Tunahitaji jeshi huru la polisi

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Wadau siku zote nimekuwa nikiwasikia wanasiasa na watu wengi wakidai tume huru ya uchaguzi, wako sahihi lakini uchaguzi huu wa uliopita wa kata 43 nimejifunza kitu kipya tunahitaji kuwa na jeshi huru la polisi.

Kama inavyojulikana kwa nature ya jeshi huwa linapokea amri na kazi yake huwa ni kutekeleza, polisi kama binadamau wana roho na nyama lakini kulingana na nature ya kazi yao wanajikuta wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata maagizo hata kama maagizo hayo ni kinyume na sheria, utawala bora na haki za binadamu.

Kwa mfumo wa utawala tulionao wakuu wa polisi wako chini ya wakuu wa mikoa na wilaya ambao nia akina Bashite Mrisho Gambo n.k. Hawa watu wanapata nafasi hizi kwa ukada wa chama chao ccm. Wakati wa uchaguzi uliopita wakuu hawa walitoa amri haramu kwa polisi za kuwatoa wawakilishi wa vyama kwenye vyumba vya kupigia kura, kulinda waharifu waliokuwa wanapiga watu mapanga na hatimaye kilichotokea kila mmoja anakijua.

Polisi walifanya haya kwa kutekeleza maelekezo ya wakuu wa wilaya na mikoa ambao nao waliagiza hivyo kwa kuwa Magu aliwatishia kuwafukuza kazi kama upinzani utashinda katika sehemu zao na ndio maana mkuu wa mkoa wa Mbeya aliomba msamaha kwa jimbo moja kuchukuliwa na chadema, hii inatoa picha pasipo na shaka kwamba matokeo yanalazimishwa.

Kutokana na haya yote napendekeza tutafute namna ya kulifanya jeshi la polisi lifanye kazi professionally, liwe katika position ya kukataa amri haramu za wakuu wa wilaya na mikoa ambao ni makada wa ccm ambao wako tayari kufanya lolote hata kama ni kuua ilimradi chama chao kishinde uchaguzi.

Nawasilisha
 
Jeshi la polisi huru na wazalendo inahitajiwa...kuna kila sbb ya polisi kupewa au kupokea amri kutoka kwa wanasiasa...dc na rc ni wanasiasa
 
Jeshi huru la polisi ina maana CCM iondoke madarakani maana polisiCCM ndiyo oxygen ya CCM
 
Mtuache na jeshi letu, Mngejua tunalala nje kuwalinda nyie msingekuwa mnatusakama.
 
Mkuu katiba tu. Itaweka sawa kila kitu.
Katiba ndo hiyo wanaikataa, what can we do? Maana kama akina Mrisho Gambo wakati wa uchaguzi wanavaa mpaka mavazi ya chama bila aibu unategemea nini?
 
Back
Top Bottom