Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,159
Hivi Leo zimetolewa taarifa za kufutwa kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Uganda, Jenerali Kayihura na Waziri wa Usalama Henry Tumukunde, ambako kumefanywa na Rais Museveni.
Sababu za kufutwa kwao kazi ni kukithiri kwa matukio ya mauaji ya raia wasio na hatia, kutekwa na kuteswa kwa watu.
Sababu zilizotolewa huko Uganda kwa kufutwa kazi kwa watu hao wawili ndiyo kilio cha muda mrefu hapa nchini kuwa IGP Simon Sirro na Waziri wake wa ndani Mwiguru Nchemba, wajiuzulu nafasi zao au Rais atengue nafasi hizo kutokana na matukio ya watu "wasiojulikana" kuua watu hapa nchini bila watu hao kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Rais wa Uganda ameamua kuwafuta kazi watu hao ambao walikuwa wanaharibu sifa ya utendaji kazi wa Jeshi hilo nchini Uganda.
Ni wakati muafaka kwa sasa Rais wetu naye afuate nyayo za Rais mwenzake wa nchi jirani kwa kuwafuta kazi IGP Simon Sirro na Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba