Tunavuna aibu – Wapinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunavuna aibu – Wapinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 1, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,737
  Trophy Points: 280
  Tunavuna aibu – Wapinzani
  Stella Nyemenohi
  Daily News; Thursday,January 01, 2009 @20:00

  BAADHI ya vyama vya upinzani vimeshutumu majibizano baina ya Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuielezea hali hiyo kuwa ni fedheha kwa upinzani. Wakati chama cha Democratic (DP) kimesema ugomvi huo hauna maslahi yoyote kwa wananchi, kwa upande wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), kimesema hiyo ni aibu ambayo upinzani unaivuna.

  Ingawa Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema alisema anaamini kuwa hali hiyo ya mikwaruzano ni ya mpito, lakini alisema kitendo cha vyama vya upinzani kutofautiana kunadhihirisha kuwa dhamana waliyopewa hawajaitambua.

  Mrema ambaye alisisitiza kuwa vyama vya upinzani vinakwenda pabaya, alisema ipo haja ya kurudi katika meza ya mazungumzo hususani baada ya uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini kumalizika.


  “Ni kweli tunavuna aibu. Fedheha tunapata, lakini najua tutafika mahala tutajitambua,” alisema Mrema na kusisitiza kuwa shetani aliyejiingiza kati ya CUF na Chadema, anaathiri vyama vyote vya upinzani.

  Hata hivyo, Mrema alisema pamoja na mikwaruzano hiyo kuwa ya muda hususan kutokana na Uchaguzi huo Mdogo wa Mbeya Vijijini, lakini alilaumu hatua ya vyama kutokufikia Mwafaka wa kusimamisha mgombea mmoja.

  Alisema kama vyama vya upinzani vingeungana, ingelikuwa rahisi kuokoa mamilioni ya shilingi yanayotarajiwa kutumika katika kampeni. Alitoa mfano wa Chadema na kusema Sh milioni 120 ambazo chama hicho kilisema kitatumia, zingeunganishwa na zile za CUF, zingewezesha kukitikisa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo.

  Naye Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila alishutumu ugomvi baina ya CUF na Chadema kwa kusema hauna uhusiano wowote na maendeleo ya wananchi wa Mbeya Vijijini. Mtikila alisema, “wanapogombana hawa wanajimaliza wenyewe”. Alishauri ushindani wa vyama usiwe wa kukwaruzana bali uwe wa kutangaza sera zitakazowavuta wananchi.

  Tangu mchakato wa uchaguzi Mbeya Vijijini uanze, kumekuwapo na majibizano baina ya CUF na Chadema. Juzi, CUF ilikaririwa katika taarifa yake ikiishutumu Chadema kuwa haiheshimu makubaliano ya kuanzishwa kwa umoja wa upinzani.
   
 2. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini chadema na wenyewe safari hii wasiwaunge mkono wenzao wa cuf?
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mtarajiwa unasema safari hii je ujuavyo wewe mara ya mwisho ni lini na Chama kipi kiliwaunga mkono Chadema ? Hebu sema tuanzie hapo tafadhali .
   
 4. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Lunyungu sina uhakika sana mkuu.Lakini nilisikia kwenye uchaguzi wa tarime CUF hawakusimamisha mgombea na badala yake waliwaunga mkono CHADEMA ndiyo mana nikajiuliza kwanini nao chadema sasa wasiwasapoti cuf huko mbeya vijijini?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,737
  Trophy Points: 280
  Date::12/31/2008
  Maslahi binafsi kikwazo cha ushirikiano wa vyama vya upinzani
  Claud Mshana
  Mwananchi

  UMOJA ni nguvu na utengano daima ni udhaifu, msemo huo wa wahenga umekuwa ndio chachu ya kila mtu ama taasisi inayotaka kuona mambo yanaenda mbele kwa kushirikiana pamoja pale inapotakiwa kufanya hivyo.

  Msemo huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo ya watu mbalimbali hasa pale kunapoonekana kuna vikwazo ambavyo vinakatisha tamaa, na hivyo kufanya baadhi ya watu au kikundi cha watu kuanza kujitenga kwa ama kukatishwa tamaa, ama kuona mambo hayatakuwa kama wanavyofikiria.

