Tunaokolewa kwa Imani sio kwa kufuata Sheria

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
8,988
Reaction score
11,862
Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.

Tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo na si kwa matendo ya sheria. Wokovu ni kwa neema kupitia imani ya Yesu Kristo, si kwa jitihada za kufuata sheria.

YESU ANASEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.

KUSHIKA AMRI KIKAMILIFU KUNAKUJA BAADA YA KUMPENDA YESU

KAZI YA SHERIA
1. Sheria huonyesha dhambi, ila haiondoi dhambi
2. Mtu mwenye dhambi hawezi kusamehewa kwa kuanza kufuata sheria bali ataepuka dhambi mpya huku akiwa na zile dhambi za mwanzo.

Yesu ndiye njia ya kweli na uzima. Na moja ya uzima ndio pamoja na uzima katika mwili yaani kuangamiza tamaa zote za mwili ambazo ni uzinzi, uuaji, uasherati, ibaada za sanamu, uongo, wizi, ujambazi, ulevi, fitina, ubinafsi, uchawi, mawazo mabaya, tamaa mbaya, uchafu, ufisadi, ugomvi, wivu, hasira, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.

Basi ukisha kuwa na imani katika Yesu Kristo anakupatia kiongozi yaani Roho Mtakatifu atakaye kuongoza katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi kwasababu upo ndani ya Kristo Yesu yaani tumeusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake mbaya.
 
Ni neema kubwa sana kuelewa hili somo, Wakristo wengi kwenye hili wanaona malue lue

this knowledge will lift up your spiritual lank from one level to another
 
Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.

Tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo na si kwa matendo ya sheria. Wokovu ni kwa neema kupitia imani ya Yesu Kristo, si kwa jitihada za kufuata sheria.

YESU ANASEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.

KUSHIKA AMRI KIKAMILIFU KUNAKUJA BAADA YA KUMPENDA YESU

KAZI YA SHERIA
1. Sheria huonyesha dhambi, ila haiondoi dhambi
2. Mtu mwenye dhambi hawezi kusamehewa kwa kuanza kufuata sheria bali ataepuka dhambi mpya huku akiwa na zile dhambi za mwanzo.

Yesu ndiye njia ya kweli na uzima. Na moja ya uzima ndio pamoja na uzima katika mwili yaani kuangamiza tamaa zote za mwili ambazo ni uzinzi, uuaji, uasherati, ibaada za sanamu, uongo, wizi, ujambazi, ulevi, fitina, ubinafsi, uchawi, mawazo mabaya, tamaa mbaya, uchafu, ufisadi, ugomvi, wivu, hasira, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.

Basi ukisha kuwa na imani katika Yesu Kristo anakupatia kiongozi yaani Roho Mtakatifu atakaye kuongoza katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi kwasababu upo ndani ya Kristo Yesu yaani tumeusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake mbaya.
Dhambi yangu kubwa ni uasherati, sijui naiachaje.
 
Sijakuelewa hapo kwa hiyo ukiwa na imani tu hata kama unatenda matendo maovu ni sawa tu au?

La hasha! Ukiwa na imani ya kweli kwa Yesu Kristo haiwezi kukuruhusu uendelee tu na matendo maovu.

Wokovu ni kwa imani, maana yake ni kwamba hatuokolewi kwa kufuata sheria au kujilazimisha kwa nguvu zetu.

Lakini imani ya kweli huzaa mabadiliko, mtu akimwamini Yesu kwa dhati, maisha yake hubadilika; anaanza kuacha yale maovu taratibu kwa msaada wa Mungu.

Imani ya kweli = wokovu + maisha mapya yanayoacha dhambi.
 
SAWA TUKISHA KUOKOLEWA KWA IAMANI NA KUOKOLEWA KWA NEEMA BAADA YA HAPO SASA AU TUKIISHA KUPOKEA HUO UPONYAJI BAADA YA HAPO SASA ,

BAADA YA HILO SASA HAISHII HAPO...UNAFUATIWA NA WAJIBU TUNA WAJIBU WA KUFUATA NA KUFANYA NA KUMTII MUNGU NA SHERIA ZA MUNGU NA MAPENZI YA MUNGU.

HAI ISHII HAPO TU....BADO NA SISI TUNA WAJIBU WA KUFANYA NA KUFUATA...SHERIA YA MUNGU,MAPENZI YA MUNGU,AMRI ZA MUNGU,NENO LA MUNGU.

ambapo ni KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU..YA KUTOKUTENDA DHAMBI TENA.

Yn 8:11
Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.

Yn 5:14
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.

Ebr 12:14
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.

Zab 16:3
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.

TUJIEPUSHE NA DHAMBI MANA DHAMBI INATUTENGA NA MUNGU,DHAMBI NI MAUTI..

KWELI NEEMA IPO,IMANI IPO...LAKINI TUISHI MAISHA YA KUJITENGA NA DHAMBI NA KUMPINGA SHETANI.
 
Yesu alisema mkinipenda mtazishika amri zangu. I don't know how to Love.
Moyoni mwangu nampenda Yesu, kwasababu yeye ni mkombozi wangu, lakini nashindwa Kuacha uasherati.
Ukiona mtu anafundisha mafundisho ambayo yana pingana na maandiko mengine ujue ni muongo huyo.
 
Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.

Tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo na si kwa matendo ya sheria. Wokovu ni kwa neema kupitia imani ya Yesu Kristo, si kwa jitihada za kufuata sheria.

YESU ANASEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.

KUSHIKA AMRI KIKAMILIFU KUNAKUJA BAADA YA KUMPENDA YESU

KAZI YA SHERIA
1. Sheria huonyesha dhambi, ila haiondoi dhambi
2. Mtu mwenye dhambi hawezi kusamehewa kwa kuanza kufuata sheria bali ataepuka dhambi mpya huku akiwa na zile dhambi za mwanzo.

Yesu ndiye njia ya kweli na uzima. Na moja ya uzima ndio pamoja na uzima katika mwili yaani kuangamiza tamaa zote za mwili ambazo ni uzinzi, uuaji, uasherati, ibaada za sanamu, uongo, wizi, ujambazi, ulevi, fitina, ubinafsi, uchawi, mawazo mabaya, tamaa mbaya, uchafu, ufisadi, ugomvi, wivu, hasira, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.

Basi ukisha kuwa na imani katika Yesu Kristo anakupatia kiongozi yaani Roho Mtakatifu atakaye kuongoza katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi kwasababu upo ndani ya Kristo Yesu yaani tumeusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake mbaya.
Imani na sheria haviokoi bali akili na kujitambua mwanangu. Msipende na kuzoea kukariri maneno ya wengine bila kufikiria wala kuhoji mtaliwa mkijiona wakati huo nyuma hamkuwa hivyo.
 
La hasha! Ukiwa na imani ya kweli kwa Yesu Kristo haiwezi kukuruhusu uendelee tu na matendo maovu.

Wokovu ni kwa imani, maana yake ni kwamba hatuokolewi kwa kufuata sheria au kujilazimisha kwa nguvu zetu.

Lakini imani ya kweli huzaa mabadiliko, mtu akimwamini Yesu kwa dhati, maisha yake hubadilika; anaanza kuacha yale maovu taratibu kwa msaada wa Mungu.

Imani ya kweli = wokovu + maisha mapya yanayoacha dhambi.
Ukiona mtu anafundisha mafundisho yanayo pingana na maandiko mengine ujue ni muongo huyo unaposoma maandiko jaribu kusoma kwenye maelezo tofauti tofauti ili ujue yanamaanisha nini sio unasoma kidogo alafu unakuwa na tafsiri batili ambayo inapingana na mafundisho mengine.

Tuttumie tu akili za kawaida haikuitaji hata uwe na elimu ya darasa la saba ili uweze kuelewa.

Sheria ni muongozo wa mamlaka flani, mungu anayo mamlaka na ni mfalme, hata Tanzania inayo mamlaka na inaraisi lakini mamlaka lazima iwe na sheria. kwahiyo mamlaka ya mungu inasheria au utaratibu flani wa kufuata, mfano usiuwe, usizini, n.k

Nje ya hapo kwasababu hizi sheria hazikuongozi kwenye uovu hazikuongozi kwenye kukana imani yako hakuna sababu za msingi za kuzijadiri au kuzikataa hakuna andiko linalo taka uzikatae kwani sheria hizo zimekuambia usizini kwani shida ikwapi hapo hebu tumia ubongo wako vizuri sheria hii inatatizo ?

