Rais Samia na vipaumbele vinavyolenga kuipaisha Tanzania kiuchumi

Nov 10, 2014
48
18
Na Comrade Christopher H.Bomola

Mwanafalsafa Rosalynn Carter alipata kusema "kiongozi ni mtu anayewaongoza watu na kuwafikisha wanapotaka kwenda,lakini kiongozi bora ni yule anayewaongoza watu na kuwafikisha sio lazima wanapotaka wao kwenda bali wanapotakiwa kufika".

kiongozi mwenye maono ni yule ambaye kwa uzoefu na uono mpana anajua watu wake wanapostahili kufika na anaweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwa gharama yeyote ile anawafikisha katika mwisho wa safari yao.

ndivyo unavyoweza kumwelezea Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia hotuba yake aliyoitoa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 22 April,2021,hotuba iliyoainisha vipaumbele na mikakati ya utekelezaji wa vipaumbele hivyo ili kuhakikisha Taifa la Tanzania na Umma wa Watanzania wanafika mahali ambapo tunatakiwa kufika katika suala zima la maendeleo.

Mheshimiwa Rais kupitia hotuba yake ameweka mkazo kuhusu ukamilishaji wa miradi mbalimbali ambayo iliasisiwa na mtangulizi wake Hayati Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa ushirikiano na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hotuba yake Mheshimiwa Rais amewahakikishia Watanzania kuwa serikali yake itakamilisha ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati ya bwawa la umeme wa maji la Mwalimu Nyerere (JNHPP) ambalo baada ya kukamilika kwake litakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya Megawati 2115 ambazo sio tu zitaifikisha nchi yetu katika hatua ya kuwa na umeme wa uhakika lakini Taifa letu litaweza kuuza umeme katika nchi jirani na kujiingizia fedha za kigeni.

kupitia hotuba hii Mheshimiwa Rais ameainisha sekta mbalimbali, vipaumbele vyake na miradi itakayotekelezwa katika sekta husika.

baadhi ya sekta na miradi iliyoguswa katika hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni;

1. Miundombinu
Pia Mheshimiwa Rais amehaidi kukamilisha ujenzi wa reli ya mwendokasi ya kutoka Dar es salaam mpaka Mwanza (standard gauge railway) ambayo inakwenda kuondoa changamoto ya usafiri wa abiria na kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kuelekea nchi jirani hasa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo, Burundi na Rwanda.

Ukamilishaji wa ujenzi wa madaraja yote yalioanza kujengwa katika uongozi wa awamu ya tano yakiwemo daraja la JPM (Kigongo-Busisi), daraja la Tanzanite na madaraja ya flyover ambao ujenzi wake unaendelea mkoani Dar es salaam, ujenzi wa barabara mbalimbali nchi nzima na ununuzi wa ndege mpya unaoenda sambamba na maboresho makubwa yanayolenga kulijengea uwezo shirika letu la ndege ili lifanye biashara kiushindani na kutengeneza faida.

2. Uwekezaji na Biashara
Mheshimiwa Rais ameeleza nia ya serikali yake kuhakikisha inajenga mazingira wezeshi yatakayoongeza kasi ya ukuaji wa uwekezaji na ongezeko la biashara litakaloongeza wigo mpana wa ajira kwa wananchi wake, mkazo mkubwa ukiwekwa kwenye kuondoa urasimu katika kufanya uwekezaji, urasimu katika upatikanaji wa vibali vya ukaazi,kazi na biashara, na kuondoa tabia za kukusanya kodi kwa kutumia nguvu ili kujenga mazingira yanayotabirika ya uwekezaji na biashara.

Pia Rais Samia amedhamiria kufanya maboresho makubwa katika sekta ya uchumi na fedha,mabadiliko yatakayoleta matokeo chanya katika uwekezaji,viwanda na biashara hii inaonesha dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais Mama Samia katika kuipaisha nchi kimaendeleo.

3. Diplomasia na Utalii
Rais Samia ameeleza nia yake ya kufungua balozi za Tanzania katika miji ya kimkakati ili pamoja na kufanya kazi ya kujenga mahusiano ya kiuchumi zitumike kutangaza utalii katika nchi hizo, mkakati huu sio tu utaupaisha utalii wa Tanzania katika nchi husika lakini tutaimarisha diplomasia na diplomasia ya uchumi.

4. Kilimo& Uvuvi na Ufugaji
Mheshimiwa Rais ameweka mkazo katika maboresho makubwa yanayolenga kuinua sekta ya kilimo, sekta ya uvuvi na sekta ya ufugaji ili kuwaongezea tija wavuvi,wakulima na wafugaji.

kuongeza upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo,uzalishaji wa mbegu bora, mbolea, zana bora za kilimo,kuendelea kuimarisha vyama vya ushirika na skimu za umwagiliaji.

kuboresha sekta ya ufugaji, na kuimarisha sekta ya uvuvi kwa kununua meli za uvuvi.

Maboresho katika sekta hizi zinaonesha dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais Mama Samia kuipaisha heshima ya nchi kimataifa katika kilimo, uvuvi na ufugaji na pia kuimarisha upatikanaji wa bidhaa na mazao ya sekta tajwa katika soko la ndani.

5. Utawala bora
Mheshimiwa Rais ameahidi kusimamia na kuimarisha utawala, nidhamu serikalini, uwajibikaji na kuboresha maslahi ya watumishi wa serikali ikiwemo kuongeza mishahara na kupandisha madaraja kwa mujibu ya sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi wa watumishi katika utoaji wa huduma kwa wananchi lakini nidhamu ya watumishi wanapotekeleza majukumu yao.

6. Afya
Mheshimiwa Samia ameahidi kuendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kuendeleza ujenzi wa vituo vya afya, kuhakikisha upatikanaji wa madawa na kuajiri watumishi wa kada za afya katika vituo vya afya na zahanati.
Pia serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afyabkwa kila mwananchi kwa kuimarisha huduma za mfuko wa bima ya afya.

Tanzania imepata Mama ambaye kutoka moyoni anayo dhamira ya dhati kuhakikisha tunapiga hatua na kufika hatua sahihi ya maendeleo ya ndoto zetu kama Taifa, Mama mwenyewe ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama shupavu na hodari Samia Suluhu Hassan,ni jukumu letu kama wana wema wa Tanzania kumuunga mkono bila kujali tofauti zetu za vyama,itikadi wala dini,ili kumpa nafasi ya kutuongoza na kutufikisha kwenye mafanikio.

Ndimi
Christopher Bomola
Mkuranga, Pwani.
 
Karibuni kujisomea makala hii
 
Wale waarabu wa Dubai kutwa kucha wanapiga misele ikulu kumbe mko kwenye mipango ya kuwauzia nchi?? Mipango ya kipumbavu hiyo.

Acha waingie hiyo mikataba ya miaka 100 at their own risk, this is Africa. Akibadilika rais tu mikataba yote inawekwa mezani upya. Ndio watajua hawajui.
 
Back
Top Bottom