Tunaisambaratisha Tanzania!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaisambaratisha Tanzania!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Mar 16, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tangu wakati Mwalimu akiwepo kwenye madaraka au nje ya madaraka kulikuwa na changamoto kama taifa, na wale wanaotaka tuamini kwamba enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna changamoto ni watu ambao hawataki kuukubali UKWELI. Lakini tofauti na viongozi wengine waliomfuata Mwalimu kwenye Urais, yeye alikuwa anazielezea changamoto zilizopo, anazichambua,anatafuta njia za kukabiliana nazo,anakabiliana nazo,anafanya tathimini kisha anatoa mwelekeo.

  Enzi za Mwalimu kulikuwa na maandiko mengi sana yaliyoandikwa na yeye mwenyewe au yaliyotokana na maamuzi ya vikao kwa kufuata falsafa yake. Mwalimu aliandika vitabu, makala, vijarida na alitoa hotuba mbalimbali kuelezea mambo muhimu yahusuyo taifa. Kama mtu atachukua hatua ya kuyasoma au kusikiliza hotuba za mwalimu, basi bila shaka atagundua kwamba Mwalimu alijenga utaifa na kuusimamia utu wa watu wake.

  Lakini tangu kuja kwa mfumo wa vyama vingi kumekuwa na kiwewe cha kushika madaraka na kuyang'ang'ania na kupoteza kabisa watu wanaojali nchi yetu inakwenda wapi. Kiuhalisia jamii nzima imetopea kwenye kiu kubwa sana ya "kupata" bila ya kujali huko kupata kunapatikanaje.

  Sasa hivi hapa nchini kwetu kuna udini wa kutisha sana na kwa bahati mbaya Rais wetu Jakaya Kikwete aliishia kusema tu "...kampeni za uchaguzi mkuu zilitawaliwa na udini" bila ya kwenda kwa kina sana udini huo ulifanywa na nani dhidi ya nani. Matokeo yake kila mwananchi akatoka na Tafsiri yake.

  Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba sasa hivi ni waislamu "moderate" peke yao ambao wanaweza kusimama hadharani na kusema wao ni CHADEMA damu damu. Na wakristo wengi hivi sasa hata waliomo ndani ya CCM wanaamini "waislamu" wana ajenda ya siri ya kuislimisha nchi na wanaitumia CCM kama chombo cha kufanikisha azima yao hiyo. Hali ya kutokuaminiana kati ya dini hizi mbili ni mbaya kiasi kwamba hata ukiona viongozi wa dini hizi wanachekeana hadharani unatia shaka kutokana ya yale yanayotokea na kupangwa sirini!!

  Tanzania (siyo Tanganyika wala Zanzibar) ilijengwa wakati wa vuguvugu la umajumui wa kiafrika (Panafrikanisim). Tanzania hiyo ilikuwa Tanzania ya watu wote kwa maendeleo ya watu wote na kila mtanzania aliwaamini viongozi wake na wao waliamini katika dhana ya "serikali ni wananchi" na 'cheo ni dhamana" Kila jambo lilikuwa letu sote ingawa tofauti ilikuwepo.

  Tanzania ya leo kama mwaka 1995 Mwalimu aliiona ina "nyufa" basi bila shaka hii ya sasa baadhi ya kuta zake zimeshaanguka na kila apitaye nje anaona kilichomo ndani. Hakuna tena anayeutaka Muungano (wapo wanaojidai kuutaka) na wala hakuna tena anayejali kama ukivunjika kitatokea nini.

  Tanzania ya leo watu wanaamua kuwa wanachama (siyo wafuasi) wa chama fulani si kwa sababu za kupenda sera,Itikadi au falsafa ya chama husika, bali kwa sababu chama hicho kinamhakikishia uwezo wa kushinda uchaguzi ili apate "ulaji' au njia za kujinufaisha yeye mwenyewe.