  Suala la kufanya kazi kwa ushirikiano ndiyo siri pekee kwa wale wote wanaopenda kuona wanaendelea mbele licha ya kuwa na vikwazo vya aina mbalimbali vinavyokatisha tamaa.

  Hakuna taasisi iliyoonesha ushirikiano katika mambo yake ikashindwa kufikia lengo lake, liwe la kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kadhalika.

  Hapa nchini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kumekuwa na ushindani dhaifu dhidi ya chama tawala CCM katika chaguzi zote zilizofanyika tangu mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu chini ya mfumo wa vyama vingi.

  Udhaifu huo si kwamba unasababishwa na ubovu wa sera za vyama vya upinzani, la hasha bali ni ugumu wa kukiangusha chama tawala kilichoshika hatamu za uongozi wa nchi hii tangu kupatikana kwa uhuru miaka 47 iliyopita.

  Na hapa ndipo kunapokuja umuhimu wa kuwa na ushirikiano katika taasisi za siasa, hasa vyama vya upinzani kama kweli vinania ya dhati ya kukiondoa CCM madarakani.

  Mwaka 2007, viongozi wa vyama vinne vya upinzani vya NCCR Mageuzi, TLP, CUF na Chadema waliona umuhimu wa kuungana na kuwa na nguvu ya pamoja na hivyo kuweza kuleta ushindani dhidi ya CCM katika chaguzi mbalimbali na kuwa na msimamo wa pamoja katika maswala mbalimbali ya kitaifa.

  Hakuna mpenda mageuzi ambaye hakufurahia uamuzi huo wabusara uliooneshwa na upinzani, na hali ya matumaini kuwa huenda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 utakuwa na mabadiliko makubwa katika medani ya siasa hapa nchini kwa upinzani kushika hatamu za uongozi wa nchi hii.


  Matumani hayo kwa kiasi kikubwa yalichochewa na mafanikio ya kuwa na nguvu ya pamoja iliyochangia kukiondoa madarakani chama cha KANU nchini Kenya na kukiingiza chama kilichokuwa na muunganiko wa vyama mbalimbali vya upinzani nchini humo cha NARC Kenya.

  Matumaini ya ushirikiano huo yalikuwa kwa kasi na kujenga imani kubwa kuwa yataleta mabadiliko makubwa katika medani ya siasa, kwani siku chache tu baadae nguvu ya ushirikiano huo ilianza kuonekana katika chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo ya Kiteto na Tunduru ambapo moja ya makubaliano ya vyama hivyo kuachiana nafasi yalitekelezwa.

  Haikuishia hapo tu kila jambo lililokuwa na maslahi kwa taifa lilitolewa tamko la pamoja, na kuwa na msimamo wa pamoja jambo ambalo lilizidi kuongeza imani ya ushirikiano huo na kuongeza matumani kwa wananchi wapenda mageuzi.

  Kilichofatia baada ya hapo ndio kinachotia hofu kuwa kama kweli vyama vya upinzani vilikuwa na nia ya dhati ya kuungana na kuwa na nguvu ya pamoja dhidi ya chama tawala, kwani mambo yalianza kwenda mrama wakati wa hekaheka za uchaguzi mdogo katika jimbo la Tarime kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Chacha Wangwe.

  Yale makubaliano yaliyofikiwa ya vyama vya siasa vitakuwa vikiunga mkono chama chenye nguvu katika jimbo husika yakaanza kukiukwa na kila chama kikaanza harakati za kusimamisha wagombea wake.

  Yaliyojiri katika hekaheka hizo za uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime hakuna haja ya kuyarudia, vurugu maneno ya lawama kati ya viongozi wa upinzani walioamua kushirikiana ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kuhakikisha wanaleta maendelo yakawa chachu ya mgawanyiko kati yao.

  Kinachooneka hapa ni kutoaminiana baina ya vyama hivyo na hofu ya kupoteza ushawishi wa kisiasa ndio maana kila kukicha tunaona jinsi gani safari yao ya kuingia ikulu mwaka 2010 ikizidi kuwa ngumu kwa kukutana na vigingi vya kila aina.


