Elections 2015 Tunamtaka rais anayetambua maendeleo yaliyofanywa na waasisi na marais waliofuata ili ayasimamie

Sep 5, 2015
80
95
Inakera sana kusikia wapinzani wakibeza na kupotosha historia yetu kama taifa kuwa kwa takribani nusu karne sasa Tanzania haijafanya lolote chini ya chama tawala,CCM. Huu ni upotoshaji mkubwa wa kumbukumbu na historia ya nchi kule tulikotoka, tulipo na tuendako.Kila mtanzania mwenye,akili na masikio anayaona,anayasikia na anayasoma mambo yaliyofanywa na serikali za awamu zote nne zilizotuongoza. Nitadhibitisha kwa uchache ili kuweka mambo sawa.

Moja ya kazi kubwa na kujivunia ni Umoja,amani,ulinzi na usalama. Mambo haya yamesimamiwa vizuri sana na kama taifa tumeendelea kubaki kuwa wamoja,tunaopendana licha ya tofauti zetu za rangi.dini,makabila,mahali tulikotoka na ufuasi wa vyama vyetu. Hivyo Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani na kimbilio la wengi majirani ambao nchi zao zimepata machafuko. Hata hili tunabeza,basi watuambie wapi panatufaa zaidi.

Pili,Ni suala la kudumisha na kuimarisha muungano wetu adhimu na adimu barani Afrika. Mpaka sasa viongozi wetu wameendelea kuwa na utashi wa kisiasa katika kuona muungano unastawi vizuri zaidi kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili na mpaka sasa zimebaki kero nne tu toka 13 zilizokuwepo mwaka 2005. Hata hivyo kupatikana kwa muafaka wa kisiasa kule Zanzibar kupitia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kumeendelea kuupa nguvu zaidi Muungano na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani.

Tatu, Mbali na kutawaliwa kwa miaka 75 na wakoloni lakini mpaka tunapata uhuru mawasiliano nchini kwetu yalikuwa duni sana maeneo machache kupitia posta yaani unaandika barua ambayo ilichukua hadi miezi mitatu kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Simu za mezani ambayo nayo ilikuwa inachukua muda sana. Tulituma pesa kupitia posta au magari ambayo ilikuwa taabu kweli. Leo nusu karne tunayobezwa serikali imeweka mazingira rafiki yaliyovutia uwekezaji wa sekta binafsi katika mawasiliano na hadi sasa zaidi ya watanzania milioni 26.7 wanatumia simu za mkononi. Kuimarika kwa mawasilano nchini kumepelekea huduma nyingi sana kufanyika kupitia simu mbali na kuwasiliana, leo unatuma pesa,unanua,unauza na unalipia huduma mbalimbali kupitia simu ya mkononi popote ulipo. Unapokea taarifa za hali ya hewa,bei za mazao katika masoko mbalimbali na hata kuperuzi mitandao. Hakika ni hatua kubwa sana.

Nne,Wigo wa upatikanaji elimu nchini umeongezeka sana. Leo kumpata mfanyakazi wa ndani ni shughuli kweli kweli yote sababu ya shule za sekondari za kata. Tulipata uhuru tukiwa hatuna chuo kikuu hata kimoja. Kabla ya Serikali ya awamu ya kwanza kuamua kutumia jengo la TANU kama chuo kikuu huku wakijenga majengo ambapo ndio leo tunakiita Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Lakini Leo Tunavyo vyuo vikuu vikubwa na bora 11 vya umma. Wanaobeza wamepita humu humu kwenye kazi zilizofanyika. Kubwa zaidi serikali ikabuni mfumo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili watoto wa watanzania maskini nao wasijekuikosa fursa hii ya elimu ya juu.

Tano, Ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami kumeifungua sana nchi yetu; kati ya mikoa kwa mikoa,wilaya kwa wilaya na maeneo yote ya mipakani na nchi jirani. Hapa kazi kubwa ilifanyika kwani katika kutawaliwa miaka 75 na wakoloni walijenga kilomita 1300 za lami mbali na uvunaji mkubwa wa maliasili zetu lakini ndani ya nusu karne serikali imejenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 17,742. Kazi hii ikisimamiwa na DK.MAGUFULI ambaye leo ndiye RAIS ajaye chini ya CCM.

