Uchaguzi 2020 Tunaingia kwenye Uchaguzi Mkuu tukiwa tunakumbuka tambo hizi

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Wakati tunasubiri kipenga kuanza uchaguzi mkuu, tuliojsliwa kusoma alama za nyakati tunakumbuka Tambo hizi:

1. Sikuchaguliwa ili niongeze mishahara (Rais JPM)
2. Sikuleta tetemeko la ardhi na kwa Nini kila janga Ni lenu (JPM)
3. Nataka Bei ya sukari iteremke Hadi sh. 1800 (JPM )
4. Nataka Tanzania iwe Kama Dubai (JPM)
5. Nitawapiga mashangazi zenu viboko mkiniletea upuuzi (JPM)
6. Jeshi litabangua korosho hata kwa meno (JPM)
7. Nitashughulika na wahujumu uchumi hata awe mke wangu (JPM)
8. Nimekuteua, nakulipa mshahara, nimekupa gari ole wako jimboni kwako utamtangaze moinzani (JPM)
9. Nijenge shule halafu upate mimba, siwezi kusomesha wamama (JPM)
10. Mpinzani hawezi kukanyaga serikali yangu (JPM)
11. Million 50 kila Kijiji (JPM)
12. Hakuna mahala popote nilipozungumzia katiba wakati wa kampeni (JPM)
Tuchambue Ni wapi rahisi alifanya vibaya na wapi alifanya vizuri. Kwa Yale maxuri
1. Ununuzi wa ndege kwa cash
2. Ujenzi SGR bado unaendelea
3. Ujenzi uwanja ndege chato na upanuzi viwanja vingine vya ndege
4. Kukuza na kujaza wanyama hifadhi ya Burigi
5. Kuthibiti mapato ya nchi
6. Deni la taifa kuongezeka
7. Kupaisha taifa kuingia uchumi wa mwisho wa Kati
8. Kudhibiti na kuwaondoa wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona
9. Kutokupandisha mishahara ya watumishi lakini kuweka nidhamu kazini
10. Kutoa fedha on the sport kusaidia wenye uhitaji na kugharimia miradi iliyokwama
11. Slogan ya viwanda cherehani 4 tayari kiwanda. Hapa kazi tu
12. Kuwavutia wapinzania kuhamia CCM kuunga juhudi
13. Kutokusafiri nje ya nchi kuokoa fedha
14. Kuongoza kwa kutumbua na kufanya teuzi
15. Kuzunguka nchi nzima kuzindua na kufungua miradi mikubwa
16. Ujenzi wa mahakama kuu kila mkoa
17. Msimamo mkali juu ya siasa za nje
18. Kupita bila kupingwa kwenye chama chake kuwania kiti Cha urais.

Nadhani Tuanze Sasa mjadala
 
Mbona Umeme umeruka?
  • Umeme kushuka bei kwani vijijini kote kuna umeme Tarrif 0
  • umeme masaa 24 na JF kushinda kwenye Computer na simu bila kukatika
  • Umeme kuwashwa mabarabarani katika Miji karibia ya 80% Nchi nzima
Usafiri kuwa wa uhakika Nchi nzima Bukoba Dar, Arusha Lindi, Momba Rombo, Kazuramimba Kibiti.
Mafuta kutopanda bei, licha ya Corona kuishusha bei hadi 1,550 lkn hata Bodaboda wanajaza
kutokusimama kwa mabasi saa 4 usiku Mabasi yote yatembee vifua mbele 24hrs
Bodaboda kutawalazimisha kuvaa Helmet na wapakie wanavyoweza

Haya yote hayaonekani?
 
Nyumba yangu kibamba kuvunjwa bila ya malipo wala kupewa angalau kiwanja cha kuanzia maisha.
Vitu vyote nyumbani kusagwa sagwa na tinga tinga.
Itanichukua maisha yangu yote na watoto wangu na wajukuu zangu kuondoa kovu hili,hiku nikiwa najiegesha kwenye nyumba za wasamaria.
 
Kamatakamata/kuteka na kuwajeruhi hata kuwaua wapinzani wake wa kisiasa, wanaharakati na waandishi wa habari. Kuwapa kesi za UHUJUMU UCHUMI. Magufuli hafai

#LISSURAIS2020
 
"Nimekuteua, nakulipa mshahara, nimekupa gari ole wako jimboni kwako utamtangaze mpinzani (JPM)". Hili ndili kiboko yao kwa maana hawa walioteuliwa ndiyo wasimamizi wakuu wa uchaguzi. Uchaguzi mkuu ujao hautakuwa uchaguzi bali ni uchafuzi. Mimi sitapiga kura!
 
Yaani wewe Mkurugenzi nikulipe mimi mshahara harafu umtangaze mpinzani kashinda - hiiii
 
Nyumba yangu kibamba kuvunjwa bila ya malipo wala kupewa angalau kiwanja cha kuanzia maisha.
Vitu vyote nyumbani kusagwa sagwa na tinga tinga.
Itanichukua maisha yangu yote na watoto wangu na wajukuu zangu kuondoa kovu hili,hiku nikiwa najiegesha kwenye nyumba za wasamaria.
Dah inasikitisha, pole sana mkuu
 
Mbona Umeme umeruka?
  • Umeme kushuka bei kwani vijijini kote kuna umeme Tarrif 0
  • umeme masaa 24 na JF kushinda kwenye Computer na simu bila kukatika
  • Umeme kuwashwa mabarabarani katika Miji karibia ya 80% Nchi nzima
Usafiri kuwa wa uhakika Nchi nzima Bukoba Dar, Arusha Lindi, Momba Rombo, Kazuramimba Kibiti.
Mafuta kutopanda bei, licha ya Corona kuishusha bei hadi 1,550 lkn hata Bodaboda wanajaza
kutokusimama kwa mabasi saa 4 usiku Mabasi yote yatembee vifua mbele 24hrs
Bodaboda kutawalazimisha kuvaa Helmet na wapakie wanavyoweza

Haya yote hayaonekani?
Umetumwa??
 
Ongeza zaidi ila fahamu jamaa atapasua kwa kuvunja record,mtaachwa mbali sana
ushindi wake hautakuwa realistic kwa kuwa NEC ni mali yake, ivyo kauli yako ni sawa na kujisifia kuwa umeua wengi baada ya kupiga bomu mochuari, bweha mla kuku wewe
 
Kwenye mishahara na maslahi ya watumishi imekuwa changamoto. Wamepitia mengi sana ktk kipindi hiki ambayo ni vigumu sana kuyasahau, tangu kutumbuliwa, madaraja na wastaafu.
 
Umetumwa??
kichwa yako sio nzuri ipo km vile bichwa la CHADEMA?
wewe Mada yoyote hutaki ukweli unaleta siasa za kupinganapingana tu
huwezi kafanye mpambano wa Tundu Lissu, Mbowe, Msigwa na kuna mnyaturu mmoja katoa na basi kabisa la Kampeni, safari hii wapisheni ACT ndio tunaweza jibizana nao humu JF
1594642872126.png
 
Nyumba yangu kibamba kuvunjwa bila ya malipo wala kupewa angalau kiwanja cha kuanzia maisha.
Vitu vyote nyumbani kusagwa sagwa na tinga tinga.
Itanichukua maisha yangu yote na watoto wangu na wajukuu zangu kuondoa kovu hili,hiku nikiwa najiegesha kwenye nyumba za wasamaria.
Dah..kama hiki ulivhokiandika hp ni kweli pole sana ndugu na hongera kwa moyo huo mimi ningekufa na presha!
 
Hiyo Tambo #8 atawaponza wakurugenzi maana ndo tutakaoanza nao, otherwise wasifuate maelekezo haramu watende kwa mujibu wa sheria, ngoja kwanza rais atue tarehe 28
 
Back
Top Bottom