Naungana na Invisible kulaani kwa nguvu zangu zote hizi mbinu chafu zilizopitwa na wakati za kujaribu kunyamazisha sauti ya wananchi. Nataka nimhakikishie Kiranja Mkuu kuwa kachelewa na njama kama hizi hazitafanikiwa kamwe - sana sana ndio anazidi kujiwashia petroli. Najua vitendo kama hivi tutavishuhudia sana tunavyokaribia uchaguzi lakini atambue kuwa safari hii hakuna tena mtelemko, yeye na genge lake wasubiri tu kuwajibishwa kwa kuliweka taifa letu rehani. Kutapatapa kama mfa maji hakutaisadia CCM kwani sikio la kufa halina dawa na kwa kukurupuka namna hii ndio wananchi watakavyozidi kukasirika.
Tunajua the guilty are always afraid kama alivyowahi kuandika mwandishi mashuhuri wa riwaya, James Hadley Chase lakini kama mapema hivi woga tayari umewaingia mpaka wanachanganyikiwa, mbona mbele ya safari watakuwa vichaa kabisa ! Kwa jinsi wanavyotafunana wenyewe kwa wenyewe kama tunavyoshuhudia, hata kipofu sasa anaweza kuhisi uroho na ulafi wao unavyowaendesha. Tokea tupate uhuru sijawahi kuwa na tumaini kama nililonalo hivi sasa - hivi sas natafuta tu popcorn halafu nikae niwe mtazamaji kwenye hii sinema ya bure starring manyang'au ya CCM yakimalizana - then we pick the spoils.