Click_and_go
JF-Expert Member
- Nov 21, 2010
- 451
- 5
Ni miezi miwili imepita watanzania lazima mtaanza kumkumbuka DR.Slaa mtu makini na aliyekuwa na nia ya dhali ya kuibalisha tanzania ki uongozi na kuwakomboa ninyi kwenye wimbi la umaskini na kuporwa raslimali za nchi yenu.
Leo yote aliyoyasema wakati wa kampeni ndiyo hayo hayo yanatokea ni kama alikuwa amefuniliwa na mwenyezi mungu kuja kutuokoa sisi watu wake, leo hii mnaona tatizo kubwa mno la uongozi wa nchi yetu. Huhitaji elimu hata moja kujua kwamba tatizo hili sasa ni sugu na lilipofikia pahala halina matibabu (Donda ndugu), viongozi wanakataa kuwajibika hata kwenye makosa ambayo yapo wazi wazi ya kiutendaji na kibaya zaidi hakuna wa kuwawajibisha.
Hivi tunaenda wapi? kwa mfano: tulio la Juzi la Mabomu waziri kwenye dhamana ya Ulinzi anasema waziwazi hatawajibika, na wakati huo huo waziri mwenye dhamana na nishati na madini naye anakurupuka na kusema mgawo wa umeme Tanzania hauishi hadi 2033 hivi jamani hii nchi ina viongozi kweli? nchi yenye madini, gesi asilia na hadi uranium unasema mgawo mpaka 2033 na bado upo madarakani?
Haya mengine ndiyo simanzi zaidi yaani watu zaidi ya 30 wanakufa, mbunge anatoa hoja kutaka jambo hili kuongelewa as emergence katika bunge, hoja inapanguliwa - sasa emergency katika taifa hili ni ipi? kumlipa dowans?
Tutamkumbuka DR. Slaa kwa sababu maisha ya mtanzania yatazidi kuwa magumu na yasiyo na matumaini kabisa.
mchango wake unaonekana!!!