Duh, jamaa anagombea ubunge?
Sina CV yake rasmi lakini alisoma Mass Communications (bachelor's degree) Makerere University Kampala na kumaliza mwaka 1999, baadae akajiunga na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Jina kamili ni Deogratius Filikunjombe Haule. Labda kama wapo wawili
Injinia ulisoma MUK?
He he! Check out the avatar and decide for yourself. You?
Unajua nilikua nikiangalia hilo jengo lilikua linanikumbusha jengo fulani(administration),mbele kuna njia fulani niliokua nikipita wakati naenda East African school of Libriarianship. Kwahiyo ulikua unaishi wapi aisee? Club five ulikua unaenda? hivi mhandisi, kule kitivo cha technology ukipita geti dogo kwenda nje ndio kuna barabara ya Sir Apolo Kagwa?. Sijui ulioondoka lini aisee.
Namiss sana Club Obligato, Rock garden, Anje noir/anjemysteque,viper room(hotel equatoria) na samaki wa gaba beach.
Si yule aliekua askari polisi au? Kama ni hivi basi itapendeza mapolisi nao kutoa wagombea ubunge,mwe!!!. Tumezowea wahadhiri tu kila kukicha. Prof. Mwalyosi,Prof.Mungai,Prof. Msola, sasa waache wana Iringa wapate afande Deo(sijui tu kama anacheo gani sasa). Otherwise big up man!
Unajua nilikua nikiangalia hilo jengo lilikua linanikumbusha jengo fulani(administration),mbele kuna njia fulani niliokua nikipita wakati naenda East African school of Libriarianship. Kwahiyo ulikua unaishi wapi aisee? Club five ulikua unaenda? hivi mhandisi, kule kitivo cha technology ukipita geti dogo kwenda nje ndio kuna barabara ya Sir Apolo Kagwa?. Sijui ulioondoka lini aisee.
Namiss sana Club Obligato, Rock garden, Anje noir/anjemysteque,viper room(hotel equatoria) na samaki wa gaba beach.
Acheni hizo story zenu za Nsibirwa na Lumumba. Tupeni hoja za huyo jamaa wa Ludewa hapa.
Kyoka ggwe, kazi na dawa.
Haya basi, jamaa wa Ludewa alikuwa Livingstone Hall
Ndio nani huyo mkuu? tupe wasifu wake ili tumpigie kura hiyo siku itakapofika.
Namfahamu kidogo huyu ndugu kama ifuatavyo:-
Ni mseminari aliyesoma Kasita Seminary kule Morogoro na baadaye akahamia Forest Hill Sec. School mwaka 1993 na tukasoma darasa moja pale Forest (Form V na VI). Baadaye alienda Makerere Univ Uganda ambako alisomea Uandishi wa Habari na wakati huo huo akawa akiripoti na kutuma habari zake Redio One.
Baadaye alijiunga na World Vision Tanzania ambako alifanya kwa muda kidogo na baadaye akajiunga na Ikulu. Nilishittuka kusikia siku hizi ni Mfanyabiashara (aliacha kazi Ikulu) na ana fedha za kumtosha na alishaanza kampeni za kuwania Ubunge Jimbo la Ludewa kwa kutoa misaada mara kwa mara!
Zaidi ya hapo najua kuwa ni married na nlipokutana naye miaka 3 ilopita alikuwa na mtoto mmoja. SIjui kwa sasa.
My stand:
Mwacheni kijana ajaribu bahati yake ingawa mimi napata taabu sana mtu anapofanikiwa kidogo anawaza kutafuta Ubunge; sijui utamsaidia vipi kataka biashara zake au ndo itabidi aachane na biashara na afungamane na siasa kwa mujibu wa sheria.
Namshauri pia awe makini na siasa maana anaweza kujikuta Ubunge anakosa na anafilisika.
Ndio, hiyo ni Main Hall/ Ivory Tower. Mbele yake ni Freedom Square.
Nilikuwa mwana Gongom- Gongomes.
Hizo sehemu unazotaja nilivyokuwepo wala hazikuwa zimeanza isipokuwa Ange Noir, Silk, Viper room (I used to find that name rather vile) na hao samaki. Bila kusahau Kabalagala na Wandegeya.
Kwa kweli sina shaka/tatizo na umri wake kuitwa kamanda wa vijana. Nahisi (nionavyo mimi) ukamanda wa vijana kwenye hiki chama hauna cut-off ya umri. Kwasababu hata Mr paul Kimiti mbunge wa Sumbawanga mjini bado ni kamanda wa vijana wilyaya ya Sumbawanga mjini (Sina hakika kama amestaafu mwaka huu). Wengi wetu tutakumbuka kijana mwenzetu Kingunge Ngombale Mwiru, alivyotumikia nafasi ya ukamanda wa vijana mpaka miaka ya hivi karibuni. Umri sio issue kabisa kule chamani!!!