Tunajifunza nini kwa yaliyomtokea Mugabe?

Tunajifunza nini kwa yaliyomtokea Mugabe?

Je Katiba hiyo aliyoapa kuilinda ndiyo inayompa mamlaka ya kumtimua Makamu wake na nafasi hiyo "kumwandalia" mkewe Grace ambaye hana sifa za kuwa Makamu wa Rais??
Hii "kumwandalia" ni dhana! ni hisia tu!
Kama kumfurusha vice president haipo kwenye mamlaka ya president ingeombwa tafsiri ya katiba mahakama kuu ya zimbabwe.

Huwezi na hutakiwi kujichukulia sheria mkononi!

Waoga wa hoja duniani wote hutumia mibunduki!
Mifano ipo mingi sana.
 
Annael,
-JKT
-Zimbabwe
-Wanazimbwabwe
-Mugabe
-ZANU-PF
-CHADEMA
-Mbowe
-Chama imara

Najaribu kutafuta hoja ambayo inaweza kusimama kama kichwa cha habari ya uchambuzi wako naomba msaada tafadhali.
 
Kuna mijitu itatetea basi sababu upande wao kuna tabia kama za huyu bwana
 
Mkuu hebu nisaidie kitu kimoja, hivi na Mugabe kumtimua Makamu wake wa Rais na nafasi hiyo kumwandalia mkewe nayo alishauriwa na watu wa Magharibi??
Ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuelewa nini hasa kinachoendelea Zimbabwe . Ungekuwa na uwezo wa kuunganisha dots za matukio nadhani ungepata jawabu. Suala happy si kumuandalia mkewe kuwa Raisi Bali Kuna architech nyuma ya pazia . Wazungu watatumaliza
 
Mugabe amemnyanyasa sana ndugu Munagangwa ambaye ndiye alikuwa mstari wa mbele kupigania nchi yake na kuhakikisha Mugabe anaingia madarakani. Lakini kufumba na kufumbua amemfukuza na kumfuta kazi. Nayakumbuka yaliyompata Nape Nnauye aliyekipigania chama chake cha CCM na kuhakikisha mzee anapata kiti hata kwa bao la mkono. Lakini naye kufumba na kufumbua amefukuzwa kazi kama mbwa. Ipo siku wapenzi wa nchi na wenye moyo wa utu watampigania Nape dhidi ya huyu jamaa.
 
Hebu angalia kituko cha mtu huyu:

Oktoba 2015: Mimi........ naapa kwamba nitailinda katiba ya nchi yangu kwa nguvu zote na nitaiongoza nchi hii kwa misingi ya katiba:

November 2015-November 2017: Katiba kitu gani? Katiba siyo kipaumbele changu.

Swali: Unaweza kumwelezaje mtu huyu katika ulimwengu wa utawala wa katiba, sheria, utawala bora, na demokrasia?
 
Lengo lako ni kudhalilisha viongozi. Nyie vijana ambao hamjagusa hata JKT mnasumbua sana. Issue za Zimbabwe ni za wanazimbwabwe. Kuwashwa washwa kutakuondolea uwezo wa kufikiri.
Hivi umeisikikiza hotuba ya jana ya Mugabe? Je umeielewa. Usidhani ZANU-PF ni kama CHADEMA. Wanautaratibu wao na katiba yao.

Ni vizuri ungeleta katiba yao useme inasemaje. Maamuzi ya vyama hayaamuliwi kihuni kihuni kama akina Mbowe kubadili gia angani. Chama imara kinafanya maamuzi kwa kufanya mikutano halali.

Wewe ungesubiri mkutano wao wa ZANU-PF ndio uje na malalamiko yako humu kuhusu nchi za watu.
Mtu aliyekosa ajenda anarukia rukia kila jambo linalotokea. Ni ushamba, jipangeni mjenge chama kiwe imara. Issue za kudhalilisha viongozi hazisaidii zimepitwa na wakati. Sasa hivi mnapuuzwa tu mnaonekana kama mazezeta.
Mpumbavu utamjua tu! Povu mingi.
 
Hakuna marefu yasiyona ncha,hakuna mkate mgumu mbele ya chai,wakuu wa majeshi waende Zimbabwe wakafundishwe kuzisimamia nchi zao

CDA yule ni zaidi ya mzalendo,Mungu atakua amemuandalia makao mema siku za mbeleni
Kabisa
 
Tunachojifunza kutokana na kuvuliwa uenyekiti wa ZANU PF wa Robert Mugabe ni ulevi wa madaraka na ubabe wa kufanya maamuzi akiamini kuwa kwa Katiba waliyonayo nchini Zimbabwe, hakuna mwenye ubavu wa kumng'oa!

Mugabe amejiona anaweza "kumtumbua" yeyote kwenye serikali yake na kuweza "kumreplace" na yeyote kwenye serikali yake hata kama anayempa nafasi hiyo hana sifa!

Ndicho kilichomtokea Mugabe baada ya kupokea ushauri wa mkewe Grace, kuwa nafasi ya Makamu Mwenyeki wa Chama anaitaka yeye ingawa hana sifa za kuwa Makamu Mwenyekiti, yeye Mugabe akalitekeleza ombi la Mkewe na "akamtumbua" Makamu Mwenyekiti wake Munagangwa na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona!

