Tunataka akina Dr Slaa wengi bungeni!!

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,380
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,380 280

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa​

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa, amesema kuna haja kwa Rais Jakaya Kikwete, kuwaomba radhi Watanzania, kufutia kitendo cha serikali yake, kushindwa kutimiza ahadi ya kuibua ajira 1,000,000, kama alivyokuwa ameahidi katika kampeni zake za mwaka 2005...

http://www.globalpublisherstz.com/habari_mbalimbali/
 
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
31
Points
135
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 31 135
Sawa, ajira zinakuwapo lakini wapambe wake wanazinywa kwa kuwapa ndugu zao. Mpaka waishe hao ndio walala hoi wataziona. Tena ukionyesha harufu ya upinzani ndio ufe kwanza ndipo upate, maana kwa Tanzania ya leo mpinzani ni kama shetani na CCM ni mungu (sio Mungu)

Leka
 
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
3,874
Likes
314
Points
180
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
3,874 314 180

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa​

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa, amesema kuna haja kwa Rais Jakaya Kikwete, kuwaomba radhi Watanzania, kufutia kitendo cha serikali yake, kushindwa kutimiza ahadi ya kuibua ajira 1,000,000, kama alivyokuwa ameahidi katika kampeni zake za mwaka 2005...

http://www.globalpublisherstz.com/habari_mbalimbali/

CCM huwa wanaandika tu ilani bila kujua kama inatekelezeka au laa, sasa haya ndiyo matatizo yake baada ya miaka 4 na nusu hamna kitu chochote kilichofanyika.

Kama mlimnukuu vizuri JK siku ya maswali Live pale TBC1 alisema ilani haitekelezeki. kwa hiyo cha msingi ni sisi kujua kwamba CCM huwa ni wasanii na ukweli umejidhihirisha hapa, sasa tusubiri 2010 watakuja na mbinu ipi maana wale ni mafia wa kutunga mbinu za medani.

Kinachotia moyo kidogo ni kwamba wananchi wameanza kuerevuka kiasi na wanaweza kuchambua mambo ya siasa na elimu ya uraia inaanza kuwaingia ukiringanisha na mwaka 2005 wakati wa uchaguzi Mkuu.
 
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
3,874
Likes
314
Points
180
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
3,874 314 180
Sawa, ajira zinakuwapo lakini wapambe wake wanazinywa kwa kuwapa ndugu zao. Mpaka waishe hao ndio walala hoi wataziona. Tena ukionyesha harufu ya upinzani ndio ufe kwanza ndipo upate, maana kwa Tanzania ya leo mpinzani ni kama shetani na CCM ni mungu (sio Mungu)

Leka
kaka naona upo mbali, hatuongelei ajira unazofikiria wewe, tunaongelea ajira Million moja kwa vijana ambao hawakubahatika kupatia mfumo wa elimu yetu na hawa ni vijana waliko mitaani wanahangaika hawajui wafanye nini kujikwamua na maisha yao. Muwe mnasoma mnaelewa kabla ya kuanza kuandika vitu hamvielewi.
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
238
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 238 160
Hayo hayo ya kutotekelezeka kwa ilani za CCM aliyasemaga Mkapa. Sijui kwa nini mpaka leo Watanzania wanaendelea kuwaamini wana CCM na kuwapa kura wakati wanajua ilani zao za uchaguzi ni uongo mtupu.
 
B

Boramaisha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
820
Likes
7
Points
0
B

Boramaisha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
820 7 0
Hayo hayo ya kutotekelezeka kwa ilani za CCM aliyasemaga Mkapa. Sijui kwa nini mpaka leo Watanzania wanaendelea kuwaamini wana CCM na kuwapa kura wakati wanajua ilani zao za uchaguzi ni uongo mtupu.
Jasusi,

Wakati wa kampeni za JK kutaka achaguliwe kuwa rais wetu nilibahatika kukuta watu fulani influential wakizungumza na kushangaa jinsi ambavyo 'Rais mtarajiwa' anavyomwaga ahadi kila anakopita na kila akisimama jukwaani kujinadi. Swali likawa, "hivi kweli akiingia madarakani anaweze kuzitekeleza ahadi zote hizo?" Majibu tunayapata sasa. Kama sikosei kuna mahali JK aliiruka hiyo ilani ya uchaguzi na kudai kwamba hakuiandika yeye ile ni ya Chama cha Mapinduzi! Kwa maana kwamba wakati inatayarishwa yeye hakuhusika. Aliwezaje kubeba na kuanza kunadi kitu ambacho alikuwa hakiamini?! Halafu cha kushangaza hajifunzi kutokana na makosa, bado anapozungumza anaendelea kuahidi!!
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,380
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,380 280
CCM yaogopa ukweli wa Dk. Slaa

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa.

