Tunaomba ushauri: Miaka 37 ana Mchumba wa miaka 19

Tunaomba ushauri: Miaka 37 ana Mchumba wa miaka 19

ni vema mkamuacha, apange mambo yake. najua nyie ni watu wake wa karibu ila kuna baadhi ya vitu kama hivi mkiona ameng'ang'ania msimamo wake ni bora mkamuacha.
 
Mambo ya kuoa/kuolewa huwa ni suala binafsi sana, na wala kuoa/kuolewa sio jambo la lazima ila ni hiyari. Lkn sisi waswahili tumefanya kuwa jambo la lazima au wengine wanasema sharia kabisa!
 
akimsubiri huyo ajiandae kugongewa tu. Ajiandae kisaikolojia
 
acheni ujinga kuingilia mambo ya kaka yenu
 
Kuoa na kuolewa ni Upendo tu,na mengine yafuate siyo umri kwanza kama wamevuka miaka 18+

Ushahidi unaonyesha kuwa Si kweli wanaoufuata kanuni ya A,B,C,D, na E wamefanikiwa sana katika ndoa zao.

Uzuri wa mke au Mme ni tabia kama Kupendana;maana upendo unafunika yote katika kanuni ya A,B,C,D,& E.
 
hiv mwanamke akimaliz chuo yeye atakuwa na arobain na hv ss bint ndio kwanz mbichi kabisa yeye binafsi anataraji nn hapo??... itabid akubaliane na ule msemo usemao "cha ntu huliwa na ntu chuma tu ndicho kinaliwa na kutu" la cvyo ajiandae na magonjwa ya moyo
 
Wana MMU,

Kwa niaba ya familia yetu, nimekuja kuomba ushauri wa kumahauri huyu ndugu yetu Kaka Mkubwa.
Kwa kifupi ni kaka yetu mkubwa ana miaka 37 bado hajaoa na wala hana mtoto, kiuchumi anajiweza kwa kiasi fulani.
Tatizo linakuja ana mchumba "mpenzi" wa miaka 19 na yupo kidato cha 5 na yeye ndio anasema chaguo lake ni hilo.
Kama familia tunaona hilo ni tatizo kwani Msichana alishamwambia asubiri mpaka amalize chuo kikuu ndio waanze mipango ya ndoa kisha kutengeneza Familia.
Kaka yetu kwa wazazi wa bint hajulikani "rasmi" ila bint kwetu familia inamfahamu. Tumejaribu kumshauri atafute bint ambaye yupo tayari kuanza maisha hata sasa kuliko kumsubiria huyu mwanafunzi amalize chuo ndio amuoe lakini imeshindikana yeye amesimamia msimamo wake ule ule anamsubiri bint amalize chuo.
Familia tunaona hilo ni tatizo hasa ukiangalia umri wake ni mkubwa ambao kwa mwingine angekuwa tayari ana familia anayoiendesha.
Wawo kupishana huo umri sisi hatuoni tatizo, tatizo tunaloliona ni kaka kupoteza muda wa kumsubiria bint, na mnajua wachumba wa siku hizi akishafika chuo tu.....kosa.
Bado tunaendelea kumshauri.
Nawe unamshauri nini?

muacheni atajifunza yakimtokea ........
 
mambo ya mahusiano jamani sio vyema kuyaingilia ila mmshaurini tu kama imeshindikana mwacheni atakuja kujua baadaye na itakuwa too later awaulize wenzio walivyofanyiwa na mapbinti hao walivyofika chuo hawakuwaona wa thamani tena wakawa wako gadogado hawana mbele wala nyuma anajitafutia hatari huyo bro wenu muoombeeni tu akili yake irudi vyema
 
Suala la kuoa ni suala nyeti na binafsi sana.....ni suala linalohusiana moja kwa moja na hisia za mtu.....ni suala linalotaka utulivu na umakini wa hali ya juu sana katika kulifanyia maamuzi.....kuna watu walifanya pupa ya kuoa kutokana na shinikizo la ndugu jamaa na marafiki....lakini leo hii wanajutia maamuzi hayo....na wengine wanatamani wasingechukua maamuzi hayo....

Wakati tunafikiria kuoa ni lazima tuzifirie nyoyo zetu na matakwa ya nafsi zetu kwa maana wewe ndiye utakumbana na changamoto na kadhia mbali mbali za huyo uliyemteua......kwani siri ya mtungi aijuaye kata.......
 
Ana Bachelor of Computer Science.

Mwambie window 98 imeshafutwa hivyo kuendelea kutafuta software za kuisuport ni kupoteza muda. Anunua japo window 7. Akitaka aendelea kutafuta hizo spear. by the time anapata tutakuwa window 15.
 
Ni mtu na maamuzi yake...hayo ni maisha yake. Angekuwa na haraka angeshaoa siku nyingi. Hangaikeni na Yenu achaneni na ya watu. Wakipendana waoane.
 
Back
Top Bottom