  Watu hawasomi tena kwa ajili ya kuongeza maarifa ili wakaitumikie jamii inayowahusu, bali siku hizi kusoma ni zana mojawapo inayomsaidia mtu kuongeza nafasi ya kupandishwa cheo au kuongezwa mshahara. Hali hiyo imesababisha watu kuvurugana na kukanyagana kwenye kughushi vyeti au hata kuhonga ili "wafaulu' mitihani kwa kiwango cha juu sana (GPA?) kwa lengo la kuonekana "wasomi" bila ya kujali kama wana elimu stahiki kwenye fani husika.

  Maadili kwenye jamii yetu yameshapuuzwa siku nyingi sana. Mtu kuanzisha NGO ya kulelea watoto Yatima kwa lengo la kupata fedha za kuanzishia miradi yake binafsi si kosa la jinai tena. Ni sehemu ndogo sana (kama bado ipo) ambayo haijihusishi na ufisadi huu wa kimaadili. Wazazi, watoto na wanajamii wote tunaufurahia mmomonyoko huu wa maadili kwa sababu tu unatufaidisha kwa namna moja ama nyingine.

  Mtazamo wangu kama jamii ya Tanzania tukiendelea namna hii basi bila shaka huko tuendako siku si nyingi taifa letu LITASAMBARATIKA!!
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  it is TURUUUUUUUUU! - (Mama Shija, Organic chemistry Guru - Tambaza sec (up to 1993))
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Usingeweka aya hiyo yenye maandishi mekundu ungekuwa mfano wa kuigwa wa warushaji wa THREADS zenye mantiki na zinazojadilika. Maandishi mekundu yamedhihirisha kweli kuna udini na wewe ni mdini namba moja Kwa nini CCM na Uislamu? Kwa tafsirim hiyo una maana CHADEMA na UKRISTO?. Thread imekosa ladha tena, acha nijiondokee. Jamani tujadili masuala yahusuyo kuitenga Tanzania imara na siyo majungu haya.
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  MMH umeongea kweli ni jukumu lako langu na yule kuirudisha nchi kwenye umoja wa kitaifa
   
 5. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Nchi ishasambaratishwa mda mrefu. Kilichobaki ni kuchapana makonde tu hadi kieleweke.
   
 6. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndiyo tatizo letu watanzania kujigeuza mbuni kutumbukiza kichwa shimoni wakati mwili woote uko nje. Mimi nina mahusianon na wakristo na waislamu ambao pia ni wanasiasa.

  Ukienda kwenye mizingo ya ndani kabisa ya siasa za CCM kuna manung'uniko makubwa sana kutoka kwa wakristo kwamba nafasi nyingi za uteuzi wanapewa waislamu hata kama hawana "sifa". Wakati huo huo kuna shutuma kwamba Zitto alipigwa vita asiwe Mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu yeye ni 'muislamu".

  Humu Jamvini kuna watu wanaitetea CCM si kwa sababu ya hoja au wanaipinga CDM si kwa sababu ya udhaifu wake na vile vile kwa CHADEMA dhidi ya CCM.
   
 7. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Well said Kigarama! Kwanza sipendi kitu kinachoitwa udini na wafia dini.
  Yaani nikiwaza tu kuwa hizi dini tumeletewa, basi mara moja huwa nase
  ma sitapoteza mda wangu kwa kubishana na mtu fulani kisa dini. Yaani
  ni BIG NOOO!!.
  Back to the topic....nchi yetu imekosa ombwe la uongozi na sasa inajie
  ndesha yenyewe. Baadhi ya viongozi wetu "hasa walio wengi" hawapo kwa
  masirahi ya nchi wala wananchi, wapo kwa manufaa yao na familia zao.
  Ila natabiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 baada ya wiki 3 au 4
  hii nchi itaingia kwenye machafuko ambayo hayajawahi kutokea! yaani
  tutashuhudia uchadema na uccm, ukristo na uislaam. Yangu macho.
   
 8. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,540
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  By way of deception.
   