ALIPOKUJA na orodha ya walioitwa "watafuna nchi," ambayo iliwaacha uchi karibu vigogo wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wenye akili walitia akilini.

CCM ambao ni watuhumiwa wakuu, kama kawaida yao, walisema Dk. Willibrod Slaa ni mwongo na mnafiki. Lakini kadri siku zilivyokwenda na mambo kuwekwa hadharani, wanafiki, waongo, wababaishaji, wezi na mafisadi walijulikana.

Huyo si mwingine bali shujaa wa kupambana na kufichua ufisadi, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Slaa.

Sasa baada ya Dk. Slaa kuipua madai mapya ya CCM kukwepa kulipa kodi kwenye ununuzi wa magari, haraka ikajengwa ngome na kukanusha na kutishia kumfikisha mahakamani.

Yako wapi sasa? CCM wameona huu ni mwiba mwingine mkubwa na mkali. Wamefyata na kuanza kupingana hadharani hovyohovyo kama njia ya kukwepa kuwajibishwa.

Mwanzo aliposema kuna ujambazi benki kuu kwenye fuko la madeni ya nje (EPA), unaowahusisha wakubwa wa serikali ya sasa na iliyopita, CCM na serikali yake walimwita mwongo na mbea mkubwa. Ilipothibitika walifyata.

Hivi sasa wananchi wengi wanaamini kuwa serikali ya sasa ama ni tunda la ufisadi wa EPA au kimelea chake. Nani apinge au kujibu wakati ukweli uko hadharani?

Rais Kikwete alikuwa kwenye orodha ya aibu ya “watafuna nchi.” Hakujibu. Angejibu nini wakati kila kilichosemwa na Slaa kilikuwa ukweli ambao hauwezi kukanushwa.

Kuna wapumbavu na mafisadi waliosema eti Kikwete na CCM wakimjibu Slaa itakuwa sawa na mtu kuvuliwa nguo na mwehu halafu akaanza kukimbizana naye.

Pamoja na usemi huu kuwa mfu, unathibitisha jinsi gani nchi ilivyojaa vihiyo na waroho wasio na hata ubongo. Hata ndege wanajua kuwa Tanzania imo msambweni.

Nguvu ya ufisadi imemeza utu, uongozi, busara hata akili. Wananchi sasa wanajua kuwa nchi ina ombwe la uongozi na watawala wetu ni walafi na wachafu; wanaoweza kula kwa mikono na miguu, tena bila kunawa.

Katika suala la hivi karibuni sikiliza viongozi wanavyoumana. Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, John Chiligati alisema Dk. Slaa atafikishwa mahakamani.

Siku mbili baadaye Amos Makala anasema hakuna kitu kama hicho. Alikaririwa akisema, “Mimi ninayezungumza hapa ni Katibu wa Fedha na Uchumi. Ndiye mwenye dhamana ya kuzungumzia suala hili kwa niaba ya CCM.” Aibu.

Chiligati na Makala wana ofisi pale makao makuu madogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam; lakini kutokana na kuchanganywa na kashfa tajwa, walishindwa hata kuwa na msimamo wa pamoja. Je, chama kama hiki kinaweza kuivusha Tanzania?

Hakika CCM haina ubavu wa kumshitaki Slaa. Ikifanya hivyo itakuwa inashitaki wananchi na wataivua nguo zaidi na zaidi. Muhimu ni wananchi kutia akilini. Wakati ukifika watoe hukumu mujarabu.
Chanzo: MwanaHALISI Desemba 30, 2009.
 
Mwanaukweli

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Messages
4,511
Likes
362
Points
180
Mwanaukweli

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined May 18, 2007
4,511 362 180
It is becoming interesting as we approach the next election. Wengine tunaangalia, na interest hasa ni kama CCM itaendelea kuzoa viti vingi, kwani ignorance ya wapiga kura wetu imekuwa ndio mtaji wa CCM.
 
tgeofrey

tgeofrey

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2008
Messages
538
Likes
1
Points
35
Age
43
tgeofrey

tgeofrey

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2008
538 1 35
It is natural to be afraid of the truth no mater which part ur affiliated with
 
Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2009
Messages
490
Likes
14
Points
35
Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2009
490 14 35
Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.

Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.

Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.
 
Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2009
Messages
490
Likes
14
Points
35
Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2009
490 14 35
Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZ kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.

Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.

Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,668
Likes
5,067
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,668 5,067 280
Unaongea na watu wenye akili ndugu, ushauri wako unaotoa kwa watu sensible watakaosikiliza ushauri wako.

Bahati mbaya katika wenye akili Tanzania CCM hawana, ikifika kipindi cha uchaguzi wanazitoa akili zao na kizihamishia wanakojua wao

wana undergo metamorphosis of their brains only, from normal to abnormal, halafu wanashtuka miaka 2 baada ya kumchagua huyo kiongozi(ambaye naye ameshakuwa metamorphosized to certain creature).we need research on this area.

