Pamoja na jitihada za kufufua viwanda kwa ajili ya rasilimali mbali mbali na juhudi za kuanzisha viwanda vipya, nimetafakari sana na kuona umuhimu wa kuwepo kiwanda muhimu cha kufinyanga akili za viongozi wetu hasa wa kitaifa .
Hiki kiwanda ni muhimu maana sasa taasisi za elimu hasa vyuo vikuu vimebainika kuandaa wale wanaoitwa "wapumbavu". Leo ni nwazi kuwa wasomi wetu wamesaliti wanyonge na kukimbilia tabaka tawala na mwishowe kuonekana sasa ni wapumbavu.
Viongozi wetu wa kitaifa wanahitaji kufinyangwa akili zao ili zisipoteze kumbukumbu kwamba jitihada za yote yanayofanywa yilitendwa na viongozi wa CCM hihi hii leo iliyopo madarakani. Ni Viongozi wa nchi waliotokana na CCM ndio waliharibu mikataba na kuruhusu upigaji wa ACCASiIA na makampuni mengine. Ni viongozi hao waliopitisha mikataba mibopvu na hewa na ndio walioruhusu huu unyonyaji kwa nchi yetu.
Hiki kliwanda kiwafundishe viongozi wetu maana ya utu na umoja wa kitaifa namna unavyopaswa kulindwa na kuenziwa. Kifundishe maana ya neno heshima, nidhamu na kutofautishwa na uwoga na uzandiki, chuki na kiburi ambavyo leo vimetamalaki.
Kiufupi hiki kiwanda kisisahauliwe hata kidogo.
Katika viwanda vyote hiki ni muhimu kuliko vyote.
Mungu ibariki Tanzania.