Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,425
- 829,778
Jana ilipotimu sita kamili usiku fataki zikaanza kupigwa mnazi mmoja kila mmoja alifikiri lake jirani yangu ambaye kwa vyovyote alikuwa usingizini na akiota ndoto mbaya alikurupuka mpaka nje uchi kabisa huku kashikilia taulo mkononi, dakika mbili hv alipata fahamu na kujifunga taulo lake huku akiuliza kuna nini? Najua fika wanandoa wengi na wapenzi wanalala uchi hasa huku kwenye joto lakini jamani ukumbuke kuna dharura za usiku hivyo bukta, mapajyama na nite dress visicheze mbali na kitanda, ili likitokea la kutokea usipate shida