  Niliwahi kuzungumza na mwananzuoni Profesa Mwisega Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliniambia kuwa tatizo linalowakabili viongozi wa vyama vya upinzani ni hofu ya kupoteza nguvu ya kisiasa.

  Alifafanua kuwa endapo watakuwa wakisaidiana katika maeneo ambayo chama Fulani kinaonekana kuwa na nguvu na chama hicho kikashinda, idadi ya vitu bungeni itahesabiwa kwa chama kimoja kilichoshinda kiti hicho hata kama nyuma yake kulikuwa na mchango mkubwa wa vyama vingine.

  Na hilo ndilo linaloonekana hivi sasa, kwani tangu uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime upite kumekuwa na kauli za kujichanganya za viongozi wa vyama vya upinzani, leo huyo kasema hivi, kesho mwingine kakanusha na kadhalika.

  Na sasa mzimu huo umehamia katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Januari mwakani kufatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Richard Nyaulawa kufariki dunia.

  Ubinafsi ndio naoweza kusema umejaa katika vyama vyetu vya upinzani, kama kweli walikubaliana kusaidiana pale chama kimoja kinapokuwa na nguvu mahali fulani iweje leo kila chama kusimamisha mgombea wake?

  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiongea na waandishi hivi karibuni alikaririwa akisema wameiomba Chadema kuwaunga mkono katika uchaguzi huo lakini kilichoshuhudiwa ni Chadema kusimamisha mgombea wao.

  Ukichukilia mfano wa kilichotokea nchi jirani ya Kenya ambapo muungano wa NARC Kenya ulikiangusha chama kilichotawala kwa muda mrefu tangu uhuru wa nchi hiyo cha KANU, maslahi binafsi yalikuja kuvunja muungano huo na matokeo yake kila kukicha makundi mapya yanaanzishwa.

  Suala la kila chama kutaka nyazifa kubwa na muhimu kama ilivyotokea kwa NARC Kenya ndio kinachoweza kutokea hata hapa nchini kwa vyama vyetu kama swala la kila chama kutanguliza maslahi binafsi litaendelea kuwa ndio msingi wa kufikia makubaliano ya pamoja.
   
 6. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anha sasa naelewa.Kumbe makubaliano ni kukiachia chama chenye nguvu katika jimbo husika kisimamishe mgombea na wengine waunge mkono.
  Tarime tunajua chadema kina nguvu na kilikuwa kinatetea jimbo lake.Je huko mbeya vijijini ni nani wenye nguvu kati ya chadema na cuf?Tukijua hapo basi hao ndiyo wanapaswa kusimamisha mgombea kulingana na yale makubaliano yao.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Jan 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Dr. Slaa, Zitto au J.J Mnyika wakuu naomba maelezo kuhusiana na swala hili..naona Utata uliposimama!..
  Chadema nadhani hawakusimamisha mgombea Mbeya vijijini mwaka 2005, sasa ni kitu gani hasa kilichowashinda kuwaunga mkono CUF kama walivyoungwa mkono na CUF huko Tarime badala yake Chadema anao wamemsimamisha mgombea...What's going On!

  Ushindi wa Tarime ulikuwa ushindi mkubwa kwa both Upinzani na funzo kubwa kwa waasi..kwani mshikamano kati ya Chadema na CUF ndio kitu kilichoonekana kwa wananchi wengi..
  Ushindi wa Tarime utumike kama mwanga kuwa umoja unaweza kuwa na nguvu gani.. sio swala la Chadema kujivunia dhidi ya Wapinzani bali ni moja ya kielelezo kwamba inawezekana kabisa kumwondoa CCM madarakani..

