Tunamkumbuka Dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunamkumbuka Dr. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ELNIN0, Feb 18, 2011.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Ni miezi miwili imepita watanzania lazima mtaanza kumkumbuka DR.Slaa mtu makini na aliyekuwa na nia ya dhali ya kuibalisha tanzania ki uongozi na kuwakomboa ninyi kwenye wimbi la umaskini na kuporwa raslimali za nchi yenu.

  Leo yote aliyoyasema wakati wa kampeni ndiyo hayo hayo yanatokea ni kama alikuwa amefuniliwa na mwenyezi mungu kuja kutuokoa sisi watu wake, leo hii mnaona tatizo kubwa mno la uongozi wa nchi yetu. Huhitaji elimu hata moja kujua kwamba tatizo hili sasa ni sugu na lilipofikia pahala halina matibabu (Donda ndugu), viongozi wanakataa kuwajibika hata kwenye makosa ambayo yapo wazi wazi ya kiutendaji na kibaya zaidi hakuna wa kuwawajibisha.


  Hivi tunaenda wapi? kwa mfano: tulio la Juzi la Mabomu waziri kwenye dhamana ya Ulinzi anasema waziwazi hatawajibika, na wakati huo huo waziri mwenye dhamana na nishati na madini naye anakurupuka na kusema mgawo wa umeme Tanzania hauishi hadi 2033 hivi jamani hii nchi ina viongozi kweli? nchi yenye madini, gesi asilia na hadi uranium unasema mgawo mpaka 2033 na bado upo madarakani?


  Haya mengine ndiyo simanzi zaidi yaani watu zaidi ya 30 wanakufa, mbunge anatoa hoja kutaka jambo hili kuongelewa as emergence katika bunge, hoja inapanguliwa - sasa emergency katika taifa hili ni ipi? kumlipa dowans?

  Tutamkumbuka DR. Slaa kwa sababu maisha ya mtanzania yatazidi kuwa magumu na yasiyo na matumaini kabisa.
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wakati tunamkumbuka Dr.Slaa tusisahau kushindwa kwa Upinzani kushirikiana na kumsimamisha mgombea mmoja kwa ajili ya kuunganisha nguvu kuitoa CCM ndiko kunakoifanya CCM kuwa na jeuri waliyonayo na watakayokuwanayo kwa muda mrefu.

  Usisahau kuwa nchi nyengine wananchi wake wanapochukizwa na watawala na pale maji yanapowafika shingoni huamua kuwawajibisha wasiowajibika. Unamkumbuka Ben Ali? Mubarak?.....sisi bado tunalinda uchovu wetu...amani na utulivu.

  Lakini usisahau pia kuwa Mbowe alijua kuwa si presidential candidate makini, kwa hiyo ujio wa Dr. Slaa ulikuwa ni chaguo zuri lakini pia ilikuwa ni kumtoa kafara. Pia uamuzi wa kukurupuka.Hata hivyo hili lilinogesha uchaguzi wa Rais.

  Pia Dr. Slaa alitoa tamko ambalo naona kama "atakula matamshi yake" basi anaweza kuwa branded kiaina. Alisema anagombea urais mara moja tu. Sijui kwa nini alitoa kauli hii.
  well, kama unavyosema hapa kweli tunamkumbuka Dr. Slaa.
  Jee kuna anaekumbuka Prof. Lipumba alisema nini kuhusu kuichagua CCM?
   
 3. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,460
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Watanzania wengi wanamwamini na nafikiri ni kiongozi shupavu aliyetokea kuwapo baada ya Sokoine na Mwalimu.
   
 5. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nonda si kweli kushindwa kuungana kwa wapinzani kunawapa nguvu ccm,maana ni bora kuwepo wapinzani wachache wenye nia ya kweli ya kulitumikia taifa hili,ubora wa jeshi haupimwi kwa wingi wake bali uchache wenye nia ya kweli...
  Saa ya ukombozi ni sasa
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  udini
   
 7. Tumaini edson

  Tumaini edson Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atatuongoza tu, kwani mapambano huwa hayaishi hadi haki ipatikane, vinginevyo mwisho wa uhai wake, 'NINAYO NDOTO'
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Namemkumbuka BABA WA TAIFA - nahisi kutokwa na machozi juu ya mambo yanavyoendeshwa katika nchi hii

  nakumbuka WIMBO HUU walau unipe faraja rohoni kwangu - ni majonzi kuona thing's are falling apart.


  WIMBO WA TANZANIA

  1.Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote;
  Nchi yangu Tanzania,Jina lako ni tamu sana;
  Nilalapo nakuota wewe,niamkapo ni heri mama we;
  Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote;

  2. Tanzania,Tanzania,ninapokuwa safarini;
  Kutazama maajabu,biashara nayo makazi;
  Sitaweza kusahau mimi,mambo mema ya kwetu kabisa
  Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote.

  3. Tanzania,Tanzania,watu wengi wanakusifu;
  Siasa yako na destruri,ilituletea uhuru;
  Hatuwezi kusahau sisi,mambo mema ya kwetu hakika
  Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote.
   
 9. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Nadhani bado tunamwamini, tutampa Dr Slaa kipindi kimoja atengeneze njia!
   
