Mlio jirani na Rais mshaurini; ni sawa kutoa zawadi lakini kutapanya pesa nyingi kiasi hiki hapana!

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,107
49,809
Juzi hapo eti Rais akitoa mil. 500 Kwa Taifa Stars kuingia Afcon, Leo tena eti anatoa mil. 92 Kwa Ndondo Cup.

Hata Kama ni Kuunga mkono Michezo,kutapanya pesa za Walipakodi Kwa wingi huu Haikubaliki.

Matokeo yake badala ya watu kufurahia inatuma ujumbe wa Moja kwa Moja kwamba anatumia pesa za Umma vibaya.

Kwa mda mfupi kutoa mil. 592 kwa Ajili ya zawadi sioni kama Ina Tija. Zawadi zitolewe ila sio Kwa wingi huu maana Kuna maelfu ya mahitaji ya watu.

Sijui washauri wa Rais wanafanya nini,kama ni mambo ya kutafuta uungwaji mkono Kisiasa ni mara mia akiwa kwenye ziara au kwenye makongamano huko watu wanakoelezea Changamoto zao akawapa hizo hela itamsaidia kuliko hii ya sasa.

Mfano uko ziarani Wananchi wamechangia majengo Yao Nguvu ikaisha hapo ndio ukichangia hata mil.100 watafutahi Kwa kutatua shida Yao.Binafsi sijafurahishwa na hili kabisa it is too much.

---
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi yake ya kuiunga mkono Ndondo Cup kwa kuchangia Tsh. mil Tsh. 92 milioni kwa Washindi wa Ligi hiyo.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa leo katika Studio za @CloudsFMTZ Mikocheni amekabidhi zawadi kwa Washindi wa Ndondo Cup ambapo mgawanyiko wa zawadi kwa Timu zilizoshiriki Ndondo Cup 2023 msimu huu kuanzia hatua ya makundi jumla yake ni Tsh. 92 milioni.

Msigwa amekabidhi fedha hizo kwenye kipindi cha #SportsXra kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ndondo Cup ni Mashindano ya mpira wa miguu yaliyoasisiwa na Clouds Media Group chini ya Mtangazaji Shaffih Dauda ambayo hufanyika kila mwaka na kuvipa nafasi vipaji vya Wakali wa soka kuanzia ngazi ya mtaa.


Screenshot 2023-09-14 101250.png
Screenshot 2023-09-14 101326.png
Screenshot 2023-09-14 101348.png
 
Tatizo anawasikiliza machawa wa Pwani , huko kigoma ndani ndani ni disaster tupu , mfano dogo Founder tz ametuonyeaha maisha yalivyo huko , Raisi unawapa mil 500 Taifa stars Kwa lengo lipi sasa , wachezaji hao ni jukumu Lao kulipanbania Taifa na sio ombi, si ndo kazi Yao bhana , na wanalipwa mshahara , asa inawaongezea hzo ili iweje , mataifa yaliyoendelea yanapambana kuhakikisha basic needs Kwa raia zinakaa poa , wala hawahangaiki na hyo mipira , Raisi anazingua Sana
 
Tatizo letu ndio hilo, kama anapenda vijana wacheze kwanini asiwaze wafike Olympics kwenye michuano ya kimataifa?
Hizo hela adundulize basi ajenge viwanja vya michezo kila shule na vilivyoporwa avinunue tena maana wamegawiana wao kwa wao

Akili zetu mbovu sana na wenzetu wanatushinda kwa kila kitu kisa ujinga
 
Michezo inasaidia sana kuokoa vijana, na ili vijana wajikite kwenye michezo lazima waone kuna matunda, ila badala ya kusapoti yeye kama yeye, angeweka mfuko na utaratibu rasmi wa kiserikali kusapot
Hapo inawasaidiaje wakati ni watu wachache kabisa wanaoenda kunufaika?
 
Michezo inasaidia sana kuokoa vijana, na ili vijana wajikite kwenye michezo lazima waone kuna matunda, ila badala ya kusapoti yeye kama yeye, angeweka mfuko na utaratibu rasmi wa kiserikali kusapot
Lazima uwepo utaratibu wa kiserikali na sio eti rais katoa zawadi inatakiwa kuwa serikali imetoa zawadi ku support michezo.
 
Tatizo letu ndio hilo, kama anapenda vijana wacheze kwanini asiwaze wafike Olympics kwenye michuano ya kimataifa?
Hizo hela adundulize basi ajenge viwanja vya michezo kila shule na vilivyoporwa avinunue tena maana wamegawiana wao kwa wao

Akili zetu mbovu sana na wenzetu wanatushinda kwa kila kitu kisa ujinga
Kwa sababu kusaidia washindi ni kusaidia kikundi Cha wachache sana
 
Inahitajika mfumo mzuri wa kusapoti michezo kwa hapa nchini, ambapo ukiwekwa mfumo mzuri wa mapato na watu wakaona kuna umuhimu wa kufatilia michezo basi hata hizo pesa za zawadi za pongezi zinaweza zikatoka katika mapato yatokanayo na michezo hiyohiyo.
 
Baada ya CCM kunajisi siasa za nchi hii, hamasa pekee ya watanzania imebaki kwenye mpira, na kwakuwa CCM imepoteza ushawishi kwenye jamii, inalazimisha kutafuta kiki kupitia kwenye soka maana ndio lenye hamasa ya watu. Nenda Mbarali kaangalie kampeni za uchaguzi zilivyododa, ndio utajua kwa kiwango gani watu wameikinai CCM.
 
Michezo inasaidia sana kuokoa vijana, na ili vijana wajikite kwenye michezo lazima waone kuna matunda, ila badala ya kusapoti yeye kama yeye, angeweka mfuko na utaratibu rasmi wa kiserikali kusapot
Hii ndio point. Rais hawezi kuamka tu na kusema ananunua kila goli million kadhaa au anatoa kiasi kadhaa kwa watu fulani.

Unless hizo hela ziwe anatoa kwenye mshahara wake. Watu wanalia na ugumu wa maisha lakini vitendo vinavyofanywa na watawala ni vyakinyama kabisa.

Wizara ya Michezo haikuwa na budget kwaajili ya timu ya taifa?
 
Alafu kwanini pesa inapotolewa wanasema ni rais katoa ? Pesa si ni ya serikali kupitia kodi zetu, Hiyo ela ingetakiwa hata kama ni kutoka itolewe na wizara ya michezo yaani iwe hivi wizara ya michezo ya toa pesa ku support ndondo cup hapo isingekuwa na ukakasi sana kwa sababu ni kazi ya wizara ku support michezo.
Haka ka utaratibu cha zawadi kameshamiri sana siku hizi...
 
Back
Top Bottom