Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,689
- 3,259
Kwa nini tunaendelea kupoteza muda kuwa au kufuatilia mfumo wa kidemokrasia na ushahidi unaonyesha wazi kuwa ni mfumo mbovu usiofaa kitu!!? Critics mmoja alisema kuwa tofauti kubwa ya mfumo wa kidemokrasia na kidikteta ni kuwa kwenye mfumo wa kidikteta walaji ni wachache na mfumo wa kidemokrasia walaji ni wengi. Kwenye mfumo wa kidikteta ili utawale unahitaji kuwaridhisha watu wachache wenye nguvu. Lakini kwenye mfumo wa kidemokrasia unahitaji kuwaridhisha watu wengi sana. Yaani kwenye demokrasia walamba asali wanakuwa wengi sana kuliko kwenye udikteta.
Ushahidi wa wazi unaonyesha kuwa nchi za kidikteta zinaendelea au zina uwezekano mkubwa wa kuendelea kuliko za kidemokrasia. Nchi kama Morocco inayoendeshwa na mfalme mwenye mamlaka yote imeendelea sana katika Afrika. Misri ni nchi iliyoendelea katika Afrika, walitaka kujaribu Demokrasia lakini waliona kabisa wanaelekea shimoni. Libya inajaribu kujenga deokrasia lakini vurugu tupu. South Africa toka ianzishe utawala wa kidemokraisa inadidimia kwa kasi ya ajabu. Nigeria na Ethiopia zipo karibu kugawanyika na demokrasia zao.
Hata hapa toka tuanze kutumia demokrasia hakuna cha maana tulichofanya zaidi ya walamba asali kuendelea kujitajirisha. Hata hatuna tofauti yeyote na nchi kama Uganda inayoendeshwa kidikteta kwa miaka zaidi ya 30. Hatuna tofauti yeyote na Rwanda. Hatuwezi kukaa na kusema kuwa kwetu au kufuatilia kwetu demokrasia kumetufaidisha hiki na kile ukilinganisha na nchi za kidikteta. Ni kweli una nchi zina madikteta na hovyo, lakini zipo nyingi zenye madikteta wanaojielewa wanaoendeleza nchi zao. Lakini kwenye demokrasia kiongozi awe mzuri au mbaya hawezi kuendeleza nchi yake. Mfumo haumruhusu kabisa.
Inabidi tukae chini na kuachana na hiki kiini macho cha Demokrasia, kinatupotezea muda. Pengine tukiumiza kichwa tunaweza kupata mfumo mzuri, lakini ukweli wa wazi ni kuwa nchi ya kidikteta ina uwezekano mkubwa kuenelea kuliko nchi yenye au inayofuatilia demokrasia.