Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Uchaguzi Mkuu umefanyika nchini Afrika Kusini wiki iliyopita, ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa nchi hiyo Indapendent Electoral Commission, kilikitangaza Chama cha ANC cha aliyekuwa mzalendo namba moja wa nchi hiyo, Mzee Nelson Mandela, kuwa mshindi kwa kupata asilimia 57.5 kikifuatiwa na chama cha Democratic Alliance (DA) ambacho kimepata asimilia 20.7 na cha kilichofuatia ni chama cha cha mlengo wa kushoto cha Malema, cha Economic Freedom Fighters (EFF) kilichopata aslimimia 10.8
Vyama vingine vidogo vidogo vikajikusanyia asimia iliyobakia
Tunajifunza nini kutokana na uchaguzi uliomalimizika na kutangazwa huko Afrika Kusini??
Kitu kimoja tunachojifunza kutokana na uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Tume huru ya uchaguzi ( Independent Electoral Commission) ni kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki na Jeshi la Polisi la nchi hiyo lilikuwa na jukumu dogo kabisa la kusimamia usalama na wala siyo kuingilia upigaji kura na ndicho tulichokiona cha wapiga kura kupiga kura zao na matokeo yao kutangazwa kama yalivyo na wala hayakuchakachuliwa
Kwa hiyo kama nchi yetu itapenda kuendelea kudumisha amani ya nchi hii ambayo imekuwa nayo tokea nchi yetu ipate Uhuru wake ni lazima iheshimu sanduku la kura na wala siyo "kutusimikia" viongozi wao wanaowataka wao ambao hawakuchaguliwa na wananchi
Ni vyema tukaiga mfano wa Independent Electoral Commission ya Afrika Kusini katika uandaaji wa chaguzi zetu
Mungu ibariki Tanzania