Sisimizi CCM hawako kwa ajili ya nchi bali njaa za kitambo

No ninasema kwa CCM wote please ijulikane hivyo; mnaowaona wasafi (hamna kitu) metamorphosis yao ilikuwa abnormal(wanaongea tu) but they belong to the same group , they eat and drink together!
 
Exaud J. Makyao

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2008
Messages
1,523
Likes
13
Points
0
Exaud J. Makyao

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2008
1,523 13 0
Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.

Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.

Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.
Wako wengi mitaani mkuu SISIMIZI.
Tatizo ni kwamba sisi wapiga kura hatuwi makini wakati wa uchaguzi.
 
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,976
Likes
230
Points
160
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,976 230 160
tatizo ni elimu......wananchi vijijini hawaelewi kitu wakisha pewa khanga. Mijini cCM wanaiba kura
 
M

msaragambo

Senior Member
Joined
Aug 6, 2008
Messages
127
Likes
5
Points
35
M

msaragambo

Senior Member
Joined Aug 6, 2008
127 5 35
Tatizo wale wenye upeo wa kuelewa hawapigi kura wanasingizia haitasaidia kitu wanaachia wale wenaodanganyika na khanga na pilau
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,668
Likes
5,067
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,668 5,067 280
tatizo ni elimu......wananchi vijijini hawaelewi kitu wakisha pewa khanga. Mijini cCM wanaiba kura
Tatizo wale wenye upeo wa kuelewa hawapigi kura wanasingizia haitasaidia kitu wanaachia wale wenaodanganyika na khanga na pilau

You guys kwanini kila kitu tunasingizia elimu? mbona mawaziri na wabunge wa CCM wana elimu nzuri tu? na yet wanamchagua JK ndani ya chama chao kuwa rais

kuna mtu anayeweza kuniambia elimu ya Mkwawa na Mirambo?
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,286
Likes
65
Points
145
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,286 65 145
hata mimi naweza kuwa kama dokta silaha...!NI KUNIWEZESHA TU!:D..na kunihakikishia ulinzi na usalama nikiropoka wasinipotezee

BTW:yule kijana ''nyepesi'' vipi?..!ameshakufa ''kisiasa yule''...!KWISHNEY
 
Gwamahala

Gwamahala

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Messages
3,936
Likes
1,413
Points
280
Gwamahala

Gwamahala

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2009
3,936 1,413 280
Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.

Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.

Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.
Mkuu Sisimizi hapo umenena.
To be frank Dr.Slaa is the only guy humo Bungeni ambaye anatoa vitu ambavyo
vinaweza kukufanya utambue ile hadhi na kazi ya Bunge kuwa ni ya kukosoa na kuirekebisha "SIRI-KALI".
Kweli tunahitaji vijana au wazee wa aina hiyo humo Bungeni hao wanaolala wote watoke jamani.
 
M

miner

Member
Joined
Dec 14, 2009
Messages
76
Likes
0
Points
0
M

miner

Member
Joined Dec 14, 2009
76 0 0
Mkuu Sisimizi hapo umenena.
To be frank Dr.Slaa is the only guy humo Bungeni ambaye anatoa vitu ambavyo
vinaweza kukufanya utambue ile hadhi na kazi ya Bunge kuwa ni ya kukosoa na kuirekebisha "SIRI-KALI".
Kweli tunahitaji vijana au wazee wa aina hiyo humo Bungeni hao wanaolala wote watoke jamani.
Kweli tunahitaji vijana inasikitisha waliochangia hoja hii ya Sofia Simba walikua ni wazee watupu vijana wako wapi ? ukweli unabaki palepale bado wazee wanahitajika mpaka vijana waondoe woga na kujiamini na wazee watabaki kuwa kisima cha hekima vijana wajifunze sasa
 
D

Domisianus

Senior Member
Joined
Aug 1, 2008
Messages
154
Likes
1
Points
0
D

Domisianus

Senior Member
Joined Aug 1, 2008
154 1 0
Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.

Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.

Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.
Excellent thoughts, well done “Sisimizi.”
But I doubt if this idea will be digested in a positive way by many of us.
My comrade, I can give a simple example which happened in 2005 in one the constituency in Lake zone, in day time most of the people were cheering for the upinzani and one of the smart guy came to me for the sake of voting for one of the strong contester, funny enough during the night, the same guy persuade me to vote the strong contester, came to me with some cap and T-shirt of CCM contestant, once I remind him, he ended up saying that he is looking for maslahi.
So if these are the type of people we’re living with, do you think that you’re splendid thought will be taken into consideration? Absolutely not!!!!!!!!!!!! 

Forum statistics

Threads 1,250,456
Members 481,354
Posts 29,733,684