Mafundisho hayo ya kuzikataa amri za mungu yanapingana na maandiko, je maandiko yasemaje kuhusu amri hizo ?

Marko 10:17-21
17 Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?

18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.

21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

JIBU:

Mtu huyo kwenye fungu hilo hapo juu alishika amri za mungu tangu utoto wake, yesu amemuuliza kuhusiana na nazo alipoona amezishika akamwambia nifuate, hivyo huwezi kumfuata yesu bila amri za mungu.

Inamaana huwezi kwenda mbinguni bila kuzishika amri za mungu, sasa jiulize kwanini mwalimu wako muongo muongo anakufundisha uzikatae wakati hazina ubaya wowote bali zina kuonya usifanye mambo mabaya kama kuzini, kuiba, kuuwa alafu mwalimu wako mbumbumbu anakuambia usizishike kwasababu hataki huende mbinguni anajua siku ukizishika utaenda mbinguni.
 
Ukiona mtu anafundisha mafundisho yanayo pingana na maandiko mengine ujue ni muongo huyo unaposoma maandiko jaribu kusoma kwenye maelezo tofauti tofauti ili ujue yanamaanisha nini sio unasoma kidogo alafu unakuwa na tafsiri batili ambayo inapingana na mafundisho mengine.

Tuttumie tu akili za kawaida haikuitaji hata uwe na elimu ya darasa la saba ili uweze kuelewa.

Sheria ni muongozo wa mamlaka flani, mungu anayo mamlaka na ni mfalme, hata Tanzania inayo mamlaka na inaraisi lakini mamlaka lazima iwe na sheria. kwahiyo mamlaka ya mungu inasheria au utaratibu flani wa kufuata, mfano usiuwe, usizini, n.k

Nje ya hapo kwasababu hizi sheria hazikuongozi kwenye uovu hazikuongozi kwenye kukana imani yako hakuna sababu za msingi za kuzijadiri au kuzikataa hakuna andiko linalo taka uzikatae kwani sheria hizo zimekuambia usizini kwani shida ikwapi hapo hebu tumia ubongo wako vizuri sheria hii inatatizo ?

Mafundisho hayo ya kuzikataa amri za mungu yanapingana na maandiko, je maandiko yasemaje kuhusu amri hizo ?

Marko 10:17-21
17 Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?

18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.

21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

JIBU:
Inamaana huwezi kwenda mbinguni bila kuzishika amri za mungu, sasa jiulize kwanini mwalimu wako muongo muongo anakufundisha uzikatae wakati hazina ubaya wowote, hataki huende mbinguni anajua siku ukizishika utaenda mbinguni.

Sasa mbona umethibitisha mwenyewe kwamba hiyo sheria isingeweza kumsaidia huyo mtu kuingia Mbinguni mpaka Yesu aliposema umepungukiwa na kitu kimoja uza kila ulicho nacho kisha njoo unifuate (kumfuata Yesu maana yake ni kumwamini).
 
Imani na sheria haviokoi bali akili na kujitambua mwanangu. Msipende na kuzoea kukariri maneno ya wengine bila kufikiria wala kuhoji mtaliwa mkijiona wakati huo nyuma hamkuwa hivyo.

Ni kweli akili na kujitambua ni muhimu sana kwa maisha ya kila siku, lakini haviwezi kufuta makosa ya zamani. Vinaweza kukuonyesha kosa na kukufanya utamani kubadilika, lakini havina nguvu ya kukusamehe au kukufanya mpya kabisa.

Mfano: fikiria mtu amehukumiwa kwa kosa kubwa mahakamani. Anaweza kujitambua na kukiri kosa lake, anaweza kuamua kuishi maisha mapya, lakini bado hukumu iko pale pale. Akili na kujitambua havibadilishi hukumu aliyopata. Lakini kama Rais au mfalme akitoa msamaha, hukumu yote inafutwa na mtu anaachiwa huru.

Vivyo hivyo, katika maisha ya kiroho, akili na kujitambua ni mwanzo tu wa kuona kosa, lakini msamaha wa kweli hupatikana kwa imani ya kweli kwa Yesu Kristo. Yeye ndiye mwenye mamlaka ya kufuta makosa yote na kumpa mtu maisha mapya.
 
