Tunaomba Sensa isaidie kutatua changamoto na kero za muda mrefu zilizopo katika maeneo yetu

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Ninaelewa kwamba sensa ni mchakato unaofanyika katika nchi ili kuhesabu idadi ya watu na makazi kwa lengo la kupata idadi ya wananchi na makazi yao ili serikali iweze kuboresha huduma mbalimbali zenye kukidhi mahitaji na idadi ya watu.

Hivyo ni ombi letu kwa serikali kwamba Sensa iweze kusaidia katika kutatua changamoto nyingi na kero kubwa zilizopo katika maeneo yetu katika swala zima la kuchochea miradi mbalimbali ya kimaendeleo. Pamoja na kuongeza fursa ajira kwa vijana waliopo mitaani bila ya shughuli yoyote.

Hivyo sensa hii ikawe chachu ya maendeleo bora kwa kila sekta ambapo ni pamoja na Kuboresha miundombinu ya elimu Ikiwa ni kuongeza majengo na Vifaa vya kufundishia pamoja na kuongeza idadi ya walimu wenye ujuzi katika masomo mbalimbali.

Pia Iwe ni chachu ya maendeleo kwa sekta nyingi ikijumuisha sekta za afya, Sekta za nishati na madini, Pia sekta za afya na sekta za uchukuzi na barabara na mawasiliano katika maswala ya kuimarisha utendaji kazi wa sekta zote na kuhakikisha kuna usumamizi mzuri Wa fedha na rasilimali zinazopatikana ili ziweze kuonekana na kuwezesha katika ujenzi wa taifa bora.

Hakika ni wajibu wa kila raia na viongozi mbalimbali kuhakikisha sensa inafanyike katika maeneo yote bila ya vikwazo vyovyote vinavyoweza kujitokeza.

NI MUDA YA KUHESABIWA ILI KUPATA TAKWIMU ILI TUJUE KWAMBA JE?? TUPO WA NGAPI ILI MIRADI MBALIMBALI INAPOANZISHWA IWEZE KUKIDHI UHITAJI UNALINGANA NA IDADI YA WATU ILIYOPATIKANA KIPINDI CHA SENSA.
ASANTE.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Unamaanisha mchakato mkoa wa Chato usubiri mchakato wa sensa pia?
 
Katiba mpya kwanza kuhesabu baadae. Msituchoshe!!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom