JembeNaNyundo
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 533
- 652
Unajua huwa nashangaa sana wanasiasa!
Utawasikia wanasema:
Ni marufuku mkulima kuuza mahindi mabichi kwa ajili ya kuchoma, mwingine atasema huruhusiwi kuuza mahindi nje ya nchi; na wapo wanaosema hamruhusiwi kufanya sherehe zinazohusiana na matumizi mabaya ya chakula. Sasa huwa najiuliza weeee hadi nachoka.
Wakati natafuta shamba, serikali iliniona nina akili; hivyo haikufanya lolote...
Wakati naandaa shamba, sikuona hata cha bwana shamba kwa sababu serikali inaamini nina akili...
Wakati napanda mbegu na kisha kupalilia serikali bado iliniona nina akili timamu.
Ila sasa shida inakuja ninapotaka kuvuna au kupangia matumizi mazao ya shamba yangu; hapo serikali inaniona sina uwezo wa kufikiri; hivyo inaanza kuingiza vikwazo kibao...