Tunawataka waje: CUF wa Lipumba yawatambia CHADEMA

Tunawataka waje: CUF wa Lipumba yawatambia CHADEMA

Hivi mbona mnawatafuta sana chadema? Yaani hata walitulia mnawatifua tu ili mradi polisi ikawakamate viongozi wao na kuwapa kesi . Mungu anawaona
Chadema Ndio waliotangaza kumng'oa Lipumba kwenye ofisi za CUF kwasababu ya kulinda UKAWA...... badala ya kuhangaika na madiwani wao wanaonunuliwa kila leo wanahangaika na CUF isiyowahusu.
 
Chanzo cha yote haya ni kumkumbatia fisadi,Loh mnaumbuka sasa..!!Si muwaache CUF wajiamulie mambo yao,na 2020 wanaweka mgombea safi asiye na Kashfa nyie bakieni hapo hapo na huyo huyo Muone cha mtema kuni hatafikisha hata 10% ya kura..!Mnisamehe lakini kwa ukweli mchungu.!
 
Kitendo cha CHADEMA kutangaza operation ya kumuondoa Lipumba Buguruni ni kitendo cha ajabu na kinapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa wapenda demokrasia nchini. CUF ni chama halali kabisa na chenye usajili wa kudumu na katiba yao inayojitegemea hivyo kinapaswa kujiamulia mambo yake bila kuingiliwa. Kitendo cha CHADEMA kuingilia mambo ya CUF kwa kigezo cha ukawa ni kuminya demokrasia na haki za wanacuf kwani ukawa sio chama bali ni mwamvuli hivyo kila chama kinatakwa kufata katiba yake.

Kitendo cha CHADEMA kuingilia mgogoro ambao upo mahakamani ni kinyume cha sheria na kinahatarisha uvunjifu wa amani hivyo msajili wa vyama inabidi aliangalia hili ikiwezekana aionye CHADEMA kutojihusisha na mgogoro huo.

Mwisho muda wanaoupoteza kuingilia mambo yasiyowahusu bora wapambane kukikomboa chama kutoka kwa mbowe ambaye anatumia chama kwa maslai binafsi ajali hata chama kinaelekea kufa kwani madiwani wanawakimbia wamechoshwa na unafiki wa CHADEMA.
 
Chadema inawauma nini Lipumba kukalia ofisi?

au lengo lao wanataka waiteke ofisi wamtimue prof then wahamie wao kwa mgongo wa Ukawa?

kumbe amekalia ofisi ndo mtaji wake
 
Chanzo cha yote haya ni kumkumbatia fisadi,Loh mnaumbuka sasa..!!Si muwaache CUF wajiamulie mambo yao,na 2020 wanaweka mgombea safi asiye na Kashfa nyie bakieni hapo hapo na huyo huyo Muone cha mtema kuni hatafikisha hata 10% ya kura..!Mnisamehe lakini kwa ukweli mchungu.!

alipokumbatia fisadi walipata wabunge wangapi?
 
Chadema Ndio waliotangaza kumng'oa Lipumba kwenye ofisi za CUF kwasababu ya kulinda UKAWA...... badala ya kuhangaika na madiwani wao wanaonunuliwa kila leo wanahangaika na CUF isiyowahusu.
Mkuu walitangaza lini? Mimi sijasikia hilo.
 
Tunawataka waje

Sent from my iPhone 8 using JamiiForums mobile App
 
Mkuu walitangaza lini? Mimi sijasikia hilo.

CHADEMA wameanzisha operesheni maalum ya kumwondoa Profesa Ibrahimu Lipumba, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) katika chama hicho imezinduliwa leo, anaandika Irene David.

Oparesheni hiyo iliyopewa jina la “Operasheni Ondoa Msaliti CUF (OBM) imezinduliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kushirikiana na viongozi wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu mkuu wa CUF.

Maamuzi hayo yalifikiwa jana baada ya kikao cha pamoja kilichofanywa na viongozi wa Chadema Kanda ya Pwani na viongozi wa CUF kujadili mgogoro ndani ya CUF na mstakakbali wa chama hicho na vyama vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Saed Kubenea, Makamu Mwenyekiti Kanda ya Pwani ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo (Chadema) amesema: “Sisi kama Chadema kwa umakini kabisa tutawasaidia viongozi wa CUF na wanachama wao kumwondoa msaliti Prof. Lipumba Buguruni.”

