Tunanunua Simu Mbovu!

Tunanunua Simu Mbovu!

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
7,619
Reaction score
4,303
Kutokana na kichwa cha habari hapo juu ni kua hapa katika maeneo ya mijini kuna hawa mafundi saa wamekuja kugeukia ufundi wa simu na papo hapo nimeona tangazo kwenye banda la fundi saa likisema - TUNANUNUA SIMU MBOVU! chakunishangaza ni kua mimi ninasimu kama 3 hivi za siku nyingi na ni mbovu, basi nikampelekea huyu bwana fundi saa nikamwambia nimeleta simu mbovu si mnanunua kama mlivyojieleza hapa? basi jamaa akazipokea akaniambia ndio wananunua simu mbovu na nimuachie halafu nimrudie baadae, mimi nikajua nakuja kuchukua michuzi japokua kitu chenyewe ni kibovu potelea mbali anipe hela yoyote, niliporudi huyu fundi akaniambia hawezi kununua nikamuuliza kwanini? akanijibu eti simu zenyewe hazifai kwakua ni mbovu mno!!! Jamani naomba kuwasilisha hii hoja kitu kibovu ni kipi?
 
kwikwiwiwiiwiwiwiwiwiwiw pole sana mkuu haya nayo yapo.
 
sasa ungemshauri abadili tangazo lake na kuelezea vizuri ni ubovu wa aina gani anaoutaka.
 
mjini kuna mambo mengi sana kuna sehemu kwa tandale mtogole wameandika tuna nunua chochote.
sasa nilijiuliza wanawezaje kununua chochote wao wanavipeleka wapi hivyo vyovyote? lakini ndio wameshaandika tangazo.
 
Halafu nilichokuja kushtuka ni pale wakati nampatia hizo simu eti akaniuliza zina ubovu gani wakati yeye kaandika kua wananunua simu mbovu!!!
 
Kutokana na kichwa cha habari hapo juu ni kua hapa katika maeneo ya mijini kuna hawa mafundi saa wamekuja kugeukia ufundi wa simu na papo hapo nimeona tangazo kwenye banda la fundi saa likisema - TUNANUNUA SIMU MBOVU! chakunishangaza ni kua mimi ninasimu kama 3 hivi za siku nyingi na ni mbovu, basi nikampelekea huyu bwana fundi saa nikamwambia nimeleta simu mbovu si mnanunua kama mlivyojieleza hapa? basi jamaa akazipokea akaniambia ndio wananunua simu mbovu na nimuachie halafu nimrudie baadae, mimi nikajua nakuja kuchukua michuzi japokua kitu chenyewe ni kibovu potelea mbali anipe hela yoyote, niliporudi huyu fundi akaniambia hawezi kununua nikamuuliza kwanini? akanijibu eti simu zenyewe hazifai kwakua ni mbovu mno!!! Jamani naomba kuwasilisha hii hoja kitu kibovu ni kipi?
İla nawewe ulishajua simu zako mbovu kwahiyo ulitaka upate hela kwa viti vibovu,kwanza mpaka unatunza masimu ma 3 mabovu nyumbani kwako kwanini?unajaza taka tu bwana wenzio tunatupa tu,hiyo uliyopata ndıo halali kwa mtu kama wewe
 
Kwani mkuu kosa langu nini? kwakua jamaa wameandika kua wananunua si ndio maana nikawapelekea!
 
wapo watu wana kasumba ya kuhifadhi vitu kwa kufikiri vitawafaa siku za usoni.
hata mimi nina kapu kubwa huwa natunza tiketi za daladala, na koba kubwa la kuweka risiti zangu zote za vitu mbalimbali.
kila baada ya miaka 5 nachoma za daladala na kuacha zile za manunuzi ya vitu mbalimbali. haya nayo yamo.
 
Hii ni sawa na Thread moja hapa jamaa kaileta eti kuna jamaa wanarudisha Kilometer za magari nyuma! embu peruzini muone kweli ukistaajabu ya Musa basi utaona ya Firauni!
 
wapo watu wana kasumba ya kuhifadhi vitu kwa kufikiri vitawafaa siku za usoni.
hata mimi nina kapu kubwa huwa natunza tiketi za daladala, na koba kubwa la kuweka risiti zangu zote za vitu mbalimbali.
kila baada ya miaka 5 nachoma za daladala na kuacha zile za manunuzi ya vitu mbalimbali. haya nayo yamo.
Ni kweli! hata Bibi yangu anazile hela zenye matundu katikati nikimuulizaga ananiambia atakuja kuziuzaga siku moja na atapata hela nyingi tu!
 
Kweli mjini Shule!

mambo ya mjini ni darasa tosha kuna prof mmoja alisema mfn anayekaa dar mwaka ana diploma ya mambo mbalimbali, akikaa miaka kama miwili tu ana degree. ukilinganisha na yule anayekaa bushi mwamzo mwisho
 
Ni kweli! hata Bibi yangu anazile hela zenye matundu katikati nikimuulizaga ananiambia atakuja kuziuzaga siku moja na atapata hela nyingi tu!

mwache anaweza akajaziuza hata katika makumbusho. :becky:
 
Ni kweli! hata Bibi yangu anazile hela zenye matundu katikati nikimuulizaga ananiambia atakuja kuziuzaga siku moja na atapata hela nyingi tu!
Nimekuelewa sasa,(like bibi like mjukuuu)dunia imechafuka hii ndugu yangu usiamini amini tu.
 
Ni kweli! hata Bibi yangu anazile hela zenye matundu katikati nikimuulizaga ananiambia atakuja kuziuzaga siku moja na atapata hela nyingi tu!
(like bibi like mjukuuu)mtajaza mno mataka na huyo bibi yako Usawa wenyewe huu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom