Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.
Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.
Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.