“Katika hili pia tumeamua kila siku ambayo kesi ya CUF inaendeshwa mahakamani wanachadema tutajitokeza kuisindikiza CUF tunayoitambua; tumekubaliana Mameya wetu wote wa jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa mtu yeyote wa vimelea vya Lipumba.”

Kwa upande wake Dkt. Makongoro Mahanga, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Dar es Salaam amesema: “Chadema ni washirika wa CUF katika Ukawa. Hivyo tunaamini wanavyoyumbishwa CUF hata sisi hatuwezi kubaki sarama.”

“Tumeona tunaathirika. Makao makuu ya Chadema na CUF yapo katika kanda yetu. Tumejiridhisha kwamba mgogoro si kati ya Lipumba na Seif, ni kati ya dola. Tumeamua kupambana na dola kwa kuanza na hawa wasaliti wakiongozwa na Lipumba.”

Aidha, Riziki Ngwali, Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa Wabunge wa CUF bungeni, amesema “Tunataka pia Watanzania watambue kuwa mgogoro wa dola dhidi ya CUF ni wa kupandikizwa. Kwa sababu vyombo vyake vinatumika.”
 
alipokumbatia fisadi walipata wabunge wangapi?
Swali hili nenda ufipani utapata jibu.Ila kwa sasa waTZ wameelewa utendaji kazi wa mzee wa Hapa kazi tu.Sasa nyie endeleeni kuwa na vichwa vigumu kutuletea kumbukumbu mbaya za ufisadi ndo mtajua kilichomtoa kanga manyoya..!!
 
Ninachokiona ni kwamba Le Polopesa na genge lake wameanza kuogopa kivuli chao wenyewe na wanaweweseka sasa ndio wanatafuta wa kufa nae!!
 
we unashangaa chadema kutangaza hayo,ki ukweli hasa matangazo kama hayo yalikuwa yatolewe na vyama vyote vya upinzani, taasisi za binafsi na watanzania wote wanaojifahamu, ili kukomesha na kuondoa mtiririko wa uvunjwaji wa sheria za nchi hii ambao unafanywa kwa manufaa ya kikundi cha watu wachache
 
Swali hili nenda ufipani utapata jibu.Ila kwa sasa waTZ wameelewa utendaji kazi wa mzee wa Hapa kazi tu.Sasa nyie endeleeni kuwa na vichwa vigumu kutuletea kumbukumbu mbaya za ufisadi ndo mtajua kilichomtoa kanga manyoya..!!

nafsi yako usiijumuishe na za wenzio watanzania wapi hao? ufipani ni makao makuu ya cuf acha kupanic tulia

ulivyo mweupe kichwani hadi muda huu chama kipi wanachama wake wanaongozwa kuchunguzwa na takukuru kwa wizi!!!!

ufisadi upo ndani ya damu ya ccm bado mapapa mawili yanalindwa na katiba mmoja alienda kuzindua nyumba chatuuuuuu
 
we unashangaa chadema kutangaza hayo,ki ukweli hasa matangazo kama hayo yalikuwa yatolewe na vyama vyote vya upinzani, taasisi za binafsi na watanzania wote wanaojifahamu, ili kukomesha na kuondoa mtiririko wa uvunjwaji wa sheria za nchi hii ambao unafanywa kwa manufaa ya kikundi cha watu wachache
Huyu ni CCM anafurahia sana CUF ikifa.
 
Hao akina lipumba chadema wapuuzeni tu maana wanatafuta kick kwa pikipiki
 
Sasa unadhani watu wasipo ingilia kati huu mgogoro utaisha vp na cuf imekuwa vyama viwili vinavyo tumia jina moja so nikitu cha kukemewa na nilazima watu walikemee mapema kabla mambo hayajawa makubwa we kwa akili za kawaida unadhani uchaguzi ukifika itakuwaje chama kimoja kitawezaje kuwa na wagombea wawili katika sehem moja. Acha cdm waingilie ili mambo yaishe na cyo cdm peke yake bali nivyama vyote vinavyo unda ukawa.

Sent from my K-KOOL using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom