SoC04 Tunatamani Uchaguzi Mkuu na Serikali za Mitaa kufanyika kwa njia ya mtanado (Smart Vote Card)

Tanzania Tuitakayo competition threads

Festus K Fau60

New Member
May 23, 2024
1
0
Tanzania Tuitakayo-Dira: Tunatamani uchaguzi mkuu na serikali za mitaa kufanyika kwa njia mtandao (smart votecard)

Nini kifanyike kufikia njia ya usajili wa wapiga kura kwa njia ya mtandao, nirahisi sana

Kanuni za uchaguzi chini ya tume ya taifa ya uchaguzi tanzania zinamtaka mwananchi/mpiga kura mwenye sifa za kupiga kura mojawapo ya sifa ni kuwa na umri usiopungua miaka kumi na minane (18), vivyo hivyo hata mamlaka ya vitambulisho vya taifa ili wamsajili raia wa nchi hii mojawapo wa sifa lazima awe ametimiza umri wa miaka 18, hata mamlaka ya mawasiliano tanzania na makapuni ya simu pia bila kusahau wataalamu toka wizara ya habari mawasiliano na tekenolojia.

Kwaiyo kupitia mamalaka hizi na wadau watoa huduma tayari tunaweza kufanya muunganiko wa taarifa na kuweza kuwafikia wapiga kura kwa muda mchache na kuwapa elimu kwa njia rahisi sana ya tekenolojia na kuwafikia watu wengi zaidi, pia kuwa na kituo kimoja cha kupokelea matokeo kwa njia ya mtandao na kuonesha mwenendo wa kura unavyoenenda kwa kila mgombea kupitia simu yake mwisho wa siku inabaki tume kuthibitisha/kutangaza mshindi na kumkabithi hati yake ushindi, kwakufanya hivyo hizi hapa chini ni baadhi ya faida tunazoweza kuzipata kupitia mtandao kuweza kuwapata viongozi wetu tunaowapigia kura:

Kufanyika uchaguzi kwa njia ya mtandao kuna faida kubwa sana kwa taifa letu.

1. Kupunguza muda mwingi kusimama kwenye vituo vya wapiga kura

2. Kupunguza gharama za kusafirisha vifaa, waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje, gharama za uchapishaji karatasi za wapiga kura, gharama za vyombo vya usafiri/usafirishaji.

3. Jeshi la Polisi kupunguziwa majukumu ya kulinda kura kila kituo na badala yake kufanya majukumu mengine ya uzalishaji kwa manufaa zaidi ya taifa.

4. Wananchi/wapiga kura kupunguziwa muda wa kukaa kituoni muda mrefu wakati mwingine kutumia siku nzima na kusuimamisha uzalishaji kwa taifa.

5. Kuongeza imani kwa wapiga kura kwa kuamini kuwa kiongozi aliyechaguliwa ni halali na nichaguo lao.

6. Kupunguza rushwa na fujo wakati wa upigaji kura kwa maana mpiga kula huweza kupiga akiwa popote ilimradi awe amesajilwa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa(nida) kwa kushilikiana na tume yataifa ya uchaguzi tanzania.

7. Kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wanaochaguliwa na wananchi/wapiga kura.

8. Kupunguza upotevu wa masanduku ya kura ambayo tayari wananchi/wapiga kura walishamchagua kiongozi wao ghafla utasikia sanduku la kura limepotea.

9. Kupunguza muda wa uhesabuji wa kura maana baada ya zoezi la upigaji kura kuisha kura ukusanywa toka vituo mbalimbali na kupelekwa sehemu maalumu kwa ajili ya majumuisho ambayo kwa amaeneo ambayo hayafikiki kirahisi inakuwa changamoto sana ambayo uongeza wasiwasi kwa wapiga kura.

10. Kuhamasisha watu wengi kupiga kura kuliko sasa, wengi hukata tamaa kwa kuogopa msumruru mkubwa wa wapiga kura

11. Itaongeza amani utulivu na mshikamano kwa taifa na kupunguza malalamiko ya kila wakati baada uchaguzi kuwa kura zinaibiwa maana kila anayeshindwa mara nyingi tumekuwa tukisikia kuwa ameibiwa kura na wakati mwingine kupelekea kuaminishwa wapiga kura kuwa kuna vitendo vya kiulaghai vimetendeka na kumbe wakati mwingine sikweli.

12. Kupunguza uhuru wa mtu kutokupiga kura kwa sababu tu kituo alichojiandikishia lazima apigie kura hapohapo alipojiandikishia, pia uhakiki wa daftari la wapiga kura kila baada ya miaka mitano hii nayo uongeza bajeti isiyo na ulazima maana kama mpiga kura ameshasajiliwa kwa njia ya kitambulisho cha taifa taarifa zake ni rahisi kuzipata kulikoni sasa tunavyoendesha daftari la wapiga kura

13. Kupunguza kesi za ukataji rufaa mahakani mara baada ya uchaguzi, wakati mwingine eneo /jimbo humkosa mwakilishi kwa muda kwa sababbu tu mmoja wa wagombea anamashaka na uhesabuji wa kura.

14. Kupunguza huaribikaji wa kura wakati mwingine mpiga kura anaweza kuweka vema na mkato hii hupelekea kura kuhesabika kama imeharikbika lakini kwa njia ya mtandao atakuwa na namna moja tu mfumo utamuongoza.

Imeandaliwa na

MSWETA,Faustine 0658699867 mswetaf@gmail.com
 
3. Jeshi la Polisi kupunguziwa majukumu ya kulinda kura kila kituo na badala yake kufanya majukumu mengine ya uzalishaji kwa manufaa zaidi ya taifa
Na bora.

. Itaongeza amani utulivu na mshikamano kwa taifa na kupunguza malalamiko ya kila wakati baada uchaguzi kuwa kura zinaibiwa maana kila anayeshindwa mara nyingi tumekuwa tukisikia kuwa ameibiwa kura na wakati mwingine kupelekea kuaminishwa wapiga kura kuwa kuna vitendo vya kiulaghai vimetendeka na kumbe wakati mwingine sikweli.
Kweli mwanangu aaah, mfumo uwe wa kuaminika na wote mshindi na mshindwa
 
Back
Top Bottom