eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,227
- 16,178
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Chelsea wanatarajiwa kulamba kitita cha bilioni 434 za Kitanzania kutoka kwa wasimamizi wa ligi hiyo inayotarajiwa kumalizika wikiendi hii.
Fedha hizo ambazo ni sehemu ya zawadi ya kutwaa ubingwa pamoja na haki ya matangazo ya luninga, Chelsea imejikusanyia pesa nyingi paundi mil 150, tofauti ya bingwa wa msimu wa uliopita Leicester City aliyepata paundi 93.
Hii inafuatia kuongezeka dau la udhamini kwenye matangazo ya ndani kwenye mkataba mpya wa EPL dhidi ya warusha matangazo SkySport na BT Sports wanaorusha jumla ya michezo 168 ya ligi hiyo moja kwa moja.
Mkataba mpya wa EPL na wenye haki ya kuonyesha michezo hiyo unaonyesha kila mechi moja ni sawa na paundi mil 10.19 sawa na fedha za kitanzania bil 2.7 kwa mchezo.
Mgawanyo wa fedha hizo unaonyesha mshindi wa pili anapata paundi milioni 144, mshindi wa tatu paunid milioni 142, mgao huo unaendelea kwa timu zote na timu ya mwisho inaambulia paundi mil 97