 10. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Atakumbukwa Mwalimu daima.:wink2: Laiti angalikuwepo atleast viongozi hawa wangekuwa na nidhamu walau ya woga tuu
   
 11. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Atakumbukwa Mwalimu daima.:wink2: Laiti angalikuwepo atleast viongozi hawa wangekuwa na nidhamu walau ya woga tuu
   
 12. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwenye kafara unamaanisha nini mkuu?
  CCM hawawezi kukubali vyama vya upinzani waungane kwa hiyo watatumia njia yeyote kuwarubuni...cuf ilionyesha dalili ya kutumika 2010.
  Wapinzani wa kweli ni wananchi wachukia ufisadi na wapenda maendeleo ya kweli na haki. Ndio wapiga kura... naamini wengi walifanya kazi yao 2010 BUT NEC imefanya mambo yake.
  Nani wa kulaumiwa?
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nilianza kumlilia dr wa ukweli slaa tangu tuliponyang'anywa ushindi wetu. Hawa wengine ni maneno tu.
  Mungu tukoe na hii balaa, maisha ni magumu leo hii twalala njaa, amsha mkono wako kabla hatujaisha na haya matatizo!
   
 14. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kwa kweli kama hali ya hewa ikikukataa imekukataa tu. Kweli Dr Slaa alikuwa chaguo la wengi hata waliochakachua sasa hivi wanajuta na dhamira zao zinawasuta. Sidhani kama wanapata usingizi wanapoangalia malalamika ya watanzania ya kila siku. Dhamira lazima iwasute tu.
   
 15. d

  dotto JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama dhamira inawasuta. PONGEZI ZA JESHI KIVIPI. Watu wanasombwa kwa malori magari ya jeshi wapi!!?? Shimbo alimsaidia 2010 election. So, mambo ndo hivyo!!
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Point noted, hivi CHADEMA iungane na chama gani hasa? TLP ya Mrema? NCCR - Mageuzi au CUF? Sioni chama chochote chenye msimano wa dhati wa kutetea maslahi ya nchi hii mbali na CHADEMA.

  Na wangekubali muungano wa kulazimisha lazima lazima kungetokea migongano ambayo ingepelekea vyama vyote kufa na CCM kurudi hapo ilipo.

  For sure CHADEMA stand on your own - sisi lazima tutawapa full support - Mwanza, Arusha, Mbeya, Shinyanga, Tunduma, Iringa, Mbeya na hapa hapa DAR ES SALAAM tupo pamoja.

  Mikoa mingine itafuata tu, tumeanza kuwapiga kwenye JOINTS (key regions) kuwakata makali.
   
 17. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Its not too late! we still have time to make changes, the question is how to make these changes to take place and be effective to obtain the desired output.
  Its real a challenge! Philosophers, mathematicians, engineers, public relationship officers, Editors and the few politicians with a good will for this nation lets take this as a challenge and bring here your solutions on how to make this government step down. Tufanyeni home work zetu jamani, hatuwezi kushindwa kupata wazo la kuafikiana ili tuokoe taifa. Hapa namaanisha tuache kulalamika tuanze ACTION. Don't care how long will take to get the right solution, lakini tuanze mchakato wa kuing'oa serikali hii.

  Nawasilisha!
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nonda japo maneno yako ni ya msingi na yana ukweli ndani yake lakini maelezo yako yana angalia upande mmoja wa shilingi. Umeongelea faida ya vyama kuungana lakini si hasara yake.

  Kwanza vyama vina itikadi tofauti. Hii ina fanya kuungana kuwe kugumu. Mimi nita unganaje na wewe wakati kila siku napingana na sera zako? Maana tukiungana ni lazima tutoke na ilani ya pamoja kwa hiyo ilaani haiwezi kuwa ya vitu chama chako kinacho taka kufanya. Je uko tayari kucompromise sera zako uingize za mwenzako? How far will you be willing to go?

  Tatizo la pili ni la kiutendaji. Kwa maana mkishinda ni lazima mugawane nafasi za uongozi. Kwa sababu ilani ni ya pamoja lazima wewe vyma vyote mdilute sera zenu ili kuingiza na za wenzenu. Sasa kwa mfano mimi nimemchagua mgombea uraisi kwa sababu chama chake kina sera fulani aki compromise hiyo sera si nitaona kaniangusha?

  Tatu ni swala la kwamba je hata wange ungana wange shinda? Ukiacha Chadema angalia kura za uraisi na hata ubunge walizo pata vyama vingine. Hata wange ungana isinge tosha kuiondoa CCM madarakani wala kuipa majority upinzani bungeni.

  Coalitions zina matatizo yake pia mkuu. they are unstable na haswa kwa nchi kama za kwetu zenye siasa za unafiki na ugannga njaa kuchomana visu mgongoni si inge kuwa kawaida? Angalia hata Uingereza sasa. Liberal Democrats wana wakati mgumu kwa sababu wapiga kura wao wana waona kama wasaliti kwa kukubaliana na baadhi ya sera za Conservatives. Conservatives nao wana hali mgumu kwa sababu hawa wezi kufanya vyote walivyo panga kufanya.

  Mimi nadhani solution ni kuimarisha vyama vyetu viwe competitive. Hiyo inaanza na vyama hivyo kuwa na uongozi makini na wenye vision. Vyama vingi vya upinzani havi tumii fursa za kujiendeleza na kujiongezea umaarufu. Angalia kama mabomu ya Gongo la Mboto. Ni vyama vingapi vya upinzani vimeonyesha leadership? Vingapi vimetoa matamshi? Vingapi vime kuwa proactive na kujaribu kusaidia waathirika iwe kwa hali au mali?
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sifa moja ya mtu kuwa jambazi ni kuua bila huruma. Sifa moja ya mwizi ni kuiba bila kujutia. Sifa moja ya kahaba ni kufanya mapenzi na watu wengi bila kuona aibu. Tusi tegemee kwamba watu wataona haya na nafsi zao kuwa suta kwa walicho kifanya. That will never happen.
   
 20. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  VIVA Dr Wa Ukweli; hivi siwezi kulipa kodi kwa kaserikali kadogo ka chadema? naona jamaa wananiibia tu bila sababu za msingi
   
Loading...