Ushauri unatanguliwa na pongezi za kuhitimu elimu ya sekondari. Uwanja sasa ni wako, katika kujitimizia njozi zako za maisha na kutoa mchango wa maendeleo katika jamii inayokuzunguka. Maswali ya kujiuliza ni kuwa: je, unajiona wapi baada ya miaka mitano katika taaluma yako au baada ya kumaliza masomo ya chuo? Ni katika uwanja gani wa sanaa (arts) ambapo umetambua kipaji chako na shauku yako katika kutenda kazi? Tanzania inatoa fursa nzuri ya kujiendeleza kitaaluma, hata kwa waliomaliza kidato cha nne. Hata hivyo, usomaji wa sasa unakupatia fursa ya kujiwekea mkazo katika mambo unayohitaji kuyajua ili kusaida utendaji kazi wako baadaye (iwe ni kupitia ajira au kujiajiri). Usomaji, huku ikijipatia sambamba uzoefu wa kazi kwa masaa machache katika wiki au usomaji wa kozi za ziada/maalumu ikijijenga kitaaluma ni baadhi ya mifano tu. Mimi ninakutakia kila la kheri katika njia yako ya kutimiza ndoto na njozi zako