Viongozi wetu wajifunze dhima za mikutano

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,818
21,816
Nimeshangazwa na Viongozi wetu kutojua dhima ya mkutano au kusudio la mkutano wanaoshiriki. Mfano mzuri ni mkutano wa Leo pale Manyara Babati kwenye uwanja wa Tanzanite. Dhima kubwa ya mkutano ule au tuseme sherehe ile ilikuwa kumuenzi baba wa taifa, ila Viongozi wetu walikuwa tofauti na dhima hiyo.

Kwanza, mkutano wa Leo umegeuka kuwa mkutano wa kampeni, ambapo Viongozi na wapambe wao waliishia kumsifia Rais Samiah. Kwa mfano Mrisho Mpoto yeye na bendi yake wao wameenda mbali na kuimba wimbo wa 2025 tuna Jambo letu. Yani mkutano wa kumuenzi baba wa Taifa ,baadala watunge wimbo hata wa kumbukumbu wao wakawa wanaimba kumchagua Samiah 2025.

Pili, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, Wala hakugusia chochote kuhusu mwalimu , Bali alitoa pongezi kwa Rais Samiah na kutaja pesa walizopewa kwenye miradi ya maendeleo.

Kwa uchache , Viongozi wetu na wapambe wao wajifunze Nia na dhima ya mkutano au sherehe. Sio kila sehemu uchawa. Ni aibu Viongozi kutenga siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa , kutoa pesa za maandalizi , kushona sare na kujaa uwanjani bila kujua hasa wanachokifanya.

Kama mkutano ni wa kumbukumbu basi turuhusu kumbukumbu na kama mkutano ni wa mlkampeni basi kampeni ifanyike.
 
Back
Top Bottom