Tunajifunza nini kwa yaliyomtokea Mugabe?

Tunajifunza nini kwa yaliyomtokea Mugabe?

HIVI NYIE LUMUMBA MNAKUNYWA MACHICHA GANI ASUBUHI HIV MUGABE KUWAONGOZA WATU ZAIDI YA MIAKA 50 SIO UTUMWA HUO MTU DAKIKA 5 AKIKAA KESHASINZIA HANA UWEZO TENA WA KUONGOZA ANAAMUA KUMPA DEMU WAKE NCHI AONGOZE MNAANZA KUSINGIZIA WAZUNGU WATU WALISHA MCHOKA KAMA TULIVYO WACHOKA NYIE CCM NDO MAANA
MNAOGOPA HII KITU ISAMBAE AFRICA NZIMA HEMBU KESHO AMKA ASUBUHI NENDA KWENYE MEZA ZA MAGAZETI MUWASIKILIZE WANANCHI WANVYO WAPONDA WATANZANIA WA SASA WANAULEWA WA MAMBO SIO KAMA ZAMANI
Mpe vidomge vyake huyo mshabiki wa Lumumba....

Hivi na suala la "kumtumbua" msaidizi wake Munagangwa nalo wana Lumumba watasema "katumwa" na wazungu kulitekeleza hilo!??
 
Annael hakuna ulichoongea maandishi mengi madudu tuu,Mugabe amegoma kula Siku mbili kama hujui ameondolewa kwenye uongozi wa chama hana sifa za kuwa Rais wao Leo ZANU PF wanamtangaza kiongozi wao na ndie atakua Rais wamesema sasa Raia watatumika kumtoa si jeshi tena..jeshi liliruhusu maandamo ya kusapoti kumtoa Bob jumamosi na jumapili huku Bob akiwekewa TV na kuona umati wa watu kila mji hawamtaki hana sapoti tens zaid ya kutoka yeye Kagoma kula anataka afe

mmh, unazipata wapi hizi taarifa??
 
Hujui hata unachitetea wewe. Zaidi sana unafanya ushabiki tu. Issue za Zimbabwe unazijua kiundani au unakurupuka tu.
Wewe ndo huzijui kabisa. Wasiomtaka Mugabe ni wananchi wa Zimbabwe. Wanaoishi maisha ya dhiki wakati Mugabe na dogodogo wanaishi kifahari kwa kufuru. Zimbabwe haikuwa na shida ya chakula, kapokea uchumi imara toka kwa wakoloni; Yaliyopo yote kayaleta Mugabe. Sasa dogodogo mnyanyasaji eti apewe nchi baada yake ? Mlitaka washangilie kama huku? Mzungu anaigiaje hapo?
 
Wewe ndo huzijui kabisa. Wasiomtaka Mugabe ni wananchi wa Zimbabwe. Wanaoishi maisha ya dhiki wakati Mugabe na dogodogo wanaishi kifahari kwa kufuru. Zimbabwe haikuwa na shida ya chakula, kapokea uchumi imara toka kwa wakoloni; Yaliyopo yote kayaleta Mugabe. Sasa dogodogo mnyanyasaji eti apewe nchi baada yake ? Mlitaka washangilie kama huku? Mzungu anaigiaje hapo?
Cha ajabu Mugabe kaleta mwenyewe balaa kwa "kumtumbua" Makamu wake wa Rais Munagangwa na nafasi yake akitaka "airithishe" kwa mke wake Grace!

Sasa nashangaa hawa propagandists wa Lumumba wanataka kuilinganisha hali inayotokea Zimbabwe kuwa eti imechochewa na wazungu wa Magharibi!
 
Similarities ya Mugabe na huyu wa kwetu ni kama zifuatazo:-

1. Anawaaminisha wananchi wake kuwa yeye Mugabe anapambana na mabeberu, na ambaye atamkosoa kwa hilo, yeye huyo siyo mzalendo na ni msaliti wa nchi hiyo

2.Utumbuaji wa papo kwa papo bila kutaja sababu za utumbuaji huo, utumbuaji ambao ni latest ambao ndiyo uliomfikisha Mugabe hapa alipo ambapo wananchi almost wote hawamtaki tena, ni utumbiaji wa Makamu wa Rais Munagangwa.

3. Wakati uchumi unadorora nchini mwake yeye anawaambia wananchi wake kuwa hao wanaosema uchumi unasinyaa wa Zimbabwe hao ni vibaraka wa wazungu na hampaswi kiwasikiliza!

Matokeo yake ni kuwa wale waliokuwa wakimshangilia ndiyo hao hao waliopiga kura za kumvua uenyekiti!
 
SOMO KUU NA LA MSINGI :

UKIWA MWANAUME KAMWE KAMWE KAMWEEE, USIMSIKILIZE NA WALA KUFUATA MAWAZO YA MKEO!!!
 
SOMO KUU NA LA MSINGI :

UKIWA MWANAUME KAMWE KAMWE KAMWEEE, USIMSIKILIZE NA WALA KUFUATA MAWAZO YA MKEO!!!
Hahaaa........😀😀

Umenicekesha sanaaaa

Haswa ukikumbuka wanaume wa shoka walitumbukia kwenye mtego wa kuwasikiliza wake wao.....

Adam alinasa kwenye mtego wa Eva....

Mwamba Samson alihadaiwa na Delila na akampa siri za nguvu zake, na baadaye maadui wakamteka

Kanumba naye amekufa shauri ya kabinti kadogo Lulu.....

