Tunasubiri hatua ya pili

Wakuu huyo kawambwa ameharibu sana mfumo wa elimu,hesabu za majibu ya kuchagua,hakuna jipya hapa
 
Ngeleja,maige,mkulo,ponda,na wengine waliofanya kama wao bila kufilisiwa na kufungwa wengi wataendelea hivyo hivyo
 
Wadau
Kuna mawaziri na manaibu waziri waliotuhumiwa kutumia madaraka yao vibaya na kuiibia serikali (Sisi walipa kodi). Rais amekubali kuwa hawa jamaa ni wezi na kuwaondoa katika baraza lake la mawaziri.
- Je nini kinafuata kwa hawa jamaa?
- Je wateendelea kuwa mitaani?
- Je watendelea na ubunge?
- Je bado wanasifa za kuwakilisha majimbo yao bungeni?
- Au watapelekwa mahakamani na kuwaamulu kulipa mali walizoiba?

Naomba mawazo yenu
 
yaani umeuliza swali niliokuwa naliwaza...tungekuwa na usalama wa taifa na takukuru wanaojua kazi zao mpaka mida hii wangekuwa wameshakamatwa...
 
Kitendo cha Rais kukubali kuwaondoa kwenye baraza la mawaziri, ina maana kweli ni wezi na hivyo wanatakiwa kukamatwa, kupelekwa mahakamani na kuvuliwa ubunge wakati kezi zao zinaendelea kwa manufaa ya umma
 
Si walimsaidia jamaa kuingia madarakani kwa hela zao ndizo zilizotumika kuhonga wananchi wasioshule? Jamaa na familia yake wameifanya nchi shamba la bibi. Miradi yote mikubwa ukitaka upate kandarasi lazima upitie kwa mwanae.
 
Zitarudishwa kinyemela kama ilivofanyika kwa zile za EPA, au tume itaundwa kisha zirejeshwe kama change ya Radar(kama kweli imerudi)?
 
Well, mkuu Jasusi hapo ndo panaumiza na kusikitisha zaidi, wananchi wa kawaida wanafaidika nn kwa kuwatoa mawaziri wa awali na kuweka wengine bila hatua stahiki hasa kurejsha pesa iliyopotea ikaingia kwenye maendeleo
 
Wadau
Kuna mawaziri na manaibu waziri waliotuhumiwa kutumia madaraka yao vibaya na kuiibia serikali (Sisi walipa kodi). Rais amekubali kuwa hawa jamaa ni wezi na kuwaondoa katika baraza lake la mawaziri.
- Je nini kinafuata kwa hawa jamaa?= Nikula nakunywa kwasaaaaaaaaaaaaaaaana!
- Je wateendelea kuwa mitaani?
= Hakuna sehemu nyngne yakutanulia zaidi yakitaa
-
Je watendelea na ubunge?= Posho wamwachie nani?
- Je bado wanasifa za kuwakilisha majimbo yao bungeni?=Jibu wanalo wapiga kura wao
-
Au watapelekwa mahakamani na kuwaamulu kulipa mali walizoiba?=Wizi hawakuanza wao

Nimawazo yangu
 
Wakuu nyie ni wageni Tanzania ?
Watu wameshikwa na ngozi (kina Yona, Mramba et al...) na hakuna kinachoeleweka..., ije kuwa hizi tuhuma ?, wako wapi kina Jairo..?, ni kina nani walileta Dowans na Richmond.., vipi issue za EPA..,

wakuu nadhani sisi wabongo ni wagumu wa kukumbuka, na wepesi wa kusahau.., hawa jamaa watapeta tu na kungoja kupewa post nyingine ya ulaji soon or later
 
Back
Top Bottom