Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 186
Kuanzisha chama kipya si jawabu kwani tuna utitiri wa vyama na hakuna mabadiliko.
Well!
Watanzania wanatakiwa kuingia mitaani kila siku na mabango ya kudai changes na haki bila kuogopa kupigwa na Polisi. Kwa kufanya hivi mabadiliko na haki vitapatikana katika kipindi cha wiki moja tu
Where is the starting point? Nani anatakiwa astimulate that awareness kny mioyo ya Watanzania?
Uongozi wa chama hicho utatoka wapi? Ndani ya wapiganaji wa kambi ya upinzani (Slaa, Zitto) watakaojitoa huko? Au ndani ya wanaoitwa wapinga ufisadi ndani ya chama tawala (Mwakyembe, Kilango) watakaorudisha kadi? Je, kitakuwa na wapiganaji wa nje ambao majina yao halisi hatuyajui (Mwanakijiji, Rev Kishoka)?
Tupange safu ya uongozi wa chama hicho ambacho nadhani inabidi kiitwe Chama Cha Uhuru (CHACHU):
Mwenyekiti: Dk. Wilbroad Slaa
Katibu Mwenezi: Mzee Mwanakijiji
Mweka Hazina: Comrade Companero
Mzee Mwanakijiji,
Tatizo sio vyama bali ni watu, tatizo ni Watanzania ambao wengi ni wababaishaji, wezi, mafisadi.
Tunayoyasema hapa JF hatuyaamini kabisa.
Kama kuna watu wanataka kuleta mabadiliko, tayari tuna vyama vingi, ingieni kwenye hivyo vyama na anzeni mapambano kuanzia chini.
Hatuna muda wa kuzawazisha internal bickering za kina Chadema. NCCR Mageuzi kwanza ndio tuanze kazi ya mapinduzi ya kweli. Tunaitaji divai mpya katika viriba vipya. We need a frewsh start.
Chama ninachokifiria hakitafanana na chama chochote ambacho kipo sasa hivi; kimuundo, kiitikadi, kimwelekeo na kimfumo. Kitakuwa ni chama ambacho kinarudisha nguvu ya kutawala kwa wananchi wenyewe. Chama ambacho kitakuwa radical in its ideology, liberal in its pursuit of economic prosperity, and conservative in its application of the rule of law and justice. It will be an attempt to bring immediate and recognizable change in our society.
It will stand on certain principles that were the foundations of the building of our Republic. It will not be a mere creation of an idealist but a true manifestation of the reality of our ambition we have as a people. Believe me... change is coming.
Nadhani ni wakati wa kuchukua ile kadi sasa...
Uongozi wa chama hicho utatoka wapi? Ndani ya wapiganaji wa kambi ya upinzani (Slaa, Zitto) watakaojitoa huko? Au ndani ya wanaoitwa wapinga ufisadi ndani ya chama tawala (Mwakyembe, Kilango) watakaorudisha kadi? Je, kitakuwa na wapiganaji wa nje ambao majina yao halisi hatuyajui (Mwanakijiji, Rev Kishoka)?
Tupange safu ya uongozi wa chama hicho ambacho nadhani inabidi kiitwe Chama Cha Uhuru (CHACHU):
Mwenyekiti: Dk. Wilbroad Slaa
Katibu Mwenezi: Mzee Mwanakijiji
Mweka Hazina: Comrade Companero
Najiuliza kama kuna watu wameanza kuwa kama mimi; vyama vyote vya kisiasa vilivyopo nchini haviwezi kutupatia kile tunachohitaji kama taifa. Siyo CCM, CHADEMA, CUF au TLP ambacho kilivyo sasa kinaweza kuwa tumaini la Watanzania. Je kuanzisha chama kingine ambacho kitatoka kwa wananchi na chenye ajenda ya mabadiliko ya kweli na kikiongozwa na watu wenye mwelekeo wa mabadiliko na wasiogopa political confrontation na ambacho hakitasita kufanya what is necessary to restore law and order and a constitutional rule kitaweza kuwa na nafasi.
Chama ambacho mrengo wake itakuwa ni kuhakikisha kuwa hakuna kuremberiana macho na mafisadi tena wala kuufafanua ufisadi bali kuushughulikia moja kwa moja.
Chama ambacho kitalenga kuleta mabadiliko ya kimfumo na kimuundo wa serikali yetu ndani ya miaka mitano ya kuingia madarakani kikibeba ajenda ya mabadiliko ya kweli (kikatiba, kisiasa, na kiutendaji) huku kikiwashughulikia kama simba mkali wale wote ambao wamelifikisha taifa letu hapa ikiwemo kutaifisha mali zao, kuwasweka jela na wale ambao ni vigogo wa ufisadi "kunyongwa" kama wanavyofanya huko China!
Chama ambacho hakitawabembeleza wawekezaji kama wakwe zetu!
Au ndiyo tubanane mumu kwa mumu huku tukiulizana "kajamba nani'!
Lets hope hakitaanzishwa na kuhodhiwa na wanaopenda umimi, wenye kupenda kusifiwa kila wanachokifanya, wasiokimbilia ajenda kwa ajili ya umaarufu, wasiopenda kujishabihisha na MWalimu kwa nia ya kupata uhalali na wanafiki wengine wenye kupiga kelele wakiwa njelakini wakifunguliwa mlango tu kushiba harufu za ulaji wanabadilika hata lugha...na rangi pia
omarilyas
inaonekana una matatizo na watu wengi sana ambao ungependa wawe utakavyo... ukiangalia hivyo unavyovisema unaweza kukuta wapo wengi tu wenye sifa hizo kwenye vyama karibu vyote vilivyopo sasa. Ndio maana tumehitaji chama kipya.