Waziri wa Kaskazini
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 8,714
- 19,298
Ikiwa ni metali nururifu pekee inayopatikana duniani kiasili hutumiwa kwa utengenezaji wa umeme katika tanuri nyuklia. Takriban asilimia 16 ya umeme duniani hutengenezwa kwa njia hii, katika nchi kadhaa ni sehemu kubwa ya umeme.Hivi Uranium ile kwanini tusiiwekee mipango hata kama ni ya muda mrefu.
Sawa handling ni shida lakini inawezekana.
Mwanzoni mwa upatikanaji wa teknolojia hiyo katika karne ya 20 kulikuwa na matumaini makubwa ya kuwa italeta umeme nafuu kwa watu wote.
Ila tu matatizo ya takataka nyuklia na ajali hatari za tanuri nyuklia yalichelewesha maendeleo ya matumizi yake.
Tena upatikanaji wa uranium yenyewe ni tatizo kwa sababu akiba za uranium duniani zinazofaa kwa uchimbaji rahisi kiuchumi hukadiriwa kudumu kwa miaka 50-100 pekee. Bado sioni mbadala wa Stiegler's Gorge kwa sasa tuvumiliane tu, huu mradi ukikamilika utakuwa unaweza kuzalisha watt 3000+...