Tunapocheka Wanapolia, Tusisahau Tutaacha Kucheka na Kuanza Kulia!

Ufisadi HAUNA FAIDA NA WALA HATUTALIA KWA HILI. hizo perdiem zinawanufaisha zaidi wakubwa kuliko maskini hawa. watu walipwe mishahara yao sahihi huduma ziwepo per diem kama kunufaisha pia zinanufaisha wachache si wote. nia aibu kutetea ufisadi kwa kuwa eti ulikuwa unanufaisha wachache. wacha magufuli awafanyie kazi, washughulikiwe tu no matter wat.
 
Sawa kabisa.

Hiyo hoja nakubaliana nayo kwani nami ndivyo nilivyokuwa nafikiria.

Kama kinachotokea si nguvu ya soda basi watu wajiandae kupatwa na culture shock kubwa.

Swali ibuka ni je, watu kweli wako tayari kukabiliana na hiyo culture shock katika kile kitachokuwa kipindi cha mpito?
Mimi ni mmoja kati ya waliokuwa wanatamani sana kitokee anachokifanya Magufuli na nina muunga mkono, cha ajabu katika hatua zake za awali tu kisha nigusa kiuchumi ila nitaendelea kuunga mkono haya mabadiriko, nina ukumbi wangu wa sherehe na mikutano mkoani, mpaka sasa nimepata cancellation tatu za Semina za watu wa Halmashauri wote wanahofia kwani semina zao wanahisi zitanyooshewa vidole kutokuwa na tija, nimepoteza mapato ya kukodisha ukumbi na kuhudumia breakfast, lunch na evening refreshments
 
Pole.

Sie wengine hatuguswi kiuchumi moja kwa moja na ndo maana hatuhemuki kama wanavyohemuka wengine.
 
Mh mh kwa vile taaluma ya uandishi ni kuandika ni haki yako. Ila ulichoandika ni sawa na kuogopa kuvunja choo kilichojaa kwa kuogopa kukosa pakujisaidia, kama si akili basi ni ugonjwa!
 
Mzee Mwanakijiji

Hapa umechemka Mkuu
Kwa Maana Nyingine kwa kuwa kubanwa kwa tabaka la juu kutashusha Maumivu Mpaka kwa watu wa chini hivyo basi hao watu wa juu waachwe tu sio ???
 
Last edited by a moderator:
Hivyo viwanda tulivyoahidiwa vitajengwa mijini kwa hiyo tujiandae kulia kwani nyumba zitabomolewa kama yalivyowakuta huko China.
Ingawa wenyewe China waliondolewa kwa nguvu na wengine kuuwawa na polisi.
 
Wanalia wanyonyaji na mabwanyenye wachache, na washiraka wao tu. Wako mafisadi masikini amabo watalia pia. Fisadi ni fisadi, hata kama kama ni masikini. Alie tu maana hakuna namna.

Matunda yanaonekana haraka sana. Hospitali wanapata vitanda. Sasa hata shule zitakuwa na vyoo, maana fedha za kuchimba vyoo zitapatikana kwani hazitaibiwa tena.

Hatupashwi kabisa kusema tutalia. Kupiga vita ufisadi kunaumiza mafisadi tu na sii watu wengine. Walikokuwa wananufaika na ufisadi ni fisadi washiriki; walie kama inabidi, lakini ni wachache sana.

Naudhika sana ninaposikia waalimu wanaingia choo kimoja cha shimo na wanafunzi wao wengi sana. Fedha zipo lakini zimekuwa zinaibiwa miaka yote! Karibu Mwalimu Magufuli uwaokoe Watanzania!
 
Mwanakijiji there you are these hints must be born in mind by every tanzanian.We have to support Magufuri with all our efforts and by all means, by doing this we must be aware of the consequences. Kila kiumbe duniani kinategemeana na kingine ili kuishi.Leo wadudu wote wakifa ujue pollination ya maua ili kupata matunda nitakuwa ni tabu maana itakuwepo Wind pollination tu ambayo haiko effektive sana. Vivyo hivyo kwa Maisha yetu chain inaenda kwa kutegemeana.