Mwisho, Ni kuimarika kwa uzalishaji na uboreshaji wa miundombinu ya umeme nchini. Leo serikali imewekeza katika vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme kama vile gesi, upepo na makaa ya mawe ambapo ni muda mfupi tu ujao umeme wa uhakika tena wa gharama nafuu utakuwa umepatikana. Ujenzi wa bomba la gesi umekamilika na mitambo ya kuchakata gesi imekamilika na hata baadhi yao imeanza kuwashwa kuanza kuzalisha umeme zoezi ambalo wataalamu wa TANESCO wamesema litamalizika kabla ya mwisho wa mwezi Oktoba mwaka huu. Hapa gharama za umeme zitashuka sana kutoka dola senti 42 za kimarekani kwa uniti moja ya umeme hadi dola senti 5-8 za kimarekani. Hivyo watumiaji wa umeme sasa wanakaa mkao wa kula. Pia usambazaji wa umeme vijijini umeendelea kufanyika kwa kasi sana kwani tulipata uhuru huku 2.8% ya watanzania walikuwa wanatumia umeme leo ni 36% ya watanzania huku ilani ya CCM 2015-2020 ikieleza kuwafikishia huduma hii muhimu 60% ya watanzania waishio vijijini ifikapo 2020.

Haya ni machche tu; Hivyo nashauri kusaka kura kusiwe kisingizio cha kufuta maendeleo yaliyopatikana. Ila ifahamike kukubali mafanikio ni ustaarabu na kukiri changamoto na kueleza namna ya kuzikabili ni uongozi.
Tutafakari kabla ya kuamua. Tuepuke mihemko na ushabiki ili tuamue kwa usahihi.

along toure road near sasatel offices 4x8.jpg
 
maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,198
2,000
hapo kweny elimu na umeme huna jipya watoto wa maskini mmewajengea shule zao na wa matajir shule zao. kupitia tanesco mmewaibia watanzania kwa miaka ishirini kwa kutumia IPTL sasa mnatuua na mgao usioisha wez wakubwa mwaka huu lazima mkae bench mpate akili majiz wakubwa nyie
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
5,454
2,000
Naona umeanza tena kuwatukana wapinzani hapa, wakati kinara wa kubeza mafanikio ya serikali zilizozipita katika kampeni za mwaka huu ni Magufuli.
 
Afixa0

JF-Expert Member
Jun 16, 2015
464
500
MAGUFULI NA TATIZO LA UMEME

Ukiwa jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma ulimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM ndugu Simbachawene George huku ukihimiza kuwa apewe ridhaa kwa kuwa ni mtendaji aliyetukuka!

Kwani hujui kuwa George Simbachaweni ndiye waziri waandamizi wa umeme, nishati nyinginezo na madini? Hujui kuwa wakati ukimnadi wiki iliyopita mgao ulikuwepo? Hujui kuwa mgao umeanza hivi majuzi baada ya fedha zote kulundikiwa wewe ikiwemo za kununulia mafuta mazito? Bila shaka unajua sana tu!

Jana ukiwa Arusha ukatuhadaa kuwa wanaohusika na umeme nadhani wakiwemo mabosi Simbachawene wanakuhujumu ili usipate kura! Kweli uko serious? Hizo ni siasa za aina gani?

Mara kadhaa umekuwa ukiufanya huu usanii! Kikwete akiwa na wewe unamwagia sifa lukuki ila akiwa kanda unaichanachana serikali yake (yenu) nini maana yake?

Nimegundua kuwa hata waandishi wa habari wamechoshwa ndo maana wengi wao wameamua kukuweka kando maana unaomba kura kwa njia za ulaghai wa wazi kabisa!
MAGUFULI NI MWONGOOOOOOOOOOOOO,,CCM NI WAONGOOOOOOO
 
Kaptula la Marx

JF-Expert Member
May 10, 2015
985
170
Inakera sana kusikia wapinzani wakibeza na kupotosha historia yetu kama taifa kuwa kwa takribani nusu karne sasa Tanzania haijafanya lolote chini ya chama tawala,CCM. Huu ni upotoshaji mkubwa wa kumbukumbu na historia ya nchi kule tulikotoka, tulipo na tuendako.Kila mtanzania mwenye,akili na masikio anayaona,anayasikia na anayasoma mambo yaliyofanywa na serikali za awamu zote nne zilizotuongoza. Nitadhibitisha kwa uchache ili kuweka mambo sawa.

Moja ya kazi kubwa na kujivunia ni Umoja,amani,ulinzi na usalama. Mambo haya yamesimamiwa vizuri sana na kama taifa tumeendelea kubaki kuwa wamoja,tunaopendana licha ya tofauti zetu za rangi.dini,makabila,mahali tulikotoka na ufuasi wa vyama vyetu. Hivyo Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani na kimbilio la wengi majirani ambao nchi zao zimepata machafuko. Hata hili tunabeza,basi watuambie wapi panatufaa zaidi.

Pili,Ni suala la kudumisha na kuimarisha muungano wetu adhimu na adimu barani Afrika. Mpaka sasa viongozi wetu wameendelea kuwa na utashi wa kisiasa katika kuona muungano unastawi vizuri zaidi kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili na mpaka sasa zimebaki kero nne tu toka 13 zilizokuwepo mwaka 2005. Hata hivyo kupatikana kwa muafaka wa kisiasa kule Zanzibar kupitia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kumeendelea kuupa nguvu zaidi Muungano na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani.

Tatu, Mbali na kutawaliwa kwa miaka 75 na wakoloni lakini mpaka tunapata uhuru mawasiliano nchini kwetu yalikuwa duni sana maeneo machache kupitia posta yaani unaandika barua ambayo ilichukua hadi miezi mitatu kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Simu za mezani ambayo nayo ilikuwa inachukua muda sana. Tulituma pesa kupitia posta au magari ambayo ilikuwa taabu kweli. Leo nusu karne tunayobezwa serikali imeweka mazingira rafiki yaliyovutia uwekezaji wa sekta binafsi katika mawasiliano na hadi sasa zaidi ya watanzania milioni 26.7 wanatumia simu za mkononi. Kuimarika kwa mawasilano nchini kumepelekea huduma nyingi sana kufanyika kupitia simu mbali na kuwasiliana, leo unatuma pesa,unanua,unauza na unalipia huduma mbalimbali kupitia simu ya mkononi popote ulipo. Unapokea taarifa za hali ya hewa,bei za mazao katika masoko mbalimbali na hata kuperuzi mitandao. Hakika ni hatua kubwa sana.

Nne,Wigo wa upatikanaji elimu nchini umeongezeka sana. Leo kumpata mfanyakazi wa ndani ni shughuli kweli kweli yote sababu ya shule za sekondari za kata. Tulipata uhuru tukiwa hatuna chuo kikuu hata kimoja. Kabla ya Serikali ya awamu ya kwanza kuamua kutumia jengo la TANU kama chuo kikuu huku wakijenga majengo ambapo ndio leo tunakiita Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Lakini Leo Tunavyo vyuo vikuu vikubwa na bora 11 vya umma. Wanaobeza wamepita humu humu kwenye kazi zilizofanyika. Kubwa zaidi serikali ikabuni mfumo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili watoto wa watanzania maskini nao wasijekuikosa fursa hii ya elimu ya juu.

Tano, Ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami kumeifungua sana nchi yetu; kati ya mikoa kwa mikoa,wilaya kwa wilaya na maeneo yote ya mipakani na nchi jirani. Hapa kazi kubwa ilifanyika kwani katika kutawaliwa miaka 75 na wakoloni walijenga kilomita 1300 za lami mbali na uvunaji mkubwa wa maliasili zetu lakini ndani ya nusu karne serikali imejenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 17,742. Kazi hii ikisimamiwa na DK.MAGUFULI ambaye leo ndiye RAIS ajaye chini ya CCM.