  Nimewahi kutoa Ushauri kwamba kila jimbo ambalo mgombea wa chama fulani ndiye alikuwa mshindi wa Pili chini ya CCM ndiye apendekezwe kugombea Ubunge au kuwepo na uchaguzi wa ndani kati ya wagombea wawili wenye nafasi sawa ya kushinda..
  Hizi habari za kushinda wapizani kulipizana kisasi ni akili finyu sana ikiwa kweli ndio sababu ya kufanya yaliyofanyika!
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Mkandara nadhani nawe unakosea.CUF hawako Tarime na hata bila ta Chadema CUF wasingaliweza kusimamisha mtu maana hawana Chama Tarime .CUF na TLP na NCCR walitoa matamko wote kuhusiana na kifo cha Marehemu Wangwe na madai mazito sana .Sasa usichanganye habari hapa .Omba maelezo tu lakini ukweli ni kwamba CUF Mbeya hawako na ni weak mno .Kama huamini ngojea uone kitakacho tokea .
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,737
  Trophy Points: 280
  Mimi kwa maoni yangu hili la kusimamisha mgombea kwa kuangalia chama kipi kina nguvu katika jimbo hilo si ushirikiano ulio madhubuti. Ili kuleta ushirikiano wa kweli vyama hivi vinabidi viungane na vifanye hivyo kabla ya uchaguzi wa 2010.

  Tatizo lililopo ni kwamba vingunge wote ndani ya vyama hivi wana wasi wasi kwamba pindi wakiungana basi watapoteza nafasi za juu walizokuwa nazo ndani ya vyama vyao. Lakini wanasahau kwamba Tanzania ni nchi kubwa pindi chama chao kipya kitapoingia madarakani kuna nafasi nyingi za juu ambazo kutokana na elimu na uzoefu wao waliokuwa nao wanaweza kupata nafasi hizo.

  Bado vyama vya upinzani vina safari ndefu katika nia yao ya kuing'oa CCM madarakani.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Jan 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu,
  Mkuu unazungumzia two wrong making A right!..swala hapa ni Mbeya sio Tarime..Haiwezi kuwa hivyo hata kidogo kama Chadema wanayafanya haya kama kulipa kisasi..
  CUF kusimamisha mgombea Tarime sio swala la kushinda, hawana mgombea kama Chadema wasivyokuwa na mgombea Mbeya vijijini..Umoja wa vyama sio swala la ushindi tu ama kuharibu kura bali ni ushirikiano wa mambo mengi mazito kuliko uchaguzi mmoja. Na ndio sababu sisi wananchi tuliwalaumu CUF, TLP, NCCR -Mageuzi na vyama vinginevyo kwa njama za baadhi viongozi kutaka kukomeshana..
  Swala la Marehemu Wangwe na tuhuma zilizokuwepo lipo nje ya hoja ya ngu. Hata ndani ya Chadema kuna watu walikuwa na hisia na mtazamo tofauti, hivyo huwezi kuwahukumu kwa sababu tu waliondoa trust kwa baadhi ya watu. Chama sio Mbowe wala Mtikila chama ni zaidi ya watu hao. na hakuna sehemu hata moja iliyosema Chadema wamehusika na kifo cha Wangwe..
  Leo hii kuna watu ndani ya CCM wanapiga vita Ufisadi haina maana wanakisaliti chama..Na mkuu wangu hata siku moja usifikirie kwamba Chadema inaweza kuchukua nchi kwa nguvu zake pekee.. tunakufa kabla hali hiyo haijatokea.. Na kulaumu na kunyoosheana vidole haiwezi kutusaidia sote ikiwa mnataka maswala lkama haya yazungumzwe chumbani..No Open kama hpa ndipo watu tunawaelewa vizuri msimamo wenu kama chama..hakuna mtu aliyesema CUF wangeweza kushinda Tarime.. wala sidhani kama Chadema inawaunga mkono CUF Zanzibar huwa kuna uwezekano Chadema kushinda!..
  What's Up!..
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkandara,

  Tatizo ni maslahi binafsi, waungane halafu wagawane vyeo? CHADEMA wanarudia makosa ya NCCR mwaka 1995.

  Ni kama ilivyo CCM kwenye suala la katiba, wanajua ukweli kwamba katiba huru ina faida kwa nchi lakini unyang'au wao na ubinafsi una nguvu kuliko maslahi ya nchi. Kaunda kule Zambia aliwahi kukataa katiba huru, baadaye ikaja kumdhuru kweli kweli.

  Hapa ni sawa na kuampigia mbuzi gitaa, CHADEMA walikuwa wanataka kuungana 1995 wakati hawakuwa na nguvu lakini sio 2009 wakati wana nguvu. Aliyesema wakati wa kununua insurance ni wakati huihitaji hakukosea. Kwasababu sasa CHADEMA wana nguvu, muungano wowote ungewafaa zaidi wao kwa siku za mbeleni.
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kwani mnauhakika vyama vya upinzani vinapigania haki ya mnyonge ama vinapigania maslahi? tuendeleni kuzidaganya nafsi zetu kuwa chama kile kina maslahi kwa taifaa tutaimba weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee siku kuja kugunduwa jua nalo lileeeeeeeeeeeeeeeeeeeee linazama.

  Ila mimi nafikiri hawakumtendea haki huyo mgombea wa chadema kumwondowa.LAkini kuhusu et wanapigania haki ya mnyonge THUBUTUUUUUUUUUU
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mtanzania,
  Unajua mkuu tatizo la Tanzania sio vyama hata kidogo isipokuwa ni majungu majungu yanayopikwa na baadhi ya watu kwa sababu ambazo naweza kusema ni Ubinafsi. Mimi siwezi kabisa kusema Chadema wana nguvu sawa na NCCR mwaka 1995, na itakuwa kazi sana kufikia kiwango hicho kwa sababu nikangalia matokeo ya mwaka 2005 inaonyesha wazi kwamba bado kabisa safari ni ndefu..
  Uchaguzi ule ulitakiwa uwe somo kwa vyama vya upinzani na matukio ya hizi chaguzi ndogo pia ni somo jingine kuonyesha ni kiwango gani cha ushirikiano kinahitajika..
  Sasa ikiwa ktk Uchaguzi mdogo tu tunaanza kuvumishana magongo, vipi uchaguzi mkuu ambako CCM huweka nguvu zote..
  Swala la mgombea wa Chadema Mbeya vijijini ni somo jingine jipya hasa nilipokuja gundua kwamba CUF walitegemea Chadema kuwaunga mkono na sidhani kama Lipumba amekurupuka toka huko aliko kuweka madai kama haya inanikumbusha Tarime..Chadema walisemna haya haya kuhusiana na vyama vinginevyo lakini sioni sababu ya kuingiza chuki baina ya vyama hivi hasa Chadema na CUF.
  Sasa ile bahati kubwa ya ushindi Tarime haiwezi kuwepo mikoa yote na hasa mkoa mgumu kama wa Mbeya ambako wabunge wa CCM walishinda kwa kimbunga nadhani kuliko mikoa yote ukipima asilimia za washindi..
  Hivyo maneno yako kweli kabisa kwamba ikiwa mtu hutazami maslahi ya Taifa ni vigumu sana kuona mbele..Kwa hali kama hii ya ugonvi baina ya Upinzani inawazidishia nguvu CCM.
  Watu kama Mrema na Mtikila mimi siku zote huwaona kama wale wanaotafuta Umaarufu lakini kama kweli kuna ukweli ktk madai haya nadhani Chadema wamecheza rafu... na pengine ktk kufanya hivyo CUF wamerusha kitambaa chekundu uwanjani kuomba replay ambayo imechukua nafasi ya kutengua maamuzi ya awali..Na Chadema hawataishia hapo kitendo cha CUF kitanukuliwa kwa mengine mengi yanayofuata..
  Vita kama hii haitakwisha na nina hakika itaendelea hadi uchaguzi wa 2010 na kama vyama hivi havitaweza kufikia maafikiano ya kati...Then CCM ataibuka mshindi tena vibaya sana..
   
 14. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Kinachotuponza kwenye Taifa hili ni umimi sana na Chadema kwa sasa upo kwani wamelionyesha hili wazi ,kwani walipoombwa na CUF hata kama walikuwa hawataki si wangejibu hiyo barua kuliko kukaa kimya kwanza ni Dharau walionyesha lazima tufike mahali watanzania wakubaliane kutokubaliana kwa nidhamu bila chuki nafikiri hii ndiyo sababu kuu CUF kuamua kuweka pingamizi,sasa nimeelimika kwenye hili.
   
 15. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2009
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Wacha tu wavimbe kichwa CMM knows how to play with Wananchi ngoja Uchaguzi ufike utaona hiyo Obamanize inavyowasambaratisha wapinzani na si ajabu hao chadema wasishike hata hiyo nafasi ya pili.
   