Akina Ndama wasipo wapa wakongo pesa kwenye mziki hakika dada zetu hawatakula na bar Wale jamaa hawataenda. Matokeo yake kwenye bar hawatauza na viwanda vya BIA vitadoloa, huu ni mfano TU. Big up sana kwa kuwakumbusha watanzania kujua kuwa Mwenzio anaponyolewa na ww tia kichwa maji.
 
yote yatatokea lakini mwisho wa siku baada ya mfumo sahihi kutengamaa, kwa maana safisha safisha kwisha, ndio hali itakuwa safi kwa kila mtu, huwezi kuwa na maisha bora ukiwa sehemu ni chafu kwa kila kitu....
 
Jitihada ba juhudi hizo kubwa za Jpm ni muhimu kuungwa mkono licha ya baadhi ya watu kulia na wengne kucheka kwani hali ya kiutendaji, ufisadi na rushwa ndani ya Serikali ni mbaya sana hususani vijijini kwa watendaji, kata Wdc, halmashauli za wilaya ni mbaya sana hvyo kila jitihada inapaswa kuungwa mkono na Jamii
 
Mimi ni mmoja kati ya waliokuwa wanatamani sana kitokee anachokifanya Magufuli na nina muunga mkono, cha ajabu katika hatua zake za awali tu kisha nigusa kiuchumi ila nitaendelea kuunga mkono haya mabadiriko, nina ukumbi wangu wa sherehe na mikutano mkoani, mpaka sasa nimepata cancellation tatu za Semina za watu wa Halmashauri wote wanahofia kwani semina zao wanahisi zitanyooshewa vidole kutokuwa na tija, nimepoteza mapato ya kukodisha ukumbi na kuhudumia breakfast, lunch na evening refreshments

I think wewe ni mmoja ya wachache walioelewa logic ya Mwanakijiji, tunapofurahia mabadiliko tuwe tayari na kuzipokea consequences zake tusije tukaanza kupiga kelele tukiguswa sisi dagaa kwa kudhani mafisadi ni wakubwa pekee ndio wanaumia. Binafsi hii kitu mwenyewe itanigusa sana na imeshanisumbua mpaka sasa ila lazima tupokee changes coz ni for the good.

Kuna wachapisha tshet za matukio ya serikali ni watu wa chini, kuna watu wa PA, kuna wakuu wa shule wazee wa michango ya madawati hewa hao kwa uchache ni watu wa chini huku ila wataanza nao kuisoma namba. Tuwe tayari kwa hili.
 
True!!
 
Uko sahihi mwanakijiji, ila najua umeandika hivyo baada ya kuona ukawa wanafrahia hii mshike mshike, yaani roho inakuuma tena kuona kama vile ukawa hawaumiii, bila shaka ulitamani kuingia kwa magufuli ukawa waipatepate, while it's just the opposite. Pumzika kwanza bana, wote tufuatilie ligi inavyoendelea.
Kuna mahali umesema itashuka hadi chini, well, si tulitaka mabadiliko kwa wote/yote! sasa hofu ya nini, kama hatukuwa tumekaa sawa kwenye nafasi zetu ngoja yatukute

Ujinga,Umaskini,Ufisadi na Maradhi ndo yanayoisumbua TANZANIA. Kati ya hao maadui hakuna hata adui mmoja tuliyeweza Kumtokomeza 100% badala yake tunazidi kuongeza maadui.
Kwenye hii move ya MAGUFURI watakao umia ni mafisadi tu,mtu wa hali ya chini haupo atakae umia ila badala yake atapata nafuu ya Maisha.
Hawa Mafisadi walikuwa wanaiba na kuzipeleka hizo Pesa nje ya nchi hapakuwepo na impact yoyote ya unafuu wa Maisha kwa watu wa chini badala yake ilikuwa ni shida mbele kwa mbele.