Wale wale waliokuwa wa kwanza kumshangilia Mugabe kwa kila aina ya "upuuzi" anaofanya, ndiyo hao hao waliompigia kura kwa wingi za kumvua uenyekiti wake!

Vivyo hivyo ndiyo yanayotokea nchini, kwa wale wale wanaoshangilia utumbuaji wa watendaji kila kukicha, wengine hata kwa kushindwa tu kujibu maswali ya Bwana Mkubwa katika ziara zake mikoani, ndiyo hao hao wanaoweza kumgeuka, mambo yakienda mrama!

Ni vyema Bwana Mkubwa wetu "asilewe" madaraka na atende kwa haki katika maamuzi yake na afuate Katiba aliyoapa kuilinda siku anaingia madarakani, hiyo ndiyo njia pekee ya kuepuka "aibu" ya kuvuliwa uenyekiti wa Chama, kulikomtokea Mugabe!

Kwa kuwa zipo "similarities" nyingi tu kati ya Mugabe na huyu Bwana Mkubwa wetu, ni suala la muda tu ndiyo utakaoamua......

Mungu ibariki Tanzania
mugabe matako tu..
 
Ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuelewa nini hasa kinachoendelea Zimbabwe . Ungekuwa na uwezo wa kuunganisha dots za matukio nadhani ungepata jawabu. Suala happy si kumuandalia mkewe kuwa Raisi Bali Kuna architech nyuma ya pazia . Wazungu watatumaliza
Kwani wazungu ndiyo waliomwambia Mugabe amtimue kazi Munangangwa na nafasi hiyo kumpa mkewe Grace??

Adam aliponzwa na Eva pale kwenye bustani ya Eden.......

Samson naye akaponzwa na Delila pale aipomfichulia siri za nguvu zake.....

Naye Kanumba wa kwetu kaponzwa na kabinti Lulu hadi akapoteza uhai wake!

Nyinyi wanawake fanyeni mambo yenu lakini Mungu anawaona!
 
Lengo lako ni kudhalilisha viongozi. Nyie vijana ambao hamjagusa hata JKT mnasumbua sana. Issue za Zimbabwe ni za wanazimbwabwe. Kuwashwa washwa kutakuondolea uwezo wa kufikiri.
Hivi umeisikikiza hotuba ya jana ya Mugabe? Je umeielewa. Usidhani ZANU-PF ni kama CHADEMA. Wanautaratibu wao na katiba yao.

Ni vizuri ungeleta katiba yao useme inasemaje. Maamuzi ya vyama hayaamuliwi kihuni kihuni kama akina Mbowe kubadili gia angani. Chama imara kinafanya maamuzi kwa kufanya mikutano halali.

Wewe ungesubiri mkutano wao wa ZANU-PF ndio uje na malalamiko yako humu kuhusu nchi za watu.
Mtu aliyekosa ajenda anarukia rukia kila jambo linalotokea. Ni ushamba, jipangeni mjenge chama kiwe imara. Issue za kudhalilisha viongozi hazisaidii zimepitwa na wakati. Sasa hivi mnapuuzwa tu mnaonekana kama mazezeta.
Kila mtu ana uhuru wa kuongea kile anachoona kinafaa. Kasoro kubwa kwa vyama tawala barani Afrika ni kuogopa kukosolewa. Huu ni woga wa wazi ambao sidhani kama unasaidia. Hakuna mwenye hati miliki ya nchi, ila kuna wenye hati miliki ya chama, nchi ni kwa ajili ya wanachi hivyo ukikosolewa tuliaaa kama uko kwa kinyozi wa ma.....
 
Tunajifunza nini kwa yaliyomtokea Mugabe?

NIKIZINGATIA HOTUBA NDEFU ALIYOITOA MUGABE, YA KUJARIBU KIJILINDA ASISTAAFISHWE, NA AMBAYO NI PUMBA TUPU, KWELI NIMEAMINI KWAMBA WAAFRIKA KWA ASILIMIA KUBWA SANA BADO TUNAONGOZWA NA MAKAPI YALIYOJIPENYEZA MADARAKANI KWA MABAVUMABAVU TU!
 
Ni vigumu sana kuwaongoza Slaves ambao waliisha zoea mijeledi na mateso toka kwa Slave masters. Waliounda Hilo zengwe lote huko Zimbabwe Ni wazungu waliotimuliwa kutoka kwenye mashamba makubwa wanayoyamiliki na kupewa wazawa. Sikushangaa issue ya Zimbabwe ilichukua almost dakika Kumi katika vyombo vya habari vya magharibi sababu wait ndo wahusika hasa wa hayo mapinduzi. Waafrika kwa ujinga wetu tutaendelea kuteseka kila kukicha kwa vikundi vinavyojiita kuwa Ni vya waleta mabadiliko . It's very sad . Mchango wa Mugabe wataukumbuka . A slave will always be slave
Wewe ni mzimbambwe au umeamua kuwasemea!