 9. Godfrey Electronics

  Godfrey Electronics JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 587
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nimepita wakuu, ntarudi baadae kuja kuisoma tena na kufanya maamuzi
   
 10. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,379
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Tanzania kama taifa haliko viable tena hili taifa ni total failure cha msingi tuvunje muungano halafu wale wanaolalamika sana na walalamikiwa wagawane Tanganyika kwa makubalianao rasmi.

  Sioni tena future ya nchi inayoitwa Tanzania! Ni ujinga, kujidanganya na kupoteza muda kujenga taifa la watu wasio aminiana!
   
 11. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo linajulikana na ni merehemu KIFIMBO ndio chanzo cha yote, ukiangalia harakati za kupigania uhuru au kama umebahatika kuangalia hata zile picha za uhuru utaona kuna mchanganyiko mkubwa sana na kuna vikofia vya kutosha mno, tatizo lilikuja baada ya uhuru kwa kutokugawa rasilimali za taifa kwa uadilifu.
  Hakuna solution hapa hadi pale mali za nchi hii zitakapogawanywa sawa kwa wote, waislam wa sasa sio wale wa zamani wa kumkaribisha nyerere misikitini na kumfungisha, waislam wa sasa hawapo tayari tena kurudia ujinga wa wazee wao waliomuamini nyerere kupita kiasi.
  Mara nyingi huwa nasema na kurudia CDM haina sera za kikisto, ila naamini kabisa sera hizo za kikanisa zipo kwenye agenda za baadhi ya viongozi wake.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu umeandika yote lakini ulipofika hapo ndipo umechemsha vibaya sana. Kwanza hakuna kitu - Muislaam moderate hii habari umeipata wapi?..

  Na kwa nini watu mnapenda sana kuutafsiri Uislaam wakati nyie sio Waislaam? na wala hamjui lolote kuhusu Uislaam!. Kuwepo kwa Waislaam CHADEMA ni kwa sababu hatupendi UDINI japokuwa upo na tunatazama Chadema kama chama cha siasa na sio jumuiko la watu, Chadema kama mbadala na sio kuwepo kwa Dr.Slaa au Mbowe na dini au kabila lake. Hivyo tayari wewe mwenyewe inakuweka ktk UDINI unapojaribu kujenga hoja kwa kutumia dini za watu na hata kuwa label waislaam kama moderate. Hili ni tusi kubwa kwangu mimi na waislaam kwa ujumla wetu.

  Marekani pia wanapenda sana kutumia neno hilo, lakini ukweli utabakia kwamba wale waislaam wanaopingana na Marekani ni kwa sababu Marekani inafanya Ugaidi (terrorist) nchini mwao kuwaibia mafuta na rasilimali zao kwa kuwaweka vibaraka wao. Sasa kwutokana na kwamba nchin hizo asilimia 99 ni waislaam basi mpiganaji yeyote ataitwa Muislaam mwenye siasa kali na sio Mu -Afghanstan, Iran au Iraq. Ukweli utabakia kwamba hao wangekuwa Wakristu wangelifanya hivyo hivyo maadam ni Marekani iliyowaingilia tawala za nchi zao lakini hakuna kosa kabisa wao kujitambulisha kama wakikristu - na hata wanajeshi wao husali kikristu kabla ya kwenda vitani nchi za watu lakini wao hawapewi jina wala kuitwa wakristu isipokuwa ni majeshi ya Marekani au NATO wapenda amani na usawa. Msitake kabisa kuchanganya Uzalendo wa wananchi kwa nchi zao sababu tu ni Waislaam..

  Tanzania Udini upo na unatokana na kwamba Wakristu wanajiona wao wabora zaidi ya Waislaam na pale waislaam wanapopinga mfumo uliopo mnawaona wao ndio wadini japokuwa ukweli hamtaki kuutazama. Ni rahisi kwenu kujivuna kwamba mmesoma sijui mnawekeza ktk jamii zenu na kuona maswala mengine ya kutofanikiwa ni ya Waislaam halafu mnasema hakuna Udini...Na kama Chadema wanafikiria hakuna tatizo ama waislaam ndio wakorofi basi mnatuweka hata sisi tunaofikiria tunaweza kuyapata mageuzi kupitia Chadema kutokuwa na imani na chama hicho...
   
 13. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Mkandara tatizo ni wewe kwa sababu hata hapo nimeandika kuna baadhi ya "wakristo" ndani ya CCM wanahisi kwamba hawatendewi haki kwenye uteuzi wa nafasi mbalimbali. Mkandara mimi na wewe tumo kwenye tatizo ninaloliongela na ndiyo maana kwenye bandiko zima unadai nimechemsha kwenye kusema kuna waislam "moderate". kwani kule shuleni tulifundishwa kwamba mtu akiweka alama hii ya funga na fungua usemi anamaanisha nini? Maana yake icho alichoandika hakiko hivyo kilivyoandikwa au hakuna hakika ya hicho kilichoandikwa.

  Huwezi kuniambia kwamba kina Basalahe na wenzake na Redio Imaan ya Morogoro msimamo wao dhidi ya CHADEMA umejengwa kwenye misingi ya tofauti ya sera za CHADEMA kisiasa. Halafu hata mimi najua kuna wachungaji na vingozi wengine wa kanisa wanaiunga mkono CHADEMA si kwa sababu wamefurahishwa na sera zake bali ni kwa sababu ni chama "chao" kwenye muktadha wa siasa za Tanzania.

  Soma vizuri bandiko langu utagundua kwamba mimi ninachosimamia si huu "uislam' au "ukristo" unaosimama kwa misingi ya kisiasa. Mimi nawajua waislam na ninaheshimu sana waislam kwani ni ndugu zangu kama walivyo wakristo ambao pia ni ndugu zangu. Msiugeuze huu mjadala kuwa wa kidini.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu na wewe nisome vizuri. Nazungumzia kitu kinachonihusu mimi na Waislaam. Ulichoandika hapo juu ni mawazo yako ukisisitiza ni ukweli uliopo wazi ya kwamba waislaam moderate ndio wapo Chadema..I am not a moderate Muslim na hakuna kitu hicho. Ufunge na ufungue haipotezi maana kwamba haya ni maneno yako kwa fikra zako kama ulivyoandika hapo juu. Nimeingia Chadema kwa sababu naipiga vita CCM na mfumo wake wa kiutawala haijalishi ndani ya CCM au Chadema kuna watu gani ama ndio U moderate. Hao wanaofikiria Uislaam na Ukistu ndio wanapenda sana kutugawa ktk makundi haya na wapo wajinga wanaamini hivyo kuendeleza kutuita sisi moderate ni kutuwekea mzigo tusio ubeba..

  Na siwezi kuwatetea wakristu kwa sababu sijui wanajiunga na CCM au Chadema kwa ajili gani isipokuwa kile wanachokizungumza au kutetea. Naweza tu kuwakosoa kwa yale wanayoyaandika au kuyasema lakini siwezi kusema kwamba wakristu waliopo Chadema ni wale wanaopingana na Uislaam kwa sababu sijui fikra zao wala hisia zao ila wao wenyewe. Sote tunaheshimiana lakini sio la kubandikiana kwa nini tupo Chadema kwa sababu sio kweli hata kidogo.
   
 15. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  I prefer hii nchi iuzwe kila mtu apewe chake achape mwendo
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  Mkandara,

  ..mimi nadhani kila dini inajiona yenyewe na waumini wake ni bora kuliko dini nyingine.

  ..mafundisho ya kila dini ni kwamba ukweli na haki uko katika dini husika na siyo upande mwingine.
  u
  ..mimi nadhani matatizo yetu yashughulikiwe kwa kutumia vigezo vingine, tuachane na dini kabisa.

  ..kwanza tuache kuangaliana na kunyoosheana vidole kwamba huyu Muislamu, huyu Mkristo, huyu Mhindi, etc etc.


   
 17. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi mkandara unataka kuniambia kwamba ni rahisi kwa Muislam kusimama Mtambani au kwa Mtoro na kusema kwamba yeye ni mwana CHADEMA kindakindaki na wenzake wakamuelewa!! Hivi unataka kusema leo hii hujui kwamba kuna Wakristo lukuki wanaiunga mkono CHADEMA kwa sababu ni chama "chao?" Baada ya uchaguzi wa Uzini si tuliambiwa kwamba CHADEMA ilikuwa ya Pili kwa sababu eneo hilo lina wakristo wengi huko Zanzibar. Hii maana yake ilikuwa nini Mkandara? Mimi situngi hadithi bali naongea kile kilichopo hata kama kitu hicho sikiamini!!
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakuna muislaam anayeweza kusimama msikiti wa Mtoro na akasema yeye ni CCM wala CUF isipokuwa atazungumzia adha na machafu yanayofanya dhidi ya wananchi au dini yenyewe. Kwa hao mnaowaita waislaam wanaposimama majukwaani na lkulalamika ni muhimu zaidi kuwasilikiza na kuutazama ukweli na sio dini zetu kwa sababu lisemwalo lipo!..

  Tofauti baina yangu na wao ni kwamba wao wameamua kuyazungumzia matatizo kwa waislaam na mimi napambana na matatizo kivyangu. Kama ktk Siasa kuna watu wanaamini Uanaharakati yaani wanapambana na matatizo kwa kutafuta suluhu ya matatizo na wapo wengine wamefanya hivyo kupitia vyama vyao haina maana Dr.Slaa akizungumzia mabaya basi ni kwa sababu yeyeni Chadema.. Angeyasema hayo hata kama angekuwa CUF au NCCR isipokuwa kachagua jukwaa gani la kufikisha ujumbe wake au ktk mapambano. Maswala ya Zanzibar ndio maana nikasema Udini upo, na watu kama Jussa ni hatari kabisa kwa sababu he is attacking Ukristu na sio Chadema hivyo nategemea ndani ya Chadema hakuna watu wanaofikiria kama Jussa.

  Jokakuu,
  Mkuu wangu ni kweli kabisa kwamba kila dini inajiona wao ni wabora zaidi ya wengine lakini sii watu isipokuwa mafundisho yake. Kisiasa tunaweza kusema kila dini inaona itikadi zake ndizo bora zaidi ya nyinginezo. WATU wake hawawezi kujiona bora ikiwa wanadhalilishwa iwe Wakristu huko Nigeria au Waislaam nchi nyinginezo. Kinacholiliwa ni USAWA baina yao na yeyote yule anayejiona mbora zaidi ndiye mwenye nguvu na mkandamizaji kupitia kigezo cha dini yake..Huwezi kujiona mbora ikiwa unalalamika isipokuwa umepungukiwa kama binadamu anayethaminika..

  Ni lazima kuna pungufu la ubora huo unaojionyesha ukilinganisha na mwingine. Tatizo letu sote hatutaki kuona USAWA ktk UTU wetu isipokuwa tunajaribu kuficha madonda.. Tatizo lipo na haswa mfumo wa AFYA na ELIMU ambao nimekuja gundua where the problem lies.. lazima tuuzungumzie na kupata ufumbuzi maana Dini zimeingizwa ktk utawala na ndio chanzo na sababu ya lawama zote.
   
 19. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hapa akitokea rafiki yangu Topical na Sweke34 basi thread hii itasomeka CLOSED.
  Na akitokea Kiranga (mwanasayansi wa JF) basi thread hii itawakimbiza watu kwa hoja.
  Acha niwasubiri.
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kigarama,
  Unachokisema ni kweli tupu. Lakini mimi najikita zaidi katika kutafuta ufumbuzi. Umeelezea vizuri sana jinsi kuta zilizokwisha bomoka katika jumuiya yetu. Je, tumechelewa sana kwamba nyumba nzima itaporomoka, au kuna hatua tunaweza kuchukua kunusuru hili jengo na kulirudisha katika mwelekeo sahihi?
   
Loading...