Mi nakushangaa mwankijiji hivi unafikiri hizo zinazoitwa developed countries waliendelea kwa kuhendekeza rushwa. Jambo ni moja tu mtu mwenye akili na uchungu wa maendeleo wa nchi hii hawezi kuwa na wasiwasi kabisa. Cha mno na msingi ni kwa maslahi ya maendeleo ya taifa letu, mengine yote ziada tu. Leo hii wenzetu walioendelea pengo kati ya masikini na matajiri si kubwa kama letu, wafanya kazi wa sekta tofauti serikalini karibu wanalingana vipato vyao lakini sio tanzania, kisa ufisadi uliokithiri. Mimi sikupingi lakini naona hoja yako ni dhaifu kwa mtu mwenye uchungu wa maendeleo ya nchi hii. Hebu fikiri inakuaje Kenya wanakua na shirika la ndege kubwa namna ile na sisi tanzania hatuna! inakuaje Rwanda inakua na shirika la ndege lililofanikiwa kiasi kile wakati Tanzania ndege yenyewe moja na ya kukodi! Nchi hii inataka mapinduzi ya kifikra kupambana na vyanzo ya umasikini wetu. Tanzania ni tajiri sana ila mipango yetu mibovu walio juu wanajali matumbo yao tu na familia zao. Hebu fikiri inakuaje mfanyakazi wakawaida wa TRA anamiliki ghorofa 5-10? hii kweli ni haki? hivi unadhani nchi itaendelea kwa kuwafumbia macho watu kama hawa? potelea mbali hata kama walio chini nao wataathirika lakini nia na madhumuni ni kwa Nchi yetu Tanzania.

Viva magufuli endelea na kazi.

Hongera mkuu umeongea ukweli, tunataka maisha bora kwa kila mtanzania na njia pekee ya kuyafikia ni hii Magufuli anayoifanya hamna njia nyinginw
 
mie mtazamo wangu ni hivi:-
serikali na watendaji wake wabane yale matumizi ya anasa kwa mfano yale ya kukaa meeting caterer anapewa tenda kwa mamilion wakati msosi anaolisha ni wa maelfu. yale ya gari moja la serikali V8 kumsafirisha afisa mmoja kwenda mkoani kwenye kazi ilihali afisa huyu anaweza kusafiri kwa basi akabana matumizi.

lakin kufuta kabisa na kuondoa baadhi ya gharama hilo litaleta athari kubwa sana kiutendaji na kiufanisi. Pia sio busara kubana matumizi sana bila kubuni niia mbadala za kuongeza kipato. Ikumbukwe unapobana matumizi unachokifanya ni kuzungusha ela ile ile tu tena kwa kuiahirishia matumizi na si kufungua milango ya pato jipya
magufuli habani matumizi anachofanya ni kutenga vipaumbele kwa umakini , kama sherehe za bunge hela ilienda kununua vitanda, hela za sherehe za uhuru zinajenga barabara, hizo za kadi imeamriwa kulipa madeni na matumizi mengine
 
ni bora kwasasa lakini tukiimarisha uchumi na kutofautisha kati ya masikin na tajir kuwa na utofaut mkubwa itasaidia maana hali ilivyo ikiendelea kutatokea tatizo kubwa zaidi.
Ni sahihi kabisa Mkuu.Kuna athari kubwa za kiuchumi zinakuja kwa watu wa chini.Mahoteli,kumbi za starehe,baa,kumbi za mikutano,tender za serikalini nk nk,wanufaika ni watu wa chini pia.Unapokata mirija kama hii,usitegemee watu wa chini kubaki salama.Ni hatari lakini salama.
 
Sawa kabisa.

Hiyo hoja nakubaliana nayo kwani nami ndivyo nilivyokuwa nafikiria.

Kama kinachotokea si nguvu ya soda basi watu wajiandae kupatwa na culture shock kubwa.

Swali ibuka ni je, watu kweli wako tayari kukabiliana na hiyo culture shock katika kile kitachokuwa kipindi cha mpito?
Watu hatuko tayari, kwa sasa wengi wetu tumeingia kwenye mkumbo wa kushabikia tu bila kuelewa kuwa mabadiliko yatagusa kila mtu. I quote " Change, like sunshine, can be a friend or a foe, a blessing or a curse, a dawn or a dusk" - William A. Ward.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom