Tunamuogopa Makonda ambaye tunayedhani hana uelewa?

kevylameck

Member
Nov 3, 2013
18
19
AD55BD94-8E37-4876-B1BF-85236CC4CB39.jpeg

Sun Tzu ni mwandishi wa sanaa ya vita na mikakati ya kijeshi ninayempenda na anayesifika kwa falsafa na mawazo yaliyoathiri majeshi mengi ya magharibi na mashariki ya bara la Asia.

Miongoni mwa nukuu zake nizipendazo ni hizi mbili. Moja, Tzu anasema ikiwa unamjua adui na unajijua mwenyewe, huhitaji kuogopa matokeo ya vita mia moja.

Nukuu nyingine Tzu anasema kuna njia tatu za fursa; Matukio, mwelekeo na masharti. Tzu anasema fursa zinapotokea kupitia matukio lakini ukashindwa kujibu, huna akili. Fursa zinapokuwa hai kupitia mtindo fulani na bado huwezi kufanya mipango, huna hekima, Fursa zinapojitokeza kupitia hali lakini huwezi kuzifanyia kazi, huna ujasiri.

Niongeze nyingine ya tatu. Tzu anasema ikiwa yupo salama wakati wowote uwe tayari kwa ajili yake. Ikiwa yupo katika nguvu zake za hali ya juu, mkwepe. Ikiwa mpinzani wako ana hasira ya juu, tafuta kumkasirisha, jifanye mnyonge ili apate kiburi na hasira.

Paul Makonda, Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo anachokifanya sasa labda aliwahi kumsoma Tzu ama anafahamu kile anachotakiwa kukifanya dhidi ya wapinzani wake wanaoonekana kuwa dhaifu na kuichagua njia isiyoweza kuwasaidia lolote kuelekea mbele.

Leo ameomba mdahalo wa wazi kujadili kuhusu masuala mbalimbali yanayopingwa na wapinzani wa Chama Cha Mapinduzi- CCM.

Ameomba mdahalo wa wazi na CHADEMA, akiwataka wachaguane wenyewe kwa idadi wanayotaka na wapambane na yeye mwenyewe kwenye mdahalo huo.

Bado hakuishia hapo, Makonda anawataka Chadema pia kuchagua wana habari watakaoongoza mdahalo huo - Ujasiri wa juu kabisa huu kutoka kwa Bwana Paul Makonda.

Ningekuwa mimi badala ya kejeli, matusi na dhihaka ninazoziona mtandaoni ningeitisha huo mdahalo.

Vile ambavyo tunafikiri Makonda hana uwezo wa kupambana katika hoja na kuhisi ni mjinga kama ambavyo tunasema, Mimi ningeandaa na kujiandaa na mdahalo huo kwasababu naamini ungerushwa na asilimia 90 ya vyombo vya habari vya kimataifa na kitaifa ili kudhihirisha kwamba Makonda hana uwezo na hana akili ya kupambana na wapinzani wa CCM.

Kitaaluma na kitaalamu kabisa ningewatafuta wanahabari ninaowaamini, ningewatafuta washiriki ambao ninaamini wamemzidi akili Bwana Makonda na ningeufanya mdahalo huo kuwa wa wazi ili kuonesha umma kuwa Chadema ni zaidi ya CCM katika mijadala na kujenga hoja. Ingekuwa ni fursa yangu adimu kuonesha umma kwamba Makonda si chochote, si lolote kwenye kufikiri sawia, kujenga hoja na kuwa na maarifa kuliko sisi wapinzani wake.

Tunaogopa nini? Twendeni tukaoneshe umma kwamba Makonda tumemzidi maarifa, uwezo na utashi wa kisiasa.

Mimi si muumini wa matusi na kejeli naamini katika mizani ya wazi katika kuthibitisha nani ni nani na nani ni bora kuliko mwenzie.

Nasubiri kwa hamu mtihani huo wa kutuonesha nani zaidi ya mwenzie.
 
Hakuna chombo cha habari huru cha kuwezesha huo mdahalo, Samia alitumia bbc kuiambia dunia Mbowe ni gaidi, tufanye kitu ambacho ccm hawataki kusikia, maandamano.
 
View attachment 2872152

Anachotaka kufanya Makonda kilifanywa na Waziri wa Ufaransa tycoon tapeli Bernard Tapie. Tapie akaishia kufukuzwa uwaziri Ufaransa.

History does nor repeat, but it rhymes.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom