Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,076
Tunachojifunza kutokana na kuvuliwa uenyekiti wa ZANU PF wa Robert Mugabe ni ulevi wa madaraka na ubabe wa kufanya maamuzi akiamini kuwa kwa Katiba waliyonayo nchini Zimbabwe, hakuna mwenye ubavu wa kumng'oa!
Mugabe amejiona anaweza "kumtumbua" yeyote kwenye serikali yake na kuweza "kumreplace" na yeyote kwenye serikali yake hata kama anayempa nafasi hiyo hana sifa!
Ndicho kilichomtokea Mugabe baada ya kupokea ushauri wa mkewe Grace, kuwa nafasi ya Makamu Mwenyeki wa Chama anaitaka yeye ingawa hana sifa za kuwa Makamu Mwenyekiti, yeye Mugabe akalitekeleza ombi la Mkewe na "akamtumbua" Makamu Mwenyekiti wake Munagangwa na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona!
Wale wale waliokuwa wa kwanza kumshangilia Mugabe kwa kila aina ya "upuuzi" anaofanya, ndiyo hao hao waliompigia kura kwa wingi za kumvua uenyekiti wake!
Vivyo hivyo ndiyo yanayotokea nchini, kwa wale wale wanaoshangilia utumbuaji wa watendaji kila kukicha, wengine hata kwa kushindwa tu kujibu maswali ya Bwana Mkubwa katika ziara zake mikoani, ndiyo hao hao wanaoweza kumgeuka, mambo yakienda mrama!
Ni vyema Bwana Mkubwa wetu "asilewe" madaraka na atende kwa haki katika maamuzi yake na afuate Katiba aliyoapa kuilinda siku anaingia madarakani, hiyo ndiyo njia pekee ya kuepuka "aibu" ya kuvuliwa uenyekiti wa Chama, kulikomtokea Mugabe!
Kwa kuwa zipo "similarities" nyingi tu kati ya Mugabe na huyu Bwana Mkubwa wetu, ni suala la muda tu ndiyo utakaoamua......
Mungu ibariki Tanzania