Sasa mbona umethibitisha mwenyewe kwamba hiyo sheria isingeweza kumsaidia huyo mtu kuingia Mbinguni mpaka Yesu aliposema umepungukiwa na kitu kimoja uza kila ulicho nacho kisha njoo unifuate (kumfuata Yesu maana yake ni kumwamini).
Mtu huyo alizishika amri za mungu kwanza kabla ya kumfuata yesu, inamaana kuzishika amri za mungu ni hatua ya kwanza kabla hujamfuata yesu, dogo au nikupe na unabii wa wasiku za mwisho ili tuone kama mtu unaweza kwenda mbinguni bila kuzishika amri za mungu ?
 
Ni kweli akili na kujitambua ni muhimu sana kwa maisha ya kila siku, lakini haviwezi kufuta makosa ya zamani. Vinaweza kukuonyesha kosa na kukufanya utamani kubadilika, lakini havina nguvu ya kukusamehe au kukufanya mpya kabisa.

Mfano: fikiria mtu amehukumiwa kwa kosa kubwa mahakamani. Anaweza kujitambua na kukiri kosa lake, anaweza kuamua kuishi maisha mapya, lakini bado hukumu iko pale pale. Akili na kujitambua havibadilishi hukumu aliyopata. Lakini kama Rais au mfalme akitoa msamaha, hukumu yote inafutwa na mtu anaachiwa huru.

Vivyo hivyo, katika maisha ya kiroho, akili na kujitambua ni mwanzo tu wa kuona kosa, lakini msamaha wa kweli hupatikana kwa imani ya kweli kwa Yesu Kristo. Yeye ndiye mwenye mamlaka ya kufuta makosa yote na kumpa mtu maisha mapya.
Hapo unapo amua kubadilika lazima kuna lifestyle unabadirisha lazima kuna utaratibu unabadirisha

mfano

ulihukumiwa ukiwa unauwa, sasa umeamua kubadilisha life style ukawa au uwi watu unakuwa tayari unashika sheria au utaratibu flani
 
Yesu alisema mkinipenda mtazishika amri zangu. I don't know how to Love.
Moyoni mwangu nampenda Yesu, kwasababu yeye ni mkombozi wangu, lakini nashindwa Kuacha uasherati.

Ni kweli Yesu alisema mkinipenda mtazishika amri zangu. Sasa unavyojiuliza ‘I don’t know how to love,’ fahamu kwamba kumpenda Yesu si jambo la hisia pekee, bali ni kumwamini na kumkubali katika maisha yako. Upendo kwa Yesu unamaanisha imani ya kweli kwake, na imani hiyo ndiyo inayozaa nguvu ya kuacha dhambi zile zilizo katwazwa na sheria.

Unaposema moyoni unampenda Yesu kwa sababu ni Mkombozi wako, hiyo ni hatua nzuri sana. Lakini shida ni kwamba unajikuta bado unasumbuliwa na uasherati. Hapa ujue huendi kinyume na maneno ya Yesu, bali unaonyesha kwamba bado unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu. Kwa sababu kwa nguvu zako binafsi huwezi kuacha, lakini ukimruhusu Yesu akuongoze, anakupa nguvu ya kushinda.

Mfano mdogo: mtoto mdogo anapompenda mzazi wake, si lazima akazunguke kila siku akisema ‘nakupenda.’ Badala yake, upendo wake unaonekana kwa vitendo kusikiliza na kufanya anachoambiwa. Lakini mtoto huyo hawezi kufanikiwa peke yake, mzazi wake humsaidia, humwelekeza na hata kumsamehe anapokosea. Ndivyo ilivyo kwa Yesu: upendo wetu kwake siyo maneno tu, bali ni imani inayojitokeza katika matendo mapya na matendo hayo hutokea kwa msaada wake.

Kwa hiyo, usiogope wala kujiita hujui kumpenda. Ukimpenda Yesu kwa moyo wa dhati, amri zake unajikuta unazifuata kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Hata hilo tatizo la uasherati, kadri unavyomkaribia Yesu, ndivyo unavyozidi kupata nguvu ya kuachana nalo. Sio mara moja, bali hatua kwa hatua. Upendo wa kweli kwa Yesu unabadilisha tabia yako, hadi unajikuta unaacha yale uliyoshindwa kuyaacha kwa nguvu zako.
 
Back
Top Bottom