Wanawake "ulaghai" wenu Mungu anawaona!
 
Tunajifunza kuwa lolote linaweza kutokea muda wowote

Hakuna kidume wa kujifanya ameshikilia maisha na akili ya wananchi wote

Hata TAWALA KUBWA za Babeli na Roma ziliangushwa.
 
Nimekuuliza umesikiliza hotu ya Rais wa Zimbabwe jana?
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia. Miaka miwili tu tumefanya uchaguzi. Na Rais wetu mpendwa anayependwa na watanzania 98% isipokuwa nyie tu wezi.

Kwenye uchaguzi mliangukia pua. Sasa mnaweweseka tu. Mlipewa matumaini makubwa mno. By the way. CCM is older than ZANU PF. Halafu uelewe CCM ni mlezi wa vyama vya ukombozi SADC.
Issue ya Zimbabwe itakuwa solved soon.

Wewe endelea kuwa na matumaini mfu. Watanzania wanawapuuza na utapeli wenu.
Afu hiyo neno 98% labda huko nyumban kwenu usitake kumsemea kila mtu
 
Lengo lako ni kudhalilisha viongozi. Nyie vijana ambao hamjagusa hata JKT mnasumbua sana. Issue za Zimbabwe ni za wanazimbwabwe. Kuwashwa washwa kutakuondolea uwezo wa kufikiri.
Hivi umeisikikiza hotuba ya jana ya Mugabe? Je umeielewa. Usidhani ZANU-PF ni kama CHADEMA. Wanautaratibu wao na katiba yao.

Ni vizuri ungeleta katiba yao useme inasemaje. Maamuzi ya vyama hayaamuliwi kihuni kihuni kama akina Mbowe kubadili gia angani. Chama imara kinafanya maamuzi kwa kufanya mikutano halali.

Wewe ungesubiri mkutano wao wa ZANU-PF ndio uje na malalamiko yako humu kuhusu nchi za watu.
Mtu aliyekosa ajenda anarukia rukia kila jambo linalotokea. Ni ushamba, jipangeni mjenge chama kiwe imara. Issue za kudhalilisha viongozi hazisaidii zimepitwa na wakati. Sasa hivi mnapuuzwa tu mnaonekana kama mazezeta.
Kupita JKT isiwe kigezo cha kuficha ujinga. Asiyejiheshimu hawezi kuheshimiwa pia.

Ni mpumbavu tu anayeweza kujiaminisha kuwa " maguvu,ukatili na vitisho" ni kinga dhidi ya hasira za umma ukiamua. Kama asivyotii sheria na Katiba ndivyo umma ukiamua hawataangalia cha sheria,katiba au kanuni.
 
Nimekuuliza umesikiliza hotu ya Rais wa Zimbabwe jana?
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia. Miaka miwili tu tumefanya uchaguzi. Na Rais wetu mpendwa anayependwa na watanzania 98% isipokuwa nyie tu wezi.

Kwenye uchaguzi mliangukia pua. Sasa mnaweweseka tu. Mlipewa matumaini makubwa mno. By the way. CCM is older than ZANU PF. Halafu uelewe CCM ni mlezi wa vyama vya ukombozi SADC.
Issue ya Zimbabwe itakuwa solved soon.

Wewe endelea kuwa na matumaini mfu. Watanzania wanawapuuza na utapeli wenu.
Kijiji/Mtaa wenu mmepata milioni 50?
 
Afu hiyo neno 98% labda huko nyumban kwenu usitake kumsemea kila mtu
Ati anataka kutuaminisha kuwa Magu ana uwezo wa kushinda kwa 98 percent!

Kama ni kwa "goli la mkono" hilo linawezekana
 
Umeongea kitu cha msingi sana

Lakini hicho kiburi na ulevi wa madataka vinatokana na Katiba ya nchi yetu.....

Ambayo inatamka wazi kuwa Rais ana "immunity" ya kutoshtakiwa awapo madarakani na hata pale atakapoondoka madarakani!

Hata kama atakuwa amesababisha "mauaji" ya halaiki!
Hakuna mwenye hati miliki ya cc wanaadamu isipokuwa Mungu peke yake.vingozi wengi waafrica hujiona kuwa wao ni miungu.Mgabe aende tuu hakuna lenye mwanzo lisilo kuwa na mwsho.zama zake zmeptwa nama dikteta wote walo baki wajiandae kisaikolojia maana hakuna jiwe litalo salia juu ya jiwe jingine ambalo halita bomolewa asilani.
 
Ati anataka kutuaminisha kuwa Magu ana uwezo wa kushinda kwa 98 percent!

Kama ni kwa "goli la mkono" hilo linawezekana
Ujue kuna mambo mengine watu wanaandika mashudu huku wanataka wengine tulipuke tuanze kupewa case za uchochezi
 
Watatfunga wangapi bat ukweli utabaki.
That is very true.

Kama kila ukiikosoa serikali ya awamu ya 5 utaitwa mchochezi, basi hawana budi kuongeza magereza yao, kwa kuwa wengi watatupeleka huko!
 
Nilimpenda Mugabe, hasa pale alipotwaa mashamba kutoka kwa wazungu waliyoijilimbikizia na kuwapa watu wasiokuwa nayo. Nilitamani baada ya hapo astaafu. Maadam hakufanya hivyo, he ceased being my hero. An independence hero has finished his political carrier as political cabbage!
 
Back
Top Bottom