Tunakumbuka nini kuhusu August 21?

Tunakumbuka nini kuhusu August 21?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Binafsi nilijua naenda kusikiliza vitu vizito kutoka kwa Polepole. Jina lilikuwa kubwa sana kwamba ni siku inayokwenda kushangaza watu. Watu wakaunda nadharia ya vitu ambavyo viko likely kusikika muda umefika tukapata kitu gani?

Kwanza tukawekwa zaidi ya lisaa na kutoa trafik kwa youtube mmoja. Kisha usiku wa manane mtu anakuja kuongea kwa zaidi ya lisaa vitu ambavyo angeandika kwa post moja ya insta na mambo yakaenda.

Inawezekana kuna kitu, ila hii tabia ya kuaminisha watu kuna jambo zito halafu vinakuja vitu vyepesi vitapelekea mtu kuchokwa mapema.

Kama Polepole ataongea tena, aseme tu ataongea na watanzania, bila kusema kuna mazito au mepesi atayaongea. Wala hakuna kazi, isije ikawa ni mchezo wa kisiasa au ni experiement ya kuangalia watz wanatumia bundles kiasi gani wakiambiwa kuna kitu kikubwa kinakuja.
 
Wewe kwa sababu dhambi na uhalifu ni sehemu ya maisha yako bali una haki ya kusema mambo aliyosema ni madogo.
 
Polepole ni mwehu sana.

Ati 21st to remember?

Sijaona chochote cha kukumbuka, kaongea mambo yale yale tu.
 
Polepole ni mwehu sana.

Ati 21st to remember?

Sijaona chochote cha kukumbuka, kaongea mambo yale yale tu.
Mimi nilishuhudia watu wakiombwa no. Za nida na kura. Kumbe zimeingizwa kwenye mfumo moja kwa moja wa ccm. Hili Mimi sikujua nalijuwa, na nilijiuliza sana namba za Id za kura na Nida zinapelekwa wapi?
 
Philosophical thoughts by Bishop Benson Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)


WOTE TUKO NJIAPANDA: Tupande gari gani?

Humphrey Polepole ametuweka njia panda sote. Anayedhani hayuko njia panda, yawezekana tayari ni abiria wa gari la mbele. Tutafakari:

1. Kuna watu usipowasikiliza, ni hasara. Ukiwasikiliza ni hasara pia. Humphrey Polepole ni mmoja wao. Usipomsikiliza unakosa mengi. Ukimsikiliza, anakushawishi kutenguka katika basdhi ya misimamo yako. Chagua kwa hekima.

2. Nani ni bora? Shetani aletaye habari njema au malaika aletaye habari mbaya?
Tuangalie kwa makini vipa umbele vyetu:
-Mungu/Taifa/Chama
Vs
-Chama/Taifa/Mungu

Chagua kwa hekima.

3. Twaweza kumpuuza Humphrey Polepole. Je tutapuuza madhara ya kumpuuza? Chagua kwa busara kati ya kupuuza huku usiweze kupuuza madhara ya upuuzi wako.
Kama anasema uwongo anamdanganya nani? Mungu? Wananchi? Yeye mwenyewe?

4. Kama ni kweli tufanyeje? Kama ni uwongo tufanyeje? Kwa nini aliyoyasema yanafanana na imani na uzoefu wetu? Kwa nini wanaosema aliyoyasema ni uwongo hata wao wanajiona ni waongo?

5. Viapo vyetu viko njiapanda: kukiuka kiapo kwa kusema kweli au kutunza kiapo kwa kuficha ukweli? Tunapoapa twamwapia mwanadamu au Mungu? Tukishupaza shingo (Impunity), twamfanyia Polepole, Katiba, Katiba, wananchi?

6. Hatujui tumefikaje hapa. Tuna uwezo wa kujua tutokeje. Tulinde kura moyoni? Tutiki wakati imeishatikiwa? Tusubiri reform?
Tupige kura kuamua kama tuchague au tusichague?

Unyenyekevu si udhaifu
TURUDI MEZANI
UKWELI ULIOCHELEWA NI BORA KULIKO UWONGO UNAOFARIJI.
HAKUNA TOBA ILIYOCHELEWA
 
Back
Top Bottom