 16. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unapoanzisha chama lazima kunakuwa kuna ITIKADI iliyo kusukuma kuanzisha hicho chama, na kama kuna chama ambacho mnafanana fanana kiiitikadi basi mnaungana nacho kuongeza nguvu ili chama chenu kiwe na nguvu. Sidhani kama kinachotakiwa ni kuungana tu ili mradi ( mfano mzuri anaujua Al Gore njisi Nader alivyompokonya uraisi, na hiyo ndiyo demokrasi)

  Kama Chadema na CUF vinafanana itikadi basi vinatakiwa viungane ili kiwe chama kimoja au kama itikadi yao kubwa ni kuitoa CCM madarakani tu basi pia waungane! Lakini kama itikadi zao ni tofauti hakuna haja ya kuungana hata kidogo (pro life na pro choice hawawezi kuungana hata siku moja) Tuache kulazimisha mambo kwa presha za mafisadi ambao sisi wenyewe tumewalea.

  ushauri wangu kwa vyama vya upinzani ni kuwa vinaweza kushirikia na vyama vingine katika kuhakikisha kuwa haki zinatendeka na sheria zinafuatwa ila siyo kuungana (kama itikadi zao ni tofauti) wala kuachiana majimbo. Utamwachiaje jimbo mtu aliye na itikadi tofauti na yako? ili iweje? tuache kutaka kuharibu mfumo kwa lengo moja tu bali tujenge mfumo utakao tusaidia baadaye.

  CUF kuweka pingamizi ni sawa kabisa kwa sababu kwa CUF chadema na CCM vyote ni vyama pinzani tu vyenye itikadi tofauti na yao na kwamba CUF inaona kwamba hiyo itikadi haifai ndiyo maana wakaanzisha chama kuipinga (kuzipinga). Chuki zetu kwa mafisadi zisifanye tuanze kubadilisha mfumo kwani tutapata tabu sana pale lengo linalotusukuma kufanya hivyo litaapo timia litakapotimia lisilikuwa na mfumo sahihi (mfano Kenya). Mfano Cuf na Chadema wamechukua nchi navyoni vyama viwili tofauti vyenye itikadi mbili tofauti vitatawalaje? na vitafuata itikadi ya chama kipi? lazima tuwe makini.

  Kituko kikali kuliko vyote ni pale chama ambacho kwenye kinyanganyiro cha takribani viti 200 lilpata zero leo kiachiwe na chama kilichopata viti 10 Du! kisa eti mngombea wake alikuwa wapili.

  Chadema msikubali ujinga huu kabisa nyie ni chama na mnaitikadi zenu mnzozipigania hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha kuwa mnapata wawakilishi wengi tu bungeni ili mnapiotoa hoja zenu za ufisadi mnakuwa na watu wa kuwaunga mkono. Achaneni na donto za kuungana wakati hata mfumo wetu hauruhusu jengeni chama chenu kiwe strong na atakaye kipenda atajiunga mwenyewe!
   
 17. E

  Eric Ongara Verified User

  #17
  Jan 2, 2009
  Joined: Sep 19, 2006
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Shalom, siku zote huu umekuwa mtazamo wangu, nauunga mkono hoja yako. Muungano wa vyama si sulihisho, kila chama ni mshindani wa mwenzake, wanaweza kuwa na ushirikiano katika masuala ya kitaifa au ajenda za kustawisha demokrasia kama vile masuala ya kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi!

  CUF na CHADEMA ni vyama shindani, watanzania wenye muamko wa kisiasa bado ni wachache kwa hiyo hivi vyama pamoja na CCM zinashindania watu hawa hawa, ndio nashangaa Duni analalamika kuwa opereshen Sangara inaua CUF kwa kuwa CHADEMA inavuna wanachama wa CUF katika maeneo wanaopita! Wao mwaka mzima wanajadili muafaka wanategemea nini?

  Suala la kusimamisha mgombea mwaka 2005 halina mshiko, CUF wamejiimirsha kwa kiasi gani huko mbeya vijijini tangu 2005? wao wamewekeza Zanzibar tu leo wanalalamika waachiwe? Na si kweli kuwa CUF waliiachia CHADEMA tarime! CUF walisimamisha mgombea katika ngazi ya udiwani, na Tarime NCCR pia waligombea mbao pia wana ushirikiano nao, ni kwa vipi wanasema waliiunga mkono CHADEMA? si wanaweza sema hivyo pia kwa NCCR mageuzi? au wanataka kusema waliunga mkono vyama vyote viwili?

  Kuendelea kuviangalia vyama kama kapu moja la vyama vya upinzani badala kuimarisha taasisi moja moja zenye muelekeo ni kuchelewesha mabadiliko.CHADEMA songeni mbele, wanaanchi wataonganisha vyama katika sanduku la kura kwa kumpa kura nyingi mgombea alie bora.
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  CHADEMA
  kina sera za BUSH wao lazima uwaunge mkono ,ukitofautiana nao basi wewe ni mamluki na hukitakii mema chama chenye maslahi kwa taifa na umetumwa na mafisadi ,teh teh teh teh teh teh teh teh.
  Hapo utakuja kusikia Lipumba amepewa mshiko na RA.kwi kwi kwi kwi kwi kazi kweli kweli.

  mbona chadema akina NCCR na DP waliposimamisha mgombea walionekana kama wametumwa na ccm je? leo chadema hawajatumwa na ccm kuvuruga CUF ama ni CUF ndiyo imetumwa??
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  EO,

  Nimeipenda hiyo! hatuwezi kuviangalia vyama vya upinzani kama kapu moja hivi ni vitu tofauti kabisa kufanya hivyo kunaweza kuwa na mafanikio kwa mda mfupi nakwa muda mrefu ni hatari kwa nchi kwani moja ya matunda ya vyama vingi ni kuwa na agenda mbadala za kiushindani zinazoendeleza nchi. Sasa utaona kuna vyama hapa bongo kazi yao ni kudandia tu au kukaa kimya kusubiri kuachiwa majimbo nonsense kabisa hiyo (Hongera chadema kwa hoja za ufisadi).

  Tunapenda kuona kuwa kama chadema walivyokuja na hoja ya ufisadi basi NCCR nao waje na hoja yao yenye uzito kama huo, CUF nayo ije na hoja yake ukizichanganya zote hizo utaona kuwa nchi inaendelea. Sasa wao wamefanya nini? wengine wamekaa kimya wengine wivu wengine mamluki halafu ukifika uchaguzi utaona jamaa wanaanza tuachie na sisi tugombee

  CUF fanyeni kazi yenu ya siasa kwa nguvu nanyi mtakubarika msitegemee kuachiwa ni aibu kubwa kwa chama cha siasa kutaka kuachiwa jimb0 ili ishindane na chama kimoja tu bila ushindani ni aibu kubwa sana. Ushindi mzuri sana ni ule ambao kutakuwa na wagombea wote 13 wa vyama vya siasa na mkishinda mnajua kweli sera zenu na strategy zinakubarika

  Chadema achaneni na huu utani wa kuungana bila na watu msiokuwa na malengo mamoja acha! kabisa kwangu ni kheri msipate nafasi ya kuongoza nchi ( kuna vyama vingi tu duniani ambavyo havijawahi kuunda serikali lakini vina mchango mkubwa sana kwa nchi yao) kuliko kujiingiza kwenye aina hii ya siasa mufilisi za kuuza itikadi yako kwa ajiri tu yakutaka kupata ushindi zidi ya mtu fulani
   
 20. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mbona unawaita viongozi wa chama kimoja tu ndio waje kujibu hapa? Mbona huwaiti viongozi wa CUF nao waje hapa kujibu tuhuma zao? (au hawana muda wa kufuatwilia mambo ya mtandao kama viongozi wa CCM). Usiwaonee viongozi wa chadema kwa sababu tu wameamua kujitolea kuja humu kushirikiana na sisi unapotoa matamko yawalenge wote hata hao ndugu zako

  Hoja yako ya kila mngombea aliyekuwa wa pili basi aachiwe kungombea jimbo basi kule Karatu mtamwachia CCM angombee na chadema 2010 au siyo maana CCM alikuwa wa pili na nyie mkafuata watatu( I see true colour shining through)
   
Loading...