Tetesi: Kuna Mwekezaji KIA? Je, ni siri siri tena?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,711
9,000
Kumekuwa na usiri siri wa ajabu sana. Kwanza waziri alikuwa anachenga changa mpaka akabanwa na wabunge kuhusu mikataba ya KIA na kuhakikisha kiwanja kinarudi serikalini. Sasa tunasikia kuna mwekezaji kutoka Uarabuni ?. Kama ilivyokuwa bandari

Nasikia kabla ya uwekezaji wanawekwa wanzanzibari mfano kabla ya Dubai port kupewa bandari waziri Mzanzibari ndiye aliyewekwa . Sasa kabla ya uwekezaji wa KIA nasikia Kilimanjaro nako wameweka Mzanzibari sasa sijui kama haya ni ya kweli lakini kikubwa tunaomba uwazi.

Kama kuna uwekezaji tuambiwe sababu ni zipi wakati hatuna shida ya pesa ya airport ambayo imejaa watalii. Je mwekezaji analeta nini cha maana zaidi ya kuzuia soko huru pale kama ilivyokuwa kiasi kwamba tulishidwa hata kuendeleza pale KIA. Je kuna ubaya gani KIA ikawa kama Dar-es-salaam. Na watalii wote hao kwanini KIA mpango wake ni wa siri siri
 
Kumekuwa na usiri siri wa ajabu sana. Kwanza waziri alikuwa anachenga changa mpaka akabanwa na wabunge kuhusu mikataba ya KIA na kuhakikisha kiwanja kinarudi serikalini...
Mama na Wamasai hawapatani kabisa, asije akawahamisha wamasai wa pale na kuwalundika Handeni kama alivyofanya kwa wale wa Ngorongoro.
 
Kumekuwa na usiri siri wa ajabu sana. Kwanza waziri alikuwa anachenga changa mpaka akabanwa na wabunge kuhusu mikataba ya KIA na kuhakikisha kiwanja kinarudi serikalini....
Irudi Serikalini ili iweje? Ni wapi Serikali inafanya vizuri? Serikali duniani hazifanyi biashara, biashara inafanywa na sekta binafsi. Kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingara ya biashara, sera na kuzisimamia.

Hapa JKNIA tu ukienda kwenye vyoo kama una haja kubwa ni mtihani, mara nyingine zile lift za ngazi za kutembea unakuta zimekufa. Mnang'ania tu Watanzania kuona shughuli ziko chini ya Serikali lakini nyie watu wenyewe hamuko serious kwenye kazi
 
Safi kabisa! Anaupiga mwingi,hana baya maushungi,akifa hakuna kuoza.Sema nchi ya hovyo hii basi tu Mungu ndiye anayejua
 
Ndege ngapi za kimataifa zinatua KIA.?KIA ina capacity ya kuwa kiwanja kinachoshindana na JKIA lakini usimamizi mbaya wa Kadco umedumaza maendeleo ya KIA.

Ni muda muafaka sasa wapewe wawekezaji ili upanuliwe na kuwa na miundombinu ya kisasa.

Rangi ya panya haina muhimu mradi awe na uwezo wa kukamata panya.
 
Wanaokula vya umma ni wazalendo??
Maccm mna matatizo kichwani
Sasa ni wazungu au waarabu waliokuwa wakiendesha KADCO?
Mlio wengi na ubaguzi wenu si huwa mnaimba wimbo wa uzalendo.Au kwenu mzalendo ni nani?
 
Sasa ni wazungu au waarabu waliokuwa wakiendesha KADCO?
Mlio wengi na ubaguzi wenu si huwa mnaimba wimbo wa uzalendo.Au kwenu mzalendo ni nani?
Wazalendo ndo hawalipi Kodi na kutoa gawio?

Una kiwango Gani Cha elimu dogo??
 
Wazalendo ndo hawalipi Kodi na kutoa gawio?

Una kiwango Gani Cha elimu dogo??
Jibu swali nyinyi si ndio waumini wa ubaguzi na kukataa uwekezaji kwa visingizio vya uana Nchi na uzalendo na kuwaita wengine majina ya kibaguzi?

Kiwango changu cha elimu hapa sio hoja hoja ni mada iliyopo.Wisdom is chasing you but you are always faster. Dundee United.Wacha personal attacks jibu hoja.
 
Kumekuwa na usiri siri wa ajabu sana. Kwanza waziri alikuwa anachenga changa mpaka akabanwa na wabunge kuhusu mikataba ya KIA na kuhakikisha kiwanja kinarudi serikalini. Sasa tunasikia kuna mwekezaji kutoka Uarabuni ?. Kama ilivyokuwa bandari...
Vipi TEC mara hii pia watatoa tena waraka🤣🤣🤣🤣 au wesha koma na upuuzi wao?
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Irudi Serikalini ili iweje? Ni wapi Serikali inafanya vizuri? Serikali duniani hazifanyi biashara, biashara inafanywa na sekta binafsi. Kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingara ya biashara, sera na kuzisimamia...
Watu wanaongea tu hata hawafikirii , apewe muwekezaji aboreshe , serikali tangu lini ikafanya biashara
Leading airport duniani heathrow uingereza wamempa muwekezaji tena muarabu kutoka saudi arabia.
 
Jibu swali nyinyi si ndio waumini wa ubaguzi na kukataa uwekezaji kwa visingizio vya uana Nchi na uzalendo na kuwaita wengine majina ya kibaguzi?...
Naweza kujibizana na ujinga,

Kila siku mama yako anaenda uaratabuni kuomba msaada wa tsh bil 30 wakati Kuna wazalendo wanaendesha uwanja wa kia hawatoi hata senti kwa miaka zaidi ya 25
 
Back
Top Bottom