Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,209
Naungana na wengine wote kulaani kitendo hiki. Lakini na tofautiana na wengi wanaosema polisi wachukue hatua. Nina imani kubwa kwamba polisi wenyewe ndiyo wahusika wa jambo hili, na si ajabu ni polisi kadhaa walivaa nguo za kiraia na kuvamia eneo hilo. Naamini kwamba nia yao ilikuwa kumuua ili wasingizie majambazi. Maana ni kawaida yao, tukisema serikali ya CCM inaongozwa kidikteta dhidi ya yeyote anayoipinga tunaonekana wanafiki, wakorofi na tusiyeitakia mema nchi yetu. Ndugu zangu lets not depend on polisi, pale tunapoweza kufanya kazi wenyewe, basi tutekeleze wajibu wetu, manake to some significant measures serikali ilishashindwa siku nyingi katika vita ya kupambana na majambazi, na zaidi sana na yenyewe inashiriki katika ujambazi huo. Sasa ukitaka polisi akusaidie si ni sawa na kumwajiri chui akulindie mbuzi?