Tunaibiwa na VODACOM na Serikali inaangalia tu!

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,160
1,723
Wa Tanzania wenzangu mtandao wa vodacom unatuibia hela mchana kweupe bila kujali na hakuna popote tunapoweza kushtaki.
Huduma zao za kutuma pesa ni sawa na ujambazi wa kuvunja na kuingia kabisa sababu wanachukua hela yako halafu hawafikishi kwa mhusika na kukwambia kuna "tatizo la mtandao" na utajibiwa ndani ya wiki moja!!!

Hivi jamani ni haki kweli hii!!?? Serikali mko wapi kwenye hili? Hali ya uchumi ilivyo ngumu halafu bado mnaachia majambazi kama VODACOM wawaibie wananchi wenu mchana kweupe hivi?
Hela yangu mill 1 ikae huko kwa wiki nzima je ni hasara ya sh ngapi hio naypongia mimi? Je huyo mtu nayemtumia kwa ajili ya shida yake ya ugonjwa naye awasubiri nyie WIKI NZIMA!!!??

Acheni wizi wa kutumia hela zetu.kwa kigezo cha tatizo la kimtandao!! Kama tatizo ni mtandao kwanini huo mtandao haugomi kuchukua hela zetu ila unachukua vizuri halafu unakua na tatizo kwenye kutuma!?
 
Enough is enough aisee. Wanirudishie hela nisepe. Hata vihisa vyangu vikitoka nauza vyote. Na sishauri mtu yeyote ajihusisha na hili kampuni laki jambazi!
 
Wamesubir kibubu changu cha Mpawa kimejaa nataka kuhamisha ndio wanasema nikabadil kitambulisho shubaamit.
 
wapuuzi hao nilihamisha laki 2 toka benki mpaka leo sielewi nilipigwa danadana wao na benki kila mmoja anasema iko kwa mwenzake yaani ni ujinga mtupu
 
Kenya juzi wameipiga faini Safaricom kwa kupotea network masaa 2...Tz bado sana
 
Hivi hii ni kwa mitandao yote au voda tu?Maana ukitaka kuweka vocha kwenye voda inakataa wanasema haijawa teyari kwa kutumika,hivyo unapaswa usubiri usitupe vocha.
 
Si mtandao huo tu.. Mitandao yote ni wezi sana, licha ya Pesa ya kutuma hata hizi voucher dah aisee. Tunapigwa mno.. Pole mkuu kwa kukuvurugia mahesabu
 
Back
Top Bottom