Ova
 
Hao wanajeshi wa Zimbabwe na wengine kwenye nchi zetu hizi hususani Uganda, Tanzania, DR congo, Rwanda na Burundi waache tabia ya kushinikiza viongozi ambao si machaguo ya wananchi.

Wanashirikishwa kwenye wizi wa kura na mpaka mwisho tunakuwa na viongozi ambao si machaguo wala mapenzi ya walio wengi kwa mabavu ya haohao wanajeshi (maana hata polisi ni jeshi). Tumekuwa tukiona ndege za kivita zikipiga mikwara sana nyakati za uchaguzi au pale wananchi wanapokuwa na hoja na wanataka kuifikisha kwa njia ya maandamano.

Naomba nchi tajwa hapo juu za ukanda wetu wajifunze kwa Zimbombo kwamba kile wananchi wasichokipenda mkakilazimisha kinakuwa na athari kijamii. Sasa wamemwondoa mtu waliyemweka na kumnyima Tsvagirai urais kwa miaka mingi sawa na Besigye anavyonyimwa urais, kesho mnataka kupindua...acheni kile mlichokilazimisha kifanye kazi, mwacheni mzee wa zimbombo atawale jamani mlimweka wenyewe
 
Mawazo yako hayakubaliki.Mhe.Ana miaka 37 madarakani ? Kibaya kipi alichokifanya
 
Ni vigumu sana kuwaongoza Slaves ambao waliisha zoea mijeledi na mateso toka kwa Slave masters. Waliounda Hilo zengwe lote huko Zimbabwe Ni wazungu waliotimuliwa kutoka kwenye mashamba makubwa wanayoyamiliki na kupewa wazawa. Sikushangaa issue ya Zimbabwe ilichukua almost dakika Kumi katika vyombo vya habari vya magharibi sababu wait ndo wahusika hasa wa hayo mapinduzi. Waafrika kwa ujinga wetu tutaendelea kuteseka kila kukicha kwa vikundi vinavyojiita kuwa Ni vya waleta mabadiliko . It's very sad . Mchango wa Mugabe wataukumbuka . A slave will always be slave
sio vizuri kuwasingizia wazungu kwa kila tatizo hapa Africa. Zimbabwe kuna mkwamo mkubwa wa kiuchumi, ajira hakuna, fedha hakuna na watu wanapanga foleni bank siku nzima ili kupata cash ambayo haizidi dola 30 kwa siku. Mugabe alitaka kumpa nchi mkewe kwa kuwatimua wale wote waliokua wanapinga mpango huo halafu unaleta hoja ya kitoto kwamba wazungu wanahusika kweli! !!!.
 
Ni vigumu sana kuwaongoza Slaves ambao waliisha zoea mijeledi na mateso toka kwa Slave masters. Waliounda Hilo zengwe lote huko Zimbabwe Ni wazungu waliotimuliwa kutoka kwenye mashamba makubwa wanayoyamiliki na kupewa wazawa. Sikushangaa issue ya Zimbabwe ilichukua almost dakika Kumi katika vyombo vya habari vya magharibi sababu wait ndo wahusika hasa wa hayo mapinduzi. Waafrika kwa ujinga wetu tutaendelea kuteseka kila kukicha kwa vikundi vinavyojiita kuwa Ni vya waleta mabadiliko . It's very sad . Mchango wa Mugabe wataukumbuka . A slave will always be slave

HIVI NYIE LUMUMBA MNAKUNYWA MACHICHA GANI ASUBUHI HIV MUGABE KUWAONGOZA WATU ZAIDI YA MIAKA 50 SIO UTUMWA HUO MTU DAKIKA 5 AKIKAA KESHASINZIA HANA UWEZO TENA WA KUONGOZA ANAAMUA KUMPA DEMU WAKE NCHI AONGOZE MNAANZA KUSINGIZIA WAZUNGU WATU WALISHA MCHOKA KAMA TULIVYO WACHOKA NYIE CCM NDO MAANA MNAOGOPA HII KITU ISAMBAE AFRICA NZIMA HEMBU KESHO AMKA ASUBUHI NENDA KWENYE MEZA ZA MAGAZETI MUWASIKILIZE WANANCHI WANVYO WAPONDA WATANZANIA WA SASA WANAULEWA WA MAMBO SIO KAMA ZAMANI
 
Hebu angalia kituko cha mtu huyu:

Oktoba 2015: Mimi........ naapa kwamba nitailinda katiba ya nchi yangu kwa nguvu zote na nitaiongoza nchi hii kwa misingi ya katiba:

November 2015-November 2017: Katiba kitu gani? Katiba siyo kipaumbele changu.

Swali: Unaweza kumwelezaje mtu huyu katika ulimwengu wa utawala wa katiba, sheria, utawala bora, na demokrasia?
Umeongea kitu cha msingi sana

Lakini hicho kiburi na ulevi wa madataka vinatokana na Katiba ya nchi yetu.....

Ambayo inatamka wazi kuwa Rais ana "immunity" ya kutoshtakiwa awapo madarakani na hata pale atakapoondoka madarakani!

Hata kama atakuwa amesababisha "mauaji" ya halaiki!
 
Back
Top Bottom