekuwa na busara wangemwambia arudi wakati wa uchaguzi ili ashinde kwa kishindo haya yote ya kuvamia ofisi cjui kumtimua seif ndio lawama zije chadema?? kwani lipumba alifukuzwa chamani au alijiondoa mwenyewe???
lipumba mchakato wake wa kujiuzulu haukukamilika according to katiba ya cuf
 
Chadema kinataka kukiua CUF ili kibakie kama chama kikuu cha upinzani hapa Tanzania. Kwa kufanya hivyo mtaji wa ruzuku utaongezeka. Ni biashara kama nyingine. Unaua duka la mwenzako ili wewe uuze.
 
Bila shaka programu zimegoma kichwani. Magdalena Sakahela si Katibu Mkuu wa CUF.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
ni huyu na maftah ndio wanafiki kwenye siasa wa tz na wanatumika pia
Inasemekana Sakaya amedhulumiwa hela iliyolipwa na ccm , kama shukrani kwa kujaribu kuvuruga cuf , yule jamaa yao anayeitwa Malima ni dhulumati hatari !

Huyu mama mimi binafsi nilishamtahadharisha kwa kutumia uzi wangu hapa jf, muacheni akomeshwe .
 
Chadema kinataka kukiua CUF ili kibakie kama chama kikuu cha upinzani hapa Tanzania. Kwa kufanya hivyo mtaji wa ruzuku utaongezeka. Ni biashara kama nyingine. Unaua duka la mwenzako ili wewe uuze.
Uongo utakusaidia nini ? Lipumba anang'oka kudadeki ! Kambaya kisharudi kuuza genge tandale , ccm ni wabaya sana !
 
Uongo utakusaidia nini ? Lipumba anang'oka kudadeki ! Kambaya kisharudi kuuza genge tandale , ccm ni wabaya sana !
chadema ndo wabaya hasa mfanya biashara mbowe anataka kuiua cuf ili kuongeza mtaji wa ruzuku
 
Inasemekana Sakaya amedhulumiwa hela iliyolipwa na ccm , kama shukrani kwa kujaribu kuvuruga cuf , yule jamaa yao anayeitwa Malima ni dhulumati hatari !

Huyu mama mimi binafsi nilishamtahadharisha kwa kutumia uzi wangu hapa jf, muacheni akomeshwe .
acha kuwa muongo mbowe na chadema ndo wabaya wanampango wa kuiua cuf
 
Lakini kusema ukweli, hili la CHADEMA kutangaza (kupitia kwa Kubenea - Muzee ya Shanga) operation dhidi ya CUF halijakaa sawa na wala halipendezi.
Ingekuwa ni tangazo la operation dhidi ya CCM ingeeleweka vizuri tu.
 
CUF hakuna mgogoro..kuna mission ya kuiangamiza ikiongozwa na taasisi kushirikiana na lipumba..KISA KIKUU NI ZANZIBAR
 
Wadau, kimsingi kwa mtu yeyote ambaye ni mdau wa demokrasia, hawezi kufurahia kuona migogoro ndani ya vyama vya siasa ambayo inatishia kuviua vyama hivyo. Kwa mantiki hiyo, umefika muda sasa wa wadau wa demokrasia kuwasaidia CUF kupata suluhu ya mgogoro unaowakabili. Aidha, kwa kuwa CUF ni chama cha upinzani, vyama vingine vya upinzani vina jukumu la kuwasaidia CUF kufikia Suluhu kuliko mtu mwingine yeyote.

HATARI ILIYOPO KAMA MGOGORO HUU UTAENDELEA KAMA ULIVYO;
Ikiwa, mgogoro huu utaendelea kama ulivyo bila kusuluhishwa kwa njia za kidiplomasia, madhara ya fuatayo yanatarajiwa kujitokeza.
1. Kuzidi kwa chuki miongoni mwa wana CUF wenyewe kwa wenyewe hasa chuki kati ya wana CUF wa zanzbar/ pemba dhidi ya wale wa Bara.

2. Kuzidi kwa chuki ambayo haiwezi kuwa na faidia kwa yoyote kati ya Prof. Lipumba na Maalim.
3. Kwa upande mmoja CUF ya maalim Seif itakufa kwa kukosa uungwaji mkono wa kitaasisi na kisheria (kutokana na position ya mgogoro kwa sasa) na kwa upande mwingine CUF ya Lipumba itakufa vile vile kwa kukosa uungwaji mkono wa kutosha Zanzibar lakini pia kwa kukosa "Cause and Purpose" bara. kwa hiyo wakiendelea hivi matokea yanatarajiwa kuwa "Zero sum game" kwa pande zote.

NINI CHA KUFANYA;
Kwa kuanzia,
1.Tunaziomba pande zote (Maalim na Prof. Lipumba) kwanza waache kutoleana kauli kali na za kuudhi ambazo zitaendelea kuleta uhasama.

2. Maalim aitishe vyombo vya habari akiwa pemba na kueleza wafuasi wake kuwa yuko tayari kufikia maridhiano na prof. Lipumba na Lipumba aitishe Press Dar akieleza utayari wake wa kufikia maridhiano na Maalim.

3. ACT (kwa sababu wanaweza kuaminika na pande zote), wawasaidie CUF kuwatafutia msuluhishi ambaye anaaminika na pande zote ambaye kwa haraka sana ataita wajumbe wa pande zote na kuanza hatua za maridhiano, kwa kuangalia uwezekano wa Lipumba kuendelea kuwa Mwenyekiti na Maalim kuwa Katibu kama ilivyokuwa awali.

MSULUHISHI
Napendekeza Msuluhishi awe ni Shekhe, Maalim Ally Basalleh wa dar es salaam. Hii ni kwa sababu kwa sasa kitu pekee kinachowaunganisha Lipumba na Seif ni dini, wote wanamfahamu vizuri Basalleh na wamekuwa wakiswali nyuma yake mara kwa mara. Aidha Shekhe basalleh ni msomi, mtu mzima, muelewa na mwenye busara kubwa sana.Naamini suluhu itafikiwa.

Nawatakieni suluhu njema.
 
Lipumba kapumbazika

Sent from my HUAWEI VNS-L21 using JamiiForums mobile app
 
Hapo majuzi viongozi na wanachadema walianzisha operesheni maalum ya kuihujumu CUF.

Hili sio jambo la busara katika siasa za nchi.

Hapa chama Chadema kinafanya uharamia na uonevu wa wazi dhidi CUF.

CHADEMA imetangaza rasmi kuhujumu na kuingilia mambo ya ndani ya chama cha CUF.

CUF hawatakiwa kusema tu bali wachukue hatua stahiki kwa msajili wa vyama dhidi ya Chadema.

Hebu imagine leo hii CCM itangaze operesheni maalumu ya kuondoa mafisadi na wakwepa kodi ndani ya Chadema ingakuwaje?
 
lipumba pumba

sent from aifoni seveni plasi
Kwa mtu ambaye angependa kuiona CUF ikiendelea kuwepo, huu sio muda wa kulaumiana tena, ni muda wa kila upande kukubali kuwa yaliyotokea yametokea basi. Sasa what is the way foward.
 
Back
Top Bottom