Mwisho, Ni kuimarika kwa uzalishaji na uboreshaji wa miundombinu ya umeme nchini. Leo serikali imewekeza katika vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme kama vile gesi, upepo na makaa ya mawe ambapo ni muda mfupi tu ujao umeme wa uhakika tena wa gharama nafuu utakuwa umepatikana. Ujenzi wa bomba la gesi umekamilika na mitambo ya kuchakata gesi imekamilika na hata baadhi yao imeanza kuwashwa kuanza kuzalisha umeme zoezi ambalo wataalamu wa TANESCO wamesema litamalizika kabla ya mwisho wa mwezi Oktoba mwaka huu. Hapa gharama za umeme zitashuka sana kutoka dola senti 42 za kimarekani kwa uniti moja ya umeme hadi dola senti 5-8 za kimarekani. Hivyo watumiaji wa umeme sasa wanakaa mkao wa kula. Pia usambazaji wa umeme vijijini umeendelea kufanyika kwa kasi sana kwani tulipata uhuru huku 2.8% ya watanzania walikuwa wanatumia umeme leo ni 36% ya watanzania huku ilani ya CCM 2015-2020 ikieleza kuwafikishia huduma hii muhimu 60% ya watanzania waishio vijijini ifikapo 2020.

Haya ni machche tu; Hivyo nashauri kusaka kura kusiwe kisingizio cha kufuta maendeleo yaliyopatikana. Ila ifahamike kukubali mafanikio ni ustaarabu na kukiri changamoto na kueleza namna ya kuzikabili ni uongozi.
Tutafakari kabla ya kuamua. Tuepuke mihemko na ushabiki ili tuamue kwa usahihi.

View attachment 295502
Baadhi ya makatibu wa wilaya mbalimbali nchini wamekerwa na ugumu wanaoupata katika Ukusanyaji wa wawatu sehemu mbalimbali ikiwemo na ya urais makatibu hao wamesema jukumu walilopewa ni gumu kwa kua pesa wanazopewa ni kidogo na hazitoshi kuwashawishi watu kuhudhuria mikutano yao kwani inatakiwa uwanja uonekane umejaa kwani sh/5000-10000 wanazotoa wengine wanazikataa

Makatibu hao ambao hawakutaka majina yao yawekwe hadharani wala wilaya wanazosimamia walisema wilaya zote nchini zimepewa pesa ili kuratibu mikutano hiyo na hata kuwasafirisha watu kutoka sehemu mbalimbali ili uwanja uonekane umejaa.

Wakati mwingine hua tunapata tabu sana kwa kuwakusanya na kuwasafirisha kutoka katika maeneo husika hadi katika eneo la mkutano na kuwalipa shida ni kubwa sana wakati wa kuwapa nauli sisi tunakua hatujakabidhiwa fedha hivyo kuanza kusumbuana na viongozi wa misafara ya wagombea. Mikutano yote hasa ile ya urais inatubidi tukusanye watu wa kutosha ili uwanja uonekane umejaa na hivyo inatubidi kuwalipa pesa nyingi watu hao wanaohudhuria mkutano huo.

Makatibu hao walisema wamekua na wakati mgumu kuliko mwaka wowote walizowahi kufanya kampeni kutokana na watu wengi kutokua na mwamko na chama hicho na badala yake bila kulipwa wamekua hawafiki kwenye mikutano yao.

Naibu katibu mkuu CCM bara rajabu luwavi alipoulizwa juu ya shutuma hizo kutoka kwa makatibu hao wa wilaya wa CCM alisema hazina ukweli wowote na zina lengo la kukichafua chama huku akimsifu magufuli kua ana kipaji cha kipekee kinachovutia watu kuja wenyewe kumwangalia na kusikiliza Sera

Lakini luwavi alikiri kuna watu wana safiri umbali mrefu kwa ajili ya kumuona magufuli hivyo wao hawawezi kuwazuia kwa kua ni mapenzi yao lakini sio wanawapa pesa kama makatibu hao wanavyosema.

Chanzo: Tanzania daima
 
Fababe

Member
Jun 1, 2012
27
20
Hatutaki Porojo tunataka rais alie imara na anayeweza kukemea ufisadi na rushwa sio ushabiki tu au hela alizo nazo mgombea tunataka kiongozi bora na Mwadilifu sio kuongea ongea tu👆
 
aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
2,100

JIWE
 
Top Bottom