Tunataka kuuana kwa ajili ya kitovu cha mtoto

Jamani l am not a witchman, I am only protecting my kid, dhidi ya wanaotaka niwape kitovu
Wape tu mkuu. Unaogopa nini? Unadhani/unaamini watakifanyia nini? To me, hicho kitovu kikishatoka kwa mtoto hakina tofauti na uchafu mwingine. Ukianza kuamini kuwa ati wanaweza kumdhuru mtoto kama watachukua huo uchafu basi na wewe unaanza kuwa mshirikina. Labda kama unaniambia unahisi hao ndugu wana mpango wa 'kumlisha' huyo mtoto hicho kitovu!
 
seriously,haya ni mageni kwangu kuhusu kitovu.sikujua kama mtu anaweza kufanyia ushirikina kuhusu kitovu
Labda tu hawa wanaoshabikia vitovu wangetupa Elimu kwamba je ni kweli mtoto wa kiume akiangukiwa na kitovu anakuwa si riziki, yaani Dushelele linakuwa mlenda? mwenye uelewa juu ya tetesi hizi naomba anijuze sina sababu ya kuanzisha thread nyingine, naomba lift hapa hapa.
 
Pole sana.......hebu gfsonwin, Mtambuzi, HorsePower na nyumbakubwa mje hapa kidogo

Thanks kwa mwaliko.
Kwa mtazamo wangu, kitovu kama kitovu hakina kazi yeyote kwangu kama mzazi, ila kwa sababu za imani za kishirikina na pia kwa sababu ya hao ndugu waliojitokeza kugombea kitovu, NALAZIMIKA kuamini kuna mambo ambayo yanataka kufanyika dhidi ya mtoto hivyo basi kama baba MZAZI wa MTOTO, kitovu ni bora akae nacho mwenyewe na mwisho wa siku akakifukie sehemu ambayo mtu mwingine hawezi kujua.

Ni ngumu sana kuwaamini baadhi ya ndugu au marafiki ambao wanaonyesha wazi wazi kuwa bado wako kwenye hali ya imani za jadi au kishirikina maana wanaweza kukupandikia roho za ajabu kwa mtoto au pengine hata kumdhuru kabisa! Mara ngapi tunasikia watoto wamepotea kwenye mazingira ya kutatanisha? :sad:
 
Dsm dili nyingi sana, sikujua kuwa vitovu ni biashara nzuri, ndio maana hospitali ya Mwananyamala haiishi vituko
 
Dsm dili nyingi sana, sikujua kuwa vitovu ni biashara nzuri, ndio maana hospitali ya Mwananyamala haiishi vituko.......
 
Haya mambo huwa mnayakaribisha wenyewe kwenye familia zenu. Mimi nina shida kidogo linapokuja hili suala la kurundika ndugu nyumbani kwa sababu yeyote ile.

Hivi kujifungua ni ishu saaaana mpk mama mkwe wako, mama yako, bibi wa mkweo na ukoo mzima ujae nyumbani kwako? Mimi navyofahamu, siku za kwanza za maisha ya mtoto ni very delicate, sasa kuchukua wabibi kijijini kuwajaza nyumbani wengine wana magonjwa ya kuambukiza wengine wana harufu za ugoro n.k huko ni kumnyima mtoto haki ya kupata pumzi safi.

Kwa kifupi huo ndio mshahara wa maisha ya kiswahili. Sio mtoto kazaliwa tu hata mwezi hajatimiza basi kila mtu aje kumtia mikono yake, wengine wanga, wengine wana TB, ah jamani, badilikeni. Wafukuze wote bakia na mkeo

hapo kwenye red...hahaaahaaaaa dah umenifurahisha
 
na mwenyewe kesha ukiomba....

Solution hapo ndogo waite wote waambie huwapi kitovu cha mtoto.... Wewe ndo baba utakaa nacho......

Mwisho wa siku kitapotea tu.....

Sie wengine vitovu tuliambiwa tukavifukie tu.......

Hata hivyo kuwa makini vinatumika kwenye mambo ya nguvu za giza vilevile ndo maana nakwamnia usimpe hata mmoja kati yao..na vita vitakwaisha ukiwa firm.....

Halafu waafrica bwana badala ya kuhombea dhahabu tunagombea vitovu
Umeambiwa Tanzania nchi ya kwanza kwa ushirikina, sasa unashangaa nini? Mtoto wa kwanza mara nyingi husababisha ugomvi sana kwenye familia miongoni mwa ndugu
 
usikubali katu kutoa kitovu cha mwanao wewe ndo mzazi, hao waganga wa nini nyumbani ? mtoto analindwa na Mungu na malaika zake sio na nguvu za giza na waganga wa kienyeji, ogopa sana mana vitovu vinatumika katika nguvu za giza na kuharibu kila kitu juu ya huyo mtoto, waswahili wanasema ukitaka kumroga mtu sharti ujue kitovu chake kilipo...........pole ndugu.............
 
hizo imani niushirikiana achana kama kweli ni muumini mzuri basi sali sana acahana na kungombania kitovu
 
Mimi naona mleta mada hamumtendei haki. Ingekuwa wewe mama mkwe anakuomba kitovu cha mtoto...ungempa kwa kuwa wewe unamuamini Mungu?

Anakitaka cha nini????

Mimi namuamini Mungu lakini najua uchawi upo...hivyo nisinge mpa mtu kitovu cha mwanangu... simple. Akipata matatizio nianze tena kuhangaika kwa mapadre na wachungaji???

Wakristo walio safi na wakweli hata kukumbuka habari za kitovu hatukumbukagi,kama wewe ni mkristo jichunguze una matatizo ktk ukristo wako.
 
Pole Kiranja Mkuu, iyo kitu ipo sana hasa kwa wazazi wetu. Kwanza nakushauri mkabidhi mwanao kwa Mwenyezi Mungu tu, yeye amekupa mtoto na yeye ndiye atakayemlinda mwanao. Wewe kama baba wa mtoto una final say, sio mama yake wala mama mkwe! Waambie ukweli kuwa hutowapa hicho kitovu na kwamba hizo imani zao za kishirikina wewe huzitaki kwenye familia yako. Baada ya hapo kama walikuja kumuuguza mkeo wape nauli warudi kijijini kuangalia nyumba zao na mashamba mana shughuli imekwisha, period!!

Toka lini mama akawa hana final say juu ya mtoto wake? mengine yote sema ila usimpotoshe mwenzio kwenye hili la mwenye final say kwa mtoto.
 
nani kati ya mama yako, mama mkwe na bibi alokwambia kwamba utarogwa?

Na alijuaje kama utarogwa kama na yeye si mrogaji?

Siku nyingine wakikwambia utarogwa waambie heri urogwe wewe kuliko kumroga mwanao.....

Anyway mpaka leo hawajaondoka tu? Waambie muda wao umeexpire ubakie na familia yako kukwepa kero

nimeambiwa nitarogwa kama nitaendelea kung'ang'ania kitovu cha mwanangu
 
Labda tu hawa wanaoshabikia vitovu wangetupa Elimu kwamba je ni kweli mtoto wa kiume akiangukiwa na kitovu anakuwa si riziki, yaani Dushelele linakuwa mlenda? mwenye uelewa juu ya tetesi hizi naomba anijuze sina sababu ya kuanzisha thread nyingine, naomba lift hapa hapa.

kuna sredi fulani niliwahi kuisoma kama sijakosea ni jf doctor,inshort hakuna uhusiano wa kitaalumu wa hilo ulilouliza apo juu,wanasema zamani watu walikua wanaambiwa hivyo ili wawe makini na kitovu cha mtoto kwasababu kupitia kitovu,mtoto anaweza kupata magonjwa mbali mbali kwa haraka.kwa kifupi mkuu hayo ndio niliyachota ktk hiyo sredi.
 
mbona picha ndo linaanza hapo. na kama ni mvulana na hujamtahiri then subiri wakati wa kumtahiri waanze kukililia hiko kipande kitakacho baki....................